Makapuku Forum

Makapuku Forum

| Victorien Adebayor:
.
“Sio rahisi mashabiki kuonyesha kitu kama kile hasa unapokwenda kwao, hii ni upendo mkubwa na heshima kwangu nami nawatakia kila la kheri huko mbele naamini watafanikiwa zaidi.
.
“Bado tunazungumza na Rais wa Simba hatujafikia hatua ya kukubaliana lakini kila kitu kinakwenda vizuri hakuna shida,” - amesema Adebayor [via Mwanaspoti]
Screenshot_20220405-173159_Instagram.jpg
 
Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa sababu za bei za mafuta kupanda ni pamoja na mgogoro wa kivita uliopo kati ya nchi ya Urusi na Ukraine na kupelekea kuwepo na uhaba wa upatikanaji wa mafuta duniani pia imepelekea gharama za mafuta na za usafirishaji mafuta kupanda.

Mkurugenzi wa Petroli wa Mamalaka hiyo Gerald Maganga amesema bei zilizotangazwa leo zitakazoanza kutumika kesho zimezingatia gharama zote halisi za mafuta ikiwa ni pamoja na ada ya mafuta ya shilingi 100 ambayo ilikuwa imesitishwa kuanzia mwezi December mpaka March.

Mafuta yanayopokelewa katika bandari ya Dar es Salaam kwa Petrol imepanda kutoka shilingi 2540 kwa lita kwa mwezi ulipita hadi shilingi 2861 kwa lita ikiwa ni ongezeko la shilingi 321. Kwa mafuta ya diesel yanayopita bandari ya Dar es Salaam yamepanda kutoka shilingi 2403 kwa lita mwezi uliopita hadi 2692 ikiwa ni ongezeko la shilingi 289.

Screenshot_20220405-182131_Instagram.jpg
 
Simba S.C ya Tanzania itacheza na Orlando Pirates ya South Africa katika robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo endapo Simba watafanikiwa kuwatoa Orlando Pirates watakutana na mshindi kati ya Al Ittihad na Ahli Tripoli zote za Libya.

Simba SC kutokana na kumaliza nafasi ya pili katika Kundi sasa itaanza kucheza nyumbani April 17 2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa na marudiano ni April 24 2022
Screenshot_20220405-182340_Instagram.jpg
 
Baada ya Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Msimbati iliyopo Wilaya ya Mtwara Mkoani Mtwara, Taufiq Hamisi Kuandika barua ya kuacha Shule kwa Mkuu wa Shule akidai anataka kufanya shughuli za uvuvi, hatimaye Taufiq amepata ufadhili wa masomo katika Shule ya Sekondari Ocean, iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani na amekubali kurudi Shule.

Ufadhili huo uliotolewa na Taasisi ya Kalamu Education Foundation kwa Kushirikiana na Shule ya Sekondari Ocean, unahusisha ada ya masomo na mahitaji mengine muhimu ya Shule, Kuanzia kidato cha kwanza hadi Chuo Kikuu, Meneja wa Shule hiyo, Juma Nchia amesema ufadhili huo unalenga kusaidia Wanafunzi wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali na kushindwa kuendelea au kuanza masomo yao.

Nchia amesema kuwa mbali na Taufiq, pia msaada huo umemnufaisha Mwanafunzi mwingine Issa Mohamed Abdallah kutoka Ruangwa Mkoa Wa Lindi, aliyeshindwa kuanza kidato cha kwanza na kuamua kwenda kuchimba madini kutokana na hali duni ya Familia yake "Taufiq na mwenzake wameahidi kusoma kwa bidii"
Screenshot_20220405-182554_Instagram.jpg
 
Polisi nchini Afrika Kusini wanamsaka Mwendesha toroli la mizigo la super market ambaye ameonekana kwenye video akiwa ndani ya toroli hilo huku akiwa ameshikilia lori la mafuta lililokua kwenye kasi katika moja ya Barabara kuu nchini humo.

Mwanaume huyo alionekana akitabasamu na kuwapungia mkono watu waliokuwa ndani ya magari ambapo kitendo hiki cha hatari kimesababisha Polisi wamtafute Mwanaume huyu atafikishwa mbele ya sheria hivi karibuni.
Screenshot_20220405-182809_Instagram.jpg
 
Polisi Mbeya wanamshiklia Mwanamke aitwaye Riziki Henry (22), Mkazi wa Nditu wilayani Rungwe katika Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za mauji ya Mume wake Ayubu Aron(33) ambaye alimuua kwa kumpiga na kitu butu kichwani kisha kumchoma na kitu chenye ncha kali kisogoni baada ya Mwanamke huyo kuulizwa na Mumewe kwanini karudi nyumbani usiku.

RPC wa Mbeya Ulrich Matei amesema tukio hilo la mauaji lilitokea April 2 katika kijiji cha Nditu ambapo baada ya kupigwa Aron alipelekwa ya Hospitali Wilaya ya Rungwe (Makandana) lakini akafariki siku hiyohiyo.

"Tayari mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Rungwe kwa ajili uchunguzi wa kitabibu, Mtuhumiwa alikamatwa na upelelezi wa shauri hilo unaendelea na baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani"

Wakina kalumbu njooni mumuone ndugu yenu huku
Screenshot_20220405-182918_Instagram.jpg
 
Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa sababu za bei za mafuta kupanda ni pamoja na mgogoro wa kivita uliopo kati ya nchi ya Urusi na Ukraine na kupelekea kuwepo na uhaba wa upatikanaji wa mafuta duniani pia imepelekea gharama za mafuta na za usafirishaji mafuta kupanda.

Mkurugenzi wa Petroli wa Mamalaka hiyo Gerald Maganga amesema bei zilizotangazwa leo zitakazoanza kutumika kesho zimezingatia gharama zote halisi za mafuta ikiwa ni pamoja na ada ya mafuta ya shilingi 100 ambayo ilikuwa imesitishwa kuanzia mwezi December mpaka March.

Mafuta yanayopokelewa katika bandari ya Dar es Salaam kwa Petrol imepanda kutoka shilingi 2540 kwa lita kwa mwezi ulipita hadi shilingi 2861 kwa lita ikiwa ni ongezeko la shilingi 321. Kwa mafuta ya diesel yanayopita bandari ya Dar es Salaam yamepanda kutoka shilingi 2403 kwa lita mwezi uliopita hadi 2692 ikiwa ni ongezeko la shilingi 289.

View attachment 2176871
Moto huu unawaka kote kote. Huyu boya Putin hafai [emoji16][emoji16]
20220402_202321.jpg
 
UNAAMBIWA
Kwa mujibu wa sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 Nchini Tanzania, Wazazi wanapotengana au kuachana ipo dhahania ya kisheria kwamba kwa maslahi mapana ya Mtoto ikiwa Mtoto huyo ana miaka isiyozidi 7 basi ni vyema akaishi na Mama yake huku Baba yake akitakiwa kutoa huduma ya matunzo.
Screenshot_20220405-183519_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom