Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mweeh
Screenshot_20220209-125054_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Real Madrid chenye Wafanyakazi takribani 50 ambao kila Mtu ana majukumu yake, kazi yao kubwa ilikuwa kuleta maudhui bora kwa Mashabiki wa Real Madrid

Hii ilikuwa Mei 27, 2018! Ni mandhari ya joto kidogo na jua limeanza kuzama Jijini Kiev, siku moja kabla ya fainali ya UEFA kati ya Real Madrid na Liverpool

Wakati wanafanya mazoezi ya kupiga mashuti, nyuma ya goli walikuwepo Wanahabari wakitazama mazoezi hayo ya mwisho, kila Mtu camera yake ikiwa on standby

Wakati pia macho na masikio ya Wanahabari ni kwa Legends wa Madrid kama Christian Karembeu, Claude Makelele, Alberoa, Roberto Carlos na The Prince of Madrid Raul Gonzalez “El Capitano”

Mpiga picha mmoja wa klabu anaitwa Raul Sanz, aliiweka vyema camera yake waliopewa kutoka kwa Kampuni ya Canon tawi la Concha Espina, Madrid! Tayari kwa ajili ya kupiga picha bora ya maisha yake

Cristiano Ronaldo akiwa amevalia vyema viatu vyake vya Mercurial Vapor Superfly CR7 Chapter 7 brand ya NIKE, alipokea pande zuri kutoka kwa Kocha Zinadine Zidane na golini alikuwepo Kaylor Navas Gamboa

Ronaldo alitumia mguu wake wa kushoto kupiga mpira uliopewa jina la ADIDAS FINALE 18’ ambao ndio ulitumika kwa ajili ya fainali, hakuna aliejua huu ndio mpira wake wa mwisho mazoezini na hatokuwepo hapo tena

Sanz aliwajaza vyema kwenye frame wachezaji wote wa Madrid, akamvuta vyema na Marcelo ambaye alisimama nyuma kabisa wakati Swahiba wake anapiga, akijua siri fulani kubwa kati yao

Ilikuwa picha ya mwisho Ronaldo akiwa mazoezini jioni ile, ilikuwa kama chakula cha mwisho cha Massih Issa bin Mariam na Wanafunzi wake! Hakuna aliefahamu zaidi ya hisia kali za mpiga picha Sanz

Inasalia kuwa picha bora zaidi ya vizazi na vizazi kwa Madridistas! The last supper

Picha ni siri kubwa sana, picha ni kumbukumbu kubwa sana, picha ni maagano kati ya mpigaji na camera yake! Mpe tano Mwanao mpiga picha
Screenshot_20220209-125306_Instagram.jpg
 
Ukimsikiliza Haji Manara, utagundua maelezo yake yote yamelala kwenye timu mbili tu [Simba na Yanga] na hapo ndipo huwa naamua kupuuza malalamiko au kumbukizi kama hizi.

Tukiwa wakweli, sio Simba na Yanga peke yake ambazo zinanufaika au kuathirika na baadhi ya makosa ya waamuzi. Unapokuja mbele na hoja zako za timu mbili pekee huwezi kusema ni kwa ajili ya manufaa ya taifa wala timu ya taifa.

Ukiachana na matatizo ya waamuzi, hivi vilabu ndio vinaongoza kwa kuwa na wachezaji wengi wa kigeni, hivi vilabu vingine ndio tuna vitegemea kuzalisha wachezaji wenye ubora kwa ajili ya timu ya taifa.

Simba wamenufaika lakini Yanga wamenufaika pia na makosa ya waamuzi, vilabu vyote hivi kwa pamoja vimenufaika dhidi ya vilabu vingine ila sio walipokutana wao kwa wao. Kwa hiyo kutoka mbele kwa kuzifanya Simba na Yanga ndio kilelezo cha kuathirika au kunufaika kwa baadhi ya maamuzi hautendei haki mfumo mzima wa Ligi.

Lakini kama kuna matukio ya maamuzi tata yanatokea kwenye mechi ya Polisi Tanzania dhidi ya Namungo na timu moja wapo ikanufaika halafu hausemi, basi usiseme unaipigania haki ya Ligi.

Ukweli ni kwamba, waathirika wakubwa wa maamuzi si Simba na Yanga. Vilabu vingine ndio havipati faida ya vinapocheza na timu hizi mbili lakini hata vikilalamika nani anasikiliza?

- Nicasius Agandwa
Screenshot_20220209-125817_Instagram.jpg
 
Mkaguzi wa Polisi, kutoka Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Mkoa wa Kipolisi Temeke, Tumaini Swilla ambaye ni shahidi wa upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake amesimama ghafla na kueleza hajisikii vizuri wakati akihojiwa na wakili wa utetezi Peter Kibatala leo Jumatano February 9, 2022

Mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo

Kibatala: Kwa sababu nimekupeleka katika eneo specific la hela? Sasa nenda katika maelezo ya Urio, halafu soma.

Shahidi amepewa maelezo ya Urio, yaliyoandikwa na Mkaguzi Tumaini Swila.

Kibatala: Kwa hiyo tunakubalia hapo Julai 22, 2020 Urio alitumiwa fedha kiasi Sh 199,000 na Mbowe kupitia wakala kwa ajili ya kuwapa Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya kwenda Dar

Shahidi: Ndio.

Kibatala: Je fedha hizo zinaendana na zile ulizosoma awali, ambazo Bwire na Moses Lujenje? Ambazo walitumia Sh 87,000.

Shahidi: Zinaendana.

Kibatala: Sasa naomba unijibu swali langu, hizo 87,000 walizopewa Bwire na Moses Lujenje kama ajili ya kwenda Moshi, zilikuwa ni shilingi ngapi.

Wakati Kibatala akiendelea kumhoji shahidi.

Ghafla shahidi amesimama na kueleza kuwa hajisikii vizuri
Screenshot_20220209-130258_Instagram.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemuapisha Dk Angeline Mabula kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mkuu huyo wa nchi amemuapisha Dk Mabula leo Februari 9, 2022 katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Awali Dk Mabula ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa naibu waziri wa wizara hiyo, aliteuliwa kuwa Waziri Januari 8 mwaka huu baada ya Rais Samia kufanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Dk Mabuala ameapishwa leo kutokana na kutokuwepo wakati wa uapisho wa mawaziri Januari 10 mwaka huu.
Screenshot_20220209-130425_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom