Makapuku Forum

Mashabiki nchini Algeria wakiwa kwenye mchakato wa kujipatia tiketi kuelekea mchezo wa marudiano wa Play Off kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Cameroon kesho.

Algeria ina faida ya goli moja baada ya kushinda 1-0 ugenini.
 
Bodi ya nidhamu ya CAF imemfungia kwa miezi 12 kutojihusisha na soka ofisa wa RS Berkane Majid Madrane kwa kitendo cha kuingia uwanjani na kushinikiza wachezaji na maofisa wa Berkane kumshambulia mwamuzi wa mechi yao dhidi ya Simba iliyofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Berkane wamepigwa faini ya dola 100,000 kutokana na kitendo hicho cha ofisa wao Majid Madrane na wakati huohuo RS Berkane imepigwa faini ya dola 8000 kutokana na mashabiki wao kuwarushia chupa wachezaji wa Simba katika mechi iliyochezwa iliyochezwa nchini Morocco.

[
@EliaBennet]
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Kichekesho wallah
 
Mwigizaji Will Smith amemuomba msamaha Chris Rock baada ya kumpiga kibao katika jukwaa la ugawaji wa Tuzo za Oscar akisema tabia yake haikubaliki na haina udhuru "Ningependa kukuomba msamaha hadharani, Chris, nilivuka mpaka na nilikosea"

Haya yanajiri baada ya Chuo cha filamu cha Oscars kilimlaani Smith juu ya tukio hilo na kutangaza kwamba inatathmini marekebisho rasmi, Smith alimpiga kibao Rock jukwaani baada ya Mchekeshaji huyo kufanya utani kuhusu Mke wa mwigizaji huyo, Jada Pinkett Smith.

Rock alimtania Jada Smith kwa kunyoa nywele, baaada ya kuzipoteza kutokana na hali inayofahamika kama alopecia, muda mfupi baadaye Smith alishinda tuzo yake ya kwanza ya Oscar kutokana na uigizaji wake kama Baba wa wachezaji nyota wa tennis Venus na Serena Williams katika filamu ya King Richard.

"Vurugu njia zote ni sumu na uharibifu, mwenendo wangu wa jana usiku katika Tuzo haukubailiki na hauna udhuru, utani ni sehemu ya kazi lakini mzaha kuhusu hali ya kiafya ya Jada ulikuwa mzito sana kwangu kuvumilia kihisia."

Smith amemuomba msahamaha Rock moja kwa moja, akisema alivuka mpaka pia ameomba msamaha kwa Chuo na familia ya Williams "Ninajuta sana kwamba tabia yangu imetia doa safari ambayo imekuwa ya kupendeza kwetu sote"
 
Watu sita wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya gari (fuso) lenye namba T 239 AFB walilokua wakisafiria kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo katika eneo la barabara ya Soni/Mombo wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Akizungumza na @ayotv_ kwa njia ya simu RPC wa Tanga, Safia Jongo amesema ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo March 29,2022.

Aidha Kamanda Jongo amewataka Watumiaji wa vyombo vya Moto mkoani humo kuendelea kufuata sheria,kanuni na taratibu za usalama barabarani.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto na majeruhi wapo Hospitalini hapo wakiendelea kupata matibabu.
 
Jesus!! Ajali hizi jamani
 
Sipendi violence ila hapa Smith alinifurahisha
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…