

Farhan Jr
SIMBA NA HADITHI YA KUNUNUA UKWELI
Wakati Barcelona ipo kwenye kiwango bora sana chini ya Pep Guardiola, Media zote duniani ilisifia sana na kupongeza soka lile, hakuna sehemu ambapo Barcelona ilikuwa haitajwi
Wakati Manchester United ama The Famous United ipo katika ubora mkubwa wa Class of 92 kila Mtu aliipa sifa, kila Media iliitaja United lakini ni tofauti na sasa
Wakati Yanga ya Kampa Kampa tena ipo kwenye ubora wake chini ya Yusuph Manji kila Mtu aliisifia, Media zilicover sana story za Yanga na nchi iliimba Yanga, kutokana na ubora
Sasa hivi kwa zaidi ya miaka mitano, Tanzania na Afrika inaitaja Simba sio media za ndani tu mpaka nje na CAF wanatoa mileage ya kutosha sana, kwa zaidi ya misimu minne hivi sasa
Tafsiri yake ni kuwa unapewa sifa au pongezi sio kishkaji bali kwakuwa kuna kazi umefanya, ukiharibu Media hazitobaki, ni mpaka urejee tena kileleni watu watakupa sifa zako
Kuna wakati unaweza kuhisi Simba inatajwa sana! Lakini je haistahili? Kuna wakati unahisi wachezaji wa Simba wanatajwa sana je hawastahili?
Bingwa wa Tanzania bara kwa misimu minne ni Simba, huyo Simba ndie anapeperusha bendera ya Tanzania kwa misimu mitano hivi sasa, unahisi ni sifa za kubumba?? Jibu ni HAPANA
Huyu Pape Ousman Sakho kusifiwa ni kosa?? Top quality goals kuanzia CCM Kirumba mpaka Taifa, kuanzia FA mpaka Shirikisho Afrika! Unahisi Media Zinakosea?
Mfano tu nikikaa redioni kuongea wakati Sakho kafunga mbili Afrika, kisha Mshikaji wangu huko Ifakara kafunga nne kombe la Mbuzi, nikitulia na stori ya nyumbani Ifakara kwa dakika 10 utanielewa?
Media hazijawahi kumkataa Mtu, timu wala Taasisi! Ila uhalisia upo field, ukifanya vizuri unazungumzika kirahisi mnooo!
Mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema “We dont cover by favour but we cover on MERIT”
Ukiwa kwenye ubora wako hata ukigusa jiwe litakuwa mkate