

Farhan Jr
SIMU YA PROFESA LIGI YA TANZANIA
Ukikaa vijiweni utasikia haiwezekani Simba kubeba ubingwa mara tano mfululizo kivyovyote! Kwanini iwe dhambi? Kwanini kama ana uwezo asichukue?
Profesa anasema hii ni sumu iliyojengwa ambayo mwishowe tutaona mengi ya kutisha, tutaona mengi ambayo hayapo sawa kwakuwa ni dhambi Mnyama kuondoka na tano
Ni ugonjwa wa kidunia, mara nyingi binadamu ana tabia ya kukinai! Huenda watu wamekinai ubora wa Simba, huenda watu wanataka bingwa mpya! Mind you watu wanachukia CONSISTENCY
Profesa anasema "One thing about football is not about football" yani kitu kimoja kuhusu mpira wala hakihusu mpira, kuna vitu vya nje ya mpira vinaathiri mpira duniani kote
Profesa anasema, suala la waamuzi duniani kote ni kupita hatua kwa hatua! Unaweza kuchezesha ligi ya mabingwa mikoa, ukaja Daraja la pili kisha Championship na baadae Ligi kuu
Mna uhakika Waamuzi wetu wanapita kwenye ranks zote? Mna uhakika wana uzoefu wa kutosha? Mtakuja tena kuhoji kwanini Waamuzi wengi hawachezeshi michuano ya Afrika? Majibu mnayo
England hawakuwa na Mwamuzi yoyote WORLD CUP 2018, Walisema wazi hawakupeleka jina la Michael Oliver kwakuwa wanaona hajakidhi, je huku kwetu nani anaassess, je yupo fair? Tujiulize
Profesa anamaliza kwa kusema! Mnapoona Viongozi wanafukuza Makocha bila kuogopa basi mjue wanajua Ushindi unapatikana vipi! One thing about football is not about football
Professor