Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,977
Watu watatu waliokuwa wakisafiri kutoka Kata ya Nzera kuelekea Geita Mjini wakitumia gari la abiria (hiace) wamefariki dunia papohapo na wengine 8 kujeruhiwa baada ya gari lao kugongana na Lori katika eneo la Pori la Mgodi wa GGM Wilayani Geita Mkoani Geita.
Akithibitisha uwepo wa miili hiyo iliyopokelewa katika chumba cha dharura Katika Hospitali ya Mkoa wa Geita Kaimu Mganga Mfawidhi katika Hospitali hiyo, Paschal Thumba amesema walipokea miili hiyo ya Watu 3 huku wengine wakipewa rufaa ya kupelekwa Bugando jijini Mwanza.
Jitihada za kumtafuta kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Geita zinaendelea ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.