UKIZINGUA YANGA INAKULA KWAKO
.
Uongozi wa Yanga umesisitiza msimu huu una jambo lao na kwamba hawana muda wa kubembeleza mchezaji, kama akipigiwa simu halafu asipokee au akikosa mechi ajue namba inachukuliwa na wengine.
.
Hayo yamewekwa wazi na mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Hersi Said alipokuwa akihojiwa ambapo alisema hawana nafasi ya kumbembeleza mchezaji kama atashindwa kufuata matakwa na miongozo ya timu kwa sasa kikosini.
.
“Nyie si mmeona kuna mchezaji juzijuzi alifunga bao akamwaga machozi, si mmeona wenyewe. Hakuna anayetaka kupoteza nafasi yake kikosini,” alisema Hersi.
.
“Yanga inalipa mishahara yenyewe. Ina mifumo yake ya kuajiri watu sisi tunasapoti tu. Yanga ni timu kubwa huwezi kufananisha na wengine. Huwezi kumleta mchezaji kama Bangala (Yanick) halafu hajui mshahara analipwa na nani.”
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.