Mpira wa Afrika una mambo mengi sana, ndio maana kwasasa timu nyingi zimeacha kulalamika bali kucheza mpira na kuwekeza kwenye mpira
Simba wanafanyiwa mengi sana ugenini ila wao wamechagua kuacha kulalamika na kuwekeza kwenye mpira, wakipageuza kwa Mkapa sehemu ngumu mtu kucheza
Kwa Madiba wale Mamelodi Sundowns walizuia mpaka Bus la Al Ahly lisipite, wanajua sio sahihi ila ndio fitna za soka la Afrika, kushinda mchezo haiwi tu ndani ya uwanja
Kabla ya kulalama na kuisema vibaya Simba ambayo haihusiki na maamuzi ya Marefa, jaribu kuvuta picha nao huwa wanafanyiwa mangapi nje ya nchi? Ni vile tu wameacha kulalama na kuamua kucheza mpira