Golikipa wa Misri, Mohammed Abou Gabal amezua gumzo baada ya kutumia chupa inayosemekana ina michoro ya wachezaji na aina yao ya upigaji penalti iliyomsaidia kuokoa penalti 6 katika michuano ya Afcon 2021 ikiwemo ya mchezaji bora Sadio Mane.
MTIBWA YAIPELEKA YANGA MANUNGU
.
Kama Wananchi walijipanga kwenda kuangalia timu yao ikicheza dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, mambo yamebadilika, badala yake itapigwa Manungu.
.
Mwenyekiti wa Mtibwa Sugar, Abubakar Nassor amethibitisha jambo hilo, kwamba mechi hiyo itapigwa uwanja wa Manungo, mkoani Morogoro.
YANGA YAWEKA MILIONI 230 KWA MORRISON
.
Inaelezwa kuwa vigogo wawili matajiri wa Yanga wamemuahidi Morrison Ofa nzito ya dola 100,000 (Sh230 Milioni) kama ada ya usajili tu endapo atakubali kurejea Jangwani.
.
Mbali na dau hilo mshahara wake ameahidiwa dola 8000 (Sh 18 Milioni) sawa na kiasi ambacho analipwa kiungo wa Simba Clatous Chama sasa aliporejea Msimbazi.
KIBABAGE: MSIISHIE KUSEMA WAZAWA TUMEFELI CHANGAMOTO NI NYINGI
.
Nyota wa Tanzania, Nickson Kibabage anayekipiga KMC, amesema miongoni mwa sababu kubwa iliyomfanya arejee nchini kutoka klabu ya Difaa el Jadidi ya Morocco timu aliyowahi kuichezea Simon Msuva ni Ubaguzi wa rangi.
.
“Kuna muda unavumilia hadi unaona inatosha, wenzetu ni wabinafsi sana ila wengi wa mashabiki zetu hawalijui hili hivyo kubaki na kauli ya mchezaji fulani kashindwa huko ughaibuni,” amesema Kibabage na kuongeza;
.
“Ilifika mahala unakuta wanaogelea sehemu kisha nawe unajiandaa kuungana nao ila ukiingia tu unaona wachezaji wote wanatoka wanakuacha mwenyewe, yaani unabaki na maswali mengi yasiyokuwa na majibu hivyo mwishoni nikaona inatosha.”
Rais wa Senegal Macky Sall ametangaza kuwa leo Jumatatu February 07,2022 ni siku ya mapumziko kitaifa ili Watu washerehekee ushindi wa Timu ya Taifa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) walilolibeba jana.
Rais Sall amefuta pia safari ambayo alitarajiwa kuifanya nje ya Nchi ili awakaribishe Mabingwa hao Ikulu kesho Jumanne "Tumeongoja ushindi huu kwa miaka 60"
Watoto wawili wa Familia moja wamefariki dunia Mkoani Tabora kwa kukosa hewa chanzo kikitajwa kuwa ni moto uliowashwa kwenye jiko la mkaa ndani ili kujikinga na baridi wakiwa wamelala, Watoto waliofariki ni Amani Athumani, (1) na Zainabu Athumani (1).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao amesema tukio hilo limetokea February 5, 2022 majira ya saa 6 usiku katika kijiji cha Usubilo kata ya Ifucha manispaa ya Tabora ambapo moto ulisababisha Watoto hao kukosa hewa ya kutosha.
Baba wa Watoto hao Athumani Shabani (45), Mkewe Magreth Joseph (34) pamoja na Neema Athumani (17) wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete kutokana na kuathirika kwa kukosa hewa pia kulikosababishwa na jiko hilo la mkaa na hali zao sio nzuri
Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali umeridhia na kupitisha ombi la Tanzania la kutaka Kiswahili kuwa lugha ya kazi katika Umoja huo, Dkt. Mpango amewasilisha ombi hilo la lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha za kazi katika mikutano ya Umoja wa Afrika.
Dkt. Mpango ameongeza kuwa Kiswahili ni miongoni mwa lugha za kiafrika zenye wazungumzaji wengi barani Afrika ambapo takribani watu milioni mia moja wanakitumia Kiswahili pamoja na wazungumzaji kutoka nje ya Bara la Afrika.
Kutokana na umuhimu wa lugha hiyo Makamu wa Rais amesema tayari inatumika katika jumuiya mbalimbali ikiwemo jumuiya ya Afrika Mashariki ,Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na kufundishwa kwa lugha hiyo katika nchi nyingi za Afrika Mashuleni.
Amesema tayari Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni limetangaza tarehe saba Julai ya kila mwaka kuwa siku ya maadhimisho ya lugha Kiswahili Duniani, Mkutano huo pia umeichagua Tanzania kuwa mjumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU)