Makapuku Forum

Makapuku Forum

SHERIA 17 ZA MCHEZO WA SOKA
Screenshot_20220323-163152_Instagram.jpg
Screenshot_20220323-163224_Instagram.jpg
Screenshot_20220323-163257_Instagram.jpg
Screenshot_20220323-163328_Instagram.jpg
Screenshot_20220323-163406_Instagram.jpg
 
Hawa Orlando Pirates wamedhamiria msimu huu, mechi tano kwenye makundi Shirikisho Afrika, wamepiga mabao 15

Hii ni rekodi ya mabao kwenye hatua ya makundi mpaka hivi sasa msimu wa 2021/22

Kuna uwezekano Wazulu wakatisha zaidi msimu huu?
Screenshot_20220323-163916_Instagram.jpg
 
Ligi zikiwa zimesimama kupisha mechi za kimataifa za kalenda ya FIFA, huu hapa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania na misimamo ya ligi 5 barani Ulaya.
Screenshot_20220323-164041_Instagram.jpg
Screenshot_20220323-164106_Instagram.jpg
Screenshot_20220323-164126_Instagram.jpg
Screenshot_20220323-164147_Instagram.jpg
Screenshot_20220323-164240_Instagram.jpg
Screenshot_20220323-164319_Instagram.jpg
 
Shirikisho la soka nchini Guinea (FGF) limethibitisha kuwa kiungo wao Naby Keita ameondolewa katika timu ya taifa kuelekea katika mchezo wa kirafiki siku ya Machi 25 dhidi Afrika Kusini kutokana na majeraha ya goti, taarifa zinazodaiwa kuwa Keita amekataa kujiunga na timu ya taifa Guinea hazina ukweli wowote.
Screenshot_20220323-164556_Instagram.jpg
 
Ni rasmi sasa mechi ya Mshindi wa EURO 2020 ambaye ni Italia atakipiga na bingwa wa COPA AMERICA 2021, Argentina, mechi hiyo ikitambulika kama Finalissima

Mchezo huo utapigwa Juni mosi mwaka huu kwenye dimba la Wembley, Uingereza huku ikilenga kujenga mahusiano kati ya Amerika Kusini na Ulaya, huu ukiwa ni mchezo wao watatu

Mara ya kwanza ilikuwa 1985 na ya pili ni 1993 huku fainali yao ikijulikana kama Artemio Franchi Trophy
Screenshot_20220323-164728_Instagram.jpg
 
Imeandikwa na @swalehmawele

Hata katika maisha ya kawaida wapo watu ambao wanafanya mambo makubwa au kutengeneza ramani ya mafanikio lakini mwisho wa siku hawaonekani kama mashujaa, ni vile tumeamua kutowatazama kwa jicho la tatu.

Pichani ni Tyron Damons kocha wa makipa wa Simba, raia wa Afrika Kusini aliezaliwa miaka 44 iliyopita na uzoefu wake wa kufanya kazi katika klabu za TS Galaxy, Bidvest, Mbabane, Chippa United unamrahisishia kuchora ramani nzuri ya Simba katika eneo la magolikipa.

Bila ya kumkosea heshima Milton alietimkia Yanga, bila shaka aliifanya kazi yake ipasavyo na Damons anaendeleza yale mazuri yaliyoachwa na mtangulizi wake, fundi mzuri anahitaji malighafi sahihi ili kusimamisha jengo imara.

Tunaposifu ubora wa Aishi Manula tukumbuke kuwa nyuma yake kuna hiki chuma ambacho kinampiga msasa na hatimae tunamuimba kama shujaa, Manula wa sasa hana errors nyingi ambazo tulikuwa tukiziona misimu kadhaa ya nyuma, hiyo maana yake amekuwa coached vizuri.

Utasikia kauli huko kwenye vibanda umiza, ah! ile save hata mimi nafanya maana mpira umemgonga tu, guys huko kumgonga mpira maana yake alikuwa sehemu sahihi katika wakati sahihi na lazima umpe credit kwa hilo.

Mtazame Manula pale golini, achana na saves zake kisha tazama movement ambazo anazifanya anapojiandaa kuzuia shambulizi, hizo ndizo zinazomrahishia kufanya saves na haya mambo yanaanzia mazoezini, mazoezini kuna nani? yupo Tyron Damons.
Screenshot_20220323-164854_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom