Siku za watu wengi kushare akaunti zao za Netflix zinaweza kufikia mwisho, Netflix inajaribu mfumo mpya wa kuwadhibiti wenye akaunti za msingi wanaoruhusu akaunti zao kutumiwa na Watu wengine wa nje ili kushughulikia ushiriki haramu wa neno la siri.
Uzinduzi wa jaribio hilo utawafanya Wamiliki wa akaunti za msingi za Netflix kulipa ada ya ziada, ikiwa hujui sheria na masharti ya Netflix, akaunti ya Mteja huenda isishirikiwe na Watu binafsi wasiokuwa karibu na nyumbani kwao.
Sasa, Netflix imekuwa ikiwaruhusu Watu kuteleza kwa miaka kadhaa kwa kushare neno la siri, lakini ripoti zinaonyesha kuwa kampuni hiyo imekuwa ikijaribu mfumo huu tangu mwaka jana.
Kampuni ilifanya majaribio machache yaliyowashawishi watumiaji kuweka kitambulisho cha akaunti zao kama njia ya kuwashawishi wasio na akaunti kulipia akaunti zao wenyewe, jaribio lijalo litazinduliwa nchini Chile, Costa Rica, na Peru. Mkurugenzi wa Uvumbuzi wa Bidhaa wa Netflix, Chengyi Long, alisema kampuni hiyo itawaruhusu wanachama kushiriki akaunti kwa urahisi na kwa usalama wakati wakilipa kidogo zaidi.
View attachment 2154481