Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220323-154212_Instagram.jpg
 
Inaelezwa Pablo amepanga kumuomba kocha wa Stars awaondoe wachezaji wake kwenye mpango wake kutokana na kuwa na muda mfupi wa kujiandaa na mchezo wa mwisho wa Kombe la Shirikisho Afrika.
.
WADAU mnasemaje __!!
Screenshot_20220323-154354_Instagram.jpg
 
YANGA WANAWAZA KIKOSI CHA KIMATAIFA MSIMU UJAO
.
Yanga katika dirisha dogo msimu huu iliwapiga chini Ramadhan Kabwili, Ditram Nchimbi na Adeyun Saleh na bado Uongozi umekili kuwa na idadi kubwa ya wachezaji ambao mikataba yao inamalizika lakini hilo haliwapi shida kwani walio kwenye mipango yao watawaongeza.
.
Huyu hapa Mjumbe wa kamati ya usajili ya Yanga, Hersi Said amesema;
.
“Ni kweli tuna idadi kubwa ya wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwisho wa msimu. Hatukurupuki kuongeza watu mikataba kama unavyoona malengo yetu sasa ni taji, hivyo kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi tunatakiwa kuwa na mastaa ambao watatubeba kwenye michuano hiyo.”

……………..
Screenshot_20220323-154522_Instagram.jpg
 
Cavani Kutua Inter
.
Mabingwa wa Italia, Inter Milan wanataka kumsajili straika wa Manchester United na Uruguay Edinson Cavani, 35, ili awe mbadala wa staa kutoka Chile, Alexis Sanchez, 33, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.
.
Cavani amekuwa hapati nafasi ya kutosha kikosi cha kwanza cha Man United msimu huu. Mkataba wa Cavani unaisha mwisho wa msimu huu.
Screenshot_20220323-154639_Instagram.jpg
 
Kinda wa Spain anayekipiga Barcelona, Pedri Gonzalez amepewa rasmi jezi namba 10. Umri wake ni miaka 19.
Screenshot_20220323-154754_Instagram.jpg
 
Utabiri wa Mesut Ozil msimu huu ::
.
Bingwa EPL — MAN CITY
Bingwa UCL — LIVERPOOL
Bingwa World Cup — ENGLAND
Screenshot_20220323-155053_Instagram.jpg
 
Wote viungo punda, yupi unamkubali sana hapo::
.
A: Joshua Kimmich
B: Casemiro
C: Ng’olo Kante
.
Screenshot_20220323-155200_Instagram.jpg
 


Profesa mmoja kwenye chuo cha mpira pale Johan Cruyff jijini Barcelona aliwauliza Wanafunzi wa regular classes, aliuliza “What are the timer indicators for being a Champion”

Alitaka tu kujua viashiria vya timu kuwa bingwa, ilikuwa ni Homework kwa wanafunzi wake ambao wengi walikuwa ni Wachezaji wa zamani ambao sasa wanataka kuwa Maafisa wa mpira

Mwanazuoni wa kwanza alisimama na kujibu, UNPREDICTABILITY SIR, yes ni kama ambavo Yanga haitabiriki, hujui wataingia kwa mfumo gani na kwa wachezaji gani kwenye mechi husika

Uliwahi kutabiri tu kuwa Farid Mussa atacheza beki ya kushoto?? Uliwahi kuhisi tu kuwa Kibwana Shomari angecheza kulia na kushoto?? Uliwahi kuhisi Dickson Job atacheza kati na pembeni? The answer is NO

Viashiria moja wapo vya kuwa bingwa ni kuwa huwapi watu nafasi ya kutabirika, hujulikani utakujaje kwenye mazingira gani

Mwanazuoni wa pili alijibu, UNCERTAINTY SIR! Akimaanisha kutopewa uhakika ama kutoaminiwa, yani unaenda kutwaa ubingwa mpaka dakika ya mwisho watu bado hawaamini

Iliwahi kutokea kwa Lille pale France, Leicester pale England, hata ule msimu Liverpool anabeba ubingwa, watu walikuwa na nadharia nyingi sana kuwa Liver habebi ila hatimae alibeba

Ndicho unachoona kwa Yanga hivi sasa, ilianza mara pumzi, mara wataumia wachezaji, mara raundi ya pili ila mpaka sasa gari linawaka tu, hakuna kupumzika hajapoteza

Mwanazuoni wa mwisho alimaliza, EMMANUEL SIR! Darasa sote likashangaa, Emmanuel!? Kivipi?? Tafsiri ya Emmanuel ni Mungu pamoja nasi, YES wakati mwingine ni bahati njema huleta ubingwa

Mnakumbuka Liverpool na maamuzi ya VAR? Manchester City na VAR? Au bao la jioni la Aguero? Ama Real Madrid na kamba za Ronaldo? Basi ndivyo kama Yanga, inafika wakati kila kitu kinakuwa upande wako na unakuwa bingwa mteule! EMMANUEL

Ikifikia hapo basi sio Wanadamu tena ni Mungu tu maana Yanga kashinda sehemu nyingi ambazo hatukutarajia

Walimaliza Wanafunzi na Profesa akawapigia makofi, akasema “Today lets end here, we will continue tackling more problems tomorrow concerning this case” WABHEJA SANA
Screenshot_20220323-155407_Instagram.jpg
 
Na @EmanuelMwayomboJr

Sultan Mehmed II (Mehmed the conqueror) wa Ottoman Empire aliwahi kusema, siku zote kitu kizuri kinajiuza chenyewe wala huwezi kutumia nguvu kubwa kujitangaza kama unafanya vizuri katika kazi yako. Timu ya Wananchi Young Africans Sports Club msimu huu inajiuza yenyewe kutokana na ubora wake ndani ya kiwanja.

Young Africans Sports Club ndiyo timu Bora msimu huu hadi sasa katika ligi kuu ya Soka Tanzania Bara kwa sababu performance yao ndani ya kiwanja imezungumza hadi hii Raundi ya 18 hawana mpinzani.

Yanga wanacheza kitimu zaidi na wanapambana vilivyo ndani ya kiwanja msimu huu hakuna timu yoyote iliyopambana katika ligi zaidi yao hivyo hadi sasa wana stahili kuvaa medal ya Ubingwa wa ligi mwishoni mwa msimu huu.

Taji la ligi kuu Tanzania Bara (NBC PREMIER LEAGUE) Lipo mkononi mwao Wananchi washindwe wao tu kwa sababu wana kila sifa ya kuwa mabingwa msimu huu, Yanga wamevuna alama tatu hata katika Mechi ambazo unahisi watapoteza.

Siku zote Bingwa huwa anakutana na vikwazo vingi na akaibuka mbabe. Mechi ya Polisi Tanzania, Geita Gold, Mtibwa Sugar na KMC zimetuonyesha kwamba Yanga hawatanii msimu huu kila mchezaji akiwa ndani ya kiwanja anaamini yeye ni mshindi.

Kwa Upande wangu hadi sasa Yanga ndo timu Bora ya msimu huu na Nabi ndiye kocha Bora wa msimu huu kwa sababu ameifanya Yanga kuwa timu ya Ushindani na inacheza soka la kuvutia ambalo kwa miaka mingi mashabiki wa Klabu hii walikuwa wanaliota na hawakufanikiwa kulicheza ila chini ya Nasraddine Nabi wameweza kucheza kandanda safi linalovutia machoni kwa wadau wa kandanda.
Screenshot_20220323-162738_Instagram.jpg
 
Tangu Kim Poulsen ameichukua Taifa Stars timu inaonekana, hata kama tunashindwa tunaona tumeshindwa kwa sababu wenzetu wametuzidi sio kama zama zile kila tukiingia kwenye mechi tunajua tutapigwa.

Sasa hivi timu inaonekana inashindana na inaandaliwa kwa ajili ya kushindana.

- Alex Luambano
Screenshot_20220323-163021_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom