Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20211224-064804_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20211224-064844_Opera%20Mini.jpg
 
Watoto wa England changamoto zao ni nyingi sana

Phil Foden na Jack Grealish wiki iliyopita walipigwa picha wakiwa klabu ya usiku kinyume na sheria

Ikisemekana Pep Guardiola amechukizwa sana na kitendo cha Vijana hao
Screenshot_20211224-192159_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

Nyota wa Simba, Peter Banda ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Malawi 'The Flames' kuelekea AFCON 2021 nchini Cameroon

Kikosi hicho kimesafiri kuelekea nchini Saudi Arabia ambapo kitaweka Kambi yao ya mwisho kabla ya kutua nchini Cameroon

Peter Banda Bado yupo nchini Tanzania, ambapo leo wapo Tabora watakipiga dhidi ya KMC ila tayari Shirikisho la soka nchini Malawi limetuma email kwenda Simba

Ombi la The Flames ni kuwa Peter Banda anapaswa kupanda Ndege usiku wa Jumapili hii kuelekea Mashariki ya kati kujiunga na wenzake kambini

Simba watatoa majibu baada ya mchezo wa leo kuhusu Banda kuondoka mapema, ila inatazamiwa kuwa watamruhusu Kijana aende mapema
Screenshot_20211224-192717_Instagram.jpg
 
LEWANDOWSKI:
.
“Naheshimu kazi kubwa anayofanya Cristiano Ronaldo. Kwa Messi kila kitu kinaonekana rahisi. Nadhani Cristiano amefanikiwa kwa kujituma sana.”
.
Je, nani mkali zaidi Messi au Ronaldo?
.
“Tangu nilipoanza kuwa profesheno, Messi na Ronaldo wamekuwa juu ya kila mtu. Siku zote imekuwa ni vita baina yao. Na sasa kuwashindanisha inakuwa ni kesi ya mchezaji gani unayempendelea. Jibu la swali nani zaidi ni gumu.”
Screenshot_20211224-193413_Instagram.jpg
 
GAUCHO KATUA ZAKE MBEYA KWANZA FC
.
Mbeya Kwanza wameamua kuwatema wachezaji sita kwa mpigo kisha kuongeza majembe mengine matano akiwamo kiungo fundi wa zamani wa Simba, Abduhalim Humud ‘Gaucho’.
.
Gaucho amesaini mkataba wa miaka miwili akitokea Namungo aliyoichezea msimu uliopita, huku waliotemwa kuyapisha majembe hayo mapya ni pamoja na Mohamed ‘Mo’ Rashid, Jaffar Mohammed, Elisha, Kerenzo, Ramadhan Kimata, Rajabu Kaumbu na Abdallah Makangana.
.
Mwenyekiti wa Mbeya Kwanza, Mohamed Mashango amesema wamekamilisha usajili wa nyota watano hadi sasa kwenye dirisha hili la usajili si Humud (Gaucho) tu wengine ni; Habib Kiyombo, Abubakar Abbas, Yusuph Jamal na Onana Junior.
Screenshot_20211224-193519_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

Kila nchi duniani Ina kitu kinaitwa Utamaduni, itakuja mifumo, itakuja mbinu na Kila Mabadiliko ya sayansi ya mpira ila utamaduni ni ule ule

Mfano Real Madrid miaka mingi waliamini Nahodha wao lazima awe Mhispania, ni mara chache Nahodha kutoka taifa lingine mfano sasa

Barcelona wanaamini Midfield yao inahitajika damu kutoka La Masia, piga uwa, lazima Mido moja wapo awe kapita kwenye shule yao ya soka

Kama ilivyo kwa Manchester United na damu za England, wanaamini ni sehemu muhimu kwa Mtoto wa England kucheza, ndio maana Beckham kutoka London alisafiri mpaka North East kucheza Manchester

Kama ilivyo kwa Waarabu na utamaduni wao mfano Al Ahly wanaamini sana kwenye damu zao, wanaamini sana baadhi ya maeneo uwanjani ni yao, kutafsiri mpira wao

Hata pale atakapokuja Mtu kutoka nje ya utamaduni wao sio rahisi kudumu kwa muda mrefu au kupewa uzito mkubwa! Ila hili limekuwa tofauti kwa Mwamba kutoka Mali, Aliou Dieng

Msumari huu unazidi kulitawala dimba na kutakatisha mioyo ya wahafidhina! Kutoka eneo la Kiungo na moyo wa Ahly ndipo alipo Fundi wa Mali aliegomewa kwenda kucheza soka Ulaya

Waarabu lazma wakubali Kuna mechi ilikuwa inapigwa kati ya Fabrice Ngoma na Aliou Dieng, ilikuwa ni Derby ya Wabantu ndani ya Ardhi ya Waarabu

Kuna muda Kuna Utamaduni na Kuna muda Kuna uhalisia
Screenshot_20211224-193725_Instagram.jpg
 
Watu 89 wamegundulika kuwa na dalili za maradhi ya Uviko-19 wakiwemo madaktari na wauguzi wa hospitali ya rufaa Mnazimmoja Visiwani Zanzibar.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Dk Marijani Msafiri leo Desemba 24, 2021 wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu hali ya ugonjwa huo.

Amesema wagonjwa hao ni miongoni mwa watu 143 waliofanyiwa kipimo cha Uviko 19 kuanzia Desemba 16 mwaka huu hadi leo.
Alisema kati ya wagonjwa 89, wafanyakazi, madaktari na wauguzi wa hospitali waliopatikana na Uviko-19 ni 38.

“Katika wafanyakazi hao hakuna hata mmoja aliyelazwa maana hawana dalili kubwa za kulazwa, bali wanaendelea na matibabu na kupewa mapumziko ya muda mfupi kulingana na hali zao,” amesema Dk Msafiri
Screenshot_20211224-194142_Instagram.jpg
 
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza kurejesha rasmi darasa la saba katika mfumo wa elimu ya msingi.

Sera ya elimu ya mwaka 2006 inaelekeza elimu ya Msingi ya miaka sita kuanzia darasa la kwanza mpaka darasa la sita.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Simai Mohamed Said amesema leo Ijumaa Desemba 24, 2021 kwamba lengo la kuishia darasa la sita ilikuwa ni kumuwezesha mwanafunzi kupata fursa za elimu ya maandalizi, msingi na sekondari akiwa na umri mdogo.

“Kutokana na mabadiliko mbalimbali na mikakati ya maendeleo nchini pamoja na changamoto tofauti zinazoikabili sekta ya elimu, Wizara imeona ipo haja ya kufanya tathmini kwa kina na kuzipatia ufumbuzi wa kudumu changamoto hizo.
Screenshot_20211224-194241_Instagram.jpg
 
Wakati mamia ya wananchi wakiendelea kuhangaikia usafiri katika Kituo cha mabasi cha Magufuli eneo la Mbezi Luis, jijini Dar es Salaam, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) imetoa sababu za kutotoa vibali kwa mabasi madogo (coaster) mwaka huu.

Latra imesema haijatoa vibali hivyo kwa sababu ya fujo zinazofanywa na wamiliki hao, ikiwamo upangaji holela wa nauli.

Imezoelekea kila mwisho wa mwaka, Latra hutoa vibali kwa magari hayo ili kupunguza adha ya usafiri kutokana na ongezeko la abiria linalokuwepo.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Gilliard Ngewe alisema msimu huu hawatatoa vibali kwa magari madogo, kwani yamekuwa chanzo cha fujo na yamekuwa yakijipangia nauli yanavyotaka baada ya kupewa vibali.
Screenshot_20211224-194409_Instagram.jpg
 
Mahakama ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro imemuhukumu mkazi wa Kitongoji cha Majengo Kata ya Hedaru, Elitumain John Elitumain (31) kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 12.

Akitoa hukumu hiyo leo Ijumaa Desemba 24, 2021 hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya hiyo, Mussa Hamza amesema mtuhumiwa alifikishwa mahakamani hapo akiwa na kesi ya kumbaka binti huyo ambaye alikuwa mfanyakazi wa kazi za ndani nyumbani kwa mtuhumiwa huyo.
Screenshot_20211224-194538_Instagram.jpg
 
Club ya Yanga SC imemtambulisha rasmi kiungo Salum Aboubakar maarufu ‘Sure Boy’ kama Mchezaji wake mpya huku Yanga wakiita zawadi ya mapema ya Christmas.

Sure Boy anajiunga na Yanga SC baada ya kuondoka Azam FC aliyodumu nayo kwa miaka 14 kuanzia mwaka 2007 mpaka mwaka 2021.
Screenshot_20211224-194711_Instagram.jpg
 
Zaidi ya Watu 20 wamejeruhiwa kwenye ajali ya basi kampuni ya Hokka’s iliyotokea leo baada ya Basi hilo kuacha njia kwenye eneo la daraja eneo la Misungwi Mwanza, wakati AyoTV na millardayo.com zikisubiria taarifa ya Polisi kuhusu ajali hii, Mashuhuda wamesema hakuna kifo chochote kilichotokea kwenye ajali hiyo.
Screenshot_20211224-194929_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom