Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wanawake wanene wenzangu mpooooo. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Screenshot_20211108-143240_Instagram.jpg
 
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania imetangaza kuongezeka kwa vipindi vya joto nchini Tanzania ambavyo vitaendelea hadi December 2021 huku mtawanyiko wa mvua ukitarajiwa kuongezeka vilevile mionzi ya jua la utosi ikiondoka, Meneja wa kituo kikuu cha utabiri Samwel Mbuya amesema uwepo wa jua la utosi tropiki ya kaprikoni huja na vipindi vya joto kali na hujirudia tena mwezi February wakati jua la utosi likielekea tropiki ya kansa.

"Viwango vya joto vimeongezeka kwa kiwango kikubwa sana na baadhi ya maeneo Nchini yameripoti kiwango cha nyuzi joto zaidi ya kile cha kawaida katika mwezi November mfano mkoani Kilimanjaro joto limefikia nyuzi joto 36.4 ikiwa ni ongezeko la nyuzi joto 4.6 kutoka kiwango cha kawaida cha wastani, maeneo mengine ukanda wa Pwani hali ndio kama hivyo zimeongezeka kwa takribani nyuzi joto 2.2 mpaka 4.6 juu ya kiwacho cha kawaida"

"Kwa eneo hili la ukanda wa Pwani pia kuna changamoto ya kwamba tupo karibu na bahari kwahiyo viwango vya unyevunyevu kutoka kwenye bahari vinakua vipo juu na hivyo kusababisha kuwepo kwa hali ya fukuto ambayo inaongeza hali ambayo tunaipata sasa hivi ya joto katika maeneo ya mikoa hii ya ukanda wa Pwani" ——— Samwel Mbuya kutoka TMA.
Screenshot_20211109-040637_Instagram.jpg
 
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Urua chini kwenye Kijiji cha Mfuruashe Wilayani Rombo Augustino Moshi (37) anadaiwa kumuua Mke wake aitwae Atanasia Augustine Moshi (31) kwa kumkatakata na kitu chenye ncha kali na kisha yeye mwenyewe kujinyonga kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa Polisi Kilimanjaro Simon Maigwa amesema Mwanaume huyo ambae alikua Mshereheshaji maarufu kwenye sherehe mbalimbali (MC) anadaiwa kufanya tukio hilo majira ya saa kumi na mbili alfajiri ———> “uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo ni mgogoro wa kifamilia wa muda mrefu ambao umesababishwa na wivu wa kimapenzi"
Screenshot_20211109-040814_Instagram.jpg
 
Mfadhili wa zamani wa Klabu ya Simba, Azim Dewji amesema ameamua kutumia Tsh. milioni 20 kununua Tshirt atakazozigawa kwa Vijana 2000 watakaoishabikia Timu ya Taifa ya Tanzania vs DRC Congo katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia.

Dewji ameyasema hayo leo na kuwataka Watanzania na Wadau wa soka kushirikiana kwa pamoja kuiunga mkono Taifa Stars katika mchezo huo utakaochezwa Novemba 11, 2021 na kuongeza kuwa atazikabidhi jezi hizo kwa TFF ambapo watazigawa kwa vijana hao 2000 ambao wataenda uwanjani kushabikia, pia atatoa tiketi 100 kwa ajili ya Wafanyakazi wake kwenda uwanjani.

"Tubadilike hii ni Timu yetu hatuombi pesa maana Waziri Mkuu ameshakusanya pesa na amepata za kutosha na Mama naye amesema ana imani na Timu, tumebakia sisi Wapenzi na Mashabiki kwamba lazima na sisi tuige na tufate yale yaliyozungumzwa na Viongozi wetu, tunaomba siku ya alhamis tuwape ruhusa Watanzania wakaishabikie Timu yetu"
Screenshot_20211109-040935_Instagram.jpg
 
Wakili wa Mwanaume aliyewauwa Waumini 51 wa Kiislamu katika shambulio baya kwenye Misikiti miwili mjini Christchurch, New Zealand, amesema mteja wake anafikiria kukata rufaa dhidi ya kifungo cha maisha alichopewa, akisema alishinikizwa kukiri makosa baada ya shambulio hilo la mwaka 2019.

Wakili huyo Tony Ellis, amesema Mteja wake amemfahamisha kuwa alikiri makosa baada ya kupitia visa vya udhalilishaji wakati akisubiri kuanza kwa kesi yake.

Ellis ameyawasilisha malalamiko hayo Mahakamani na uchunguzi umeanzishwa dhidi ya shambulizi hilo kujua iwapo mchakato unaostahili ulifuatwa katika uendeshwaji wa kesi hiyo.

Brenton Tarrant mwenye miaka 31, mwaka uliyopita alihukumiwa kifungo cha maisha bila ya uwezekano wa msamaha baada ya kukutwa na hatia ya kuwaua Waumini hao 51 wa Kiislamu na jaribio la kuwaua Waumini wengine 40 katika shambulio lililofanyika tarehe 15 mwezi Machi mwaka 2019 lililosemekana kuwa baya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.
Screenshot_20211109-041057_Instagram.jpg
 
Serikali ya Tanzania imeanza majadiliano kati yake na Kampuni za Shell, Equinor, Pavillion, ExxonMobil na Ophir kuhusu mradi wa gesi (LNG) Lindi utaogharimu shilingi za kitanzania Trilioni 70 ambapo Waziri wa Nishati January Makamba baada ya kufungua majadiliano hayo amesema mradi huo utabadilisha taswira ya uchumi wa Tanzania ——— "tutatoa taarifa wiki zijazo fursa zitakazopatikana wakati wa utekelezaji"
Screenshot_20211109-041427_Instagram.jpg
Screenshot_20211109-041447_Instagram.jpg
Screenshot_20211109-041506_Instagram.jpg
 
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetangaza kuanza kwa mgawo wa maji katika Mkoa Dar es Salaam unaosababishwa na upungufu wa maji Mto Ruvu, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam leo na kusema Mamlaka imeandaa utaratibu wa kuhakikisha hakuna Mwananchi anapata shida ya ukosefu wa maji licha ya uwepo wa mgao huo.

“Kwa sasa hali ya Mto Ruvu kwa majuma mawili bado iko palepale ambapo kina cha Mto kiko katika mita 1.5 hadi 1.8, kwa upande wa Ruvu Juu kina kipo mita 16 hadi 18, hivyo hali ya Mto imeendelea kuimarika, kabla ya changamoto ya kiangazi, Mamlaka huwa inazalisha lita Milioni 520 kwa siku, kwa sasa tunazalisha lita Milioni 460 kwa siku, hivyo upungufu wa maji upo kwa asilimia 12" ——— Mtendaji Mkuu DAWASA, Mhandisi Luhemeja.

Mhandisi Luhemeja ameongeza kuwa kutokana na ukubwa wa mtandao wa DAWASA, Mamlaka imetoa ratiba ya migao wa upatikanaji wa huduma ambazo zitatolewa kwa Wananchi kupitia mifumo ya kimawasiliano ya Mamlaka katika ofisi za Mikoa ya kihuduma——— "Lengo la kuwa na mgao ni kuhakikisha kila Mwananchi anaendelea kupata maji kwa uwiano"

Mtendaji Mkuu amefafanua kuwa maeneo ambayo hayataathirika na mgawo huo ni pamoja na eneo la Kisarawe, Chalinze, Pugu, Bagamoyo, Oysterbay,
Masaki, Mikocheni, Ikulu, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Kikwete (JKCI) na Soko Kuu la Kariakoo.
Screenshot_20211109-041655_Instagram.jpg
 
Polisi Mkoani Pwani wamesema wanamtafuta Mzee Charles Tulaona Mtweve (67) Mkazi wa Kijiji cha Mafizi Kata ya Gwata Wilaya ya Kisarawe ambaye alitoweka nyumbani kwake November 04,2021 akiwa na wenzake wawili kwenda kuwinda katika pori la Kijiji cha Sungura Morogoro Vijijini na hadi sasa hajulikani alipo.

RPC wa Pwani, Waknyo Nyigesa amesema ———"Mzee Charles akiwa na silaha yake (Shortgun Greener) akiwa amefuatana na Meshack Mkemi (50) na Juma Athmani (40) walikwenda kuwinda na baada ya kuwaua nguruwe pori wawili waliamua kurejea Kijijini Mafizi lakini Charles Mtweve hakufika nyumbani na hadi sasa hajulikani alipo"

"Polisi kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Dola vinafanya ufuatiliaji wa wapi Mzee huyo alipo, kwa Mtu atakayemuona Mzee Mtweve apige simu namba 0712538830 au 0786024709"
Screenshot_20211109-041852_Instagram.jpg
 
Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa limesema kwamba idadi ya Watu walio hatarini kutumbukia kwenye baa la njaa katika Mataifa 43 imeongezeka hadi Milioni 45, wakati njaa ikiongezeka kote ulimwenguni.

Shirika hilo la WFP limesema kwamba idadi hiyo iliyokuwa Milioni 42 mwanzoni mwa mwaka, imeongezeka kutokana na Watu wengine Milioni tatu wanaokabiliwa na njaa nchini Afghanistan.

Mkurugenzi Mtendaji wa WFP David Beasley amesema sababu kuu za ongezeko hilo ni mizozo, athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na njanga la COVID-19.

WFP imesema gharama ya kuepusha njaa duniani inafikia Dola Bilioni saba, kutoka Dola Bilioni 6.6 iliyokadiriwa mwanzoni mwa mwaka, WFM imesema ufadhili uliozoeleka hautatosha tena.
Screenshot_20211109-042519_Instagram.jpg
 
Wananchi ya Mtaa wa Iduda Kata ya Iziwa jijini Mbeya wamelazimika kubomoa makazi yao wao wenyewe ili kutii agizo la Mkuu wa Wilaya, Dk. Rashid Chuachua kwa lengo la kupisha mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata.

Licha ya kubomoa nyumba zao wao wenyewe, Wananchi hao wamelalamikia kutolipwa fidia ili kupisha eneo hilo.

DC Chuachua amesema ni kweli ametoa agizo hilo na kusema eneo hilo tangu mwaka 1983 limetengwa kwa ajili ya shughuli za kijamii na suala la fidia hawapaswi kulipwa kabisa ——— "tunavyo vielelezo vyote vya eneo hilo na hakuna aliyeonewa sasa wanapaswa kupisha mradi ambao utakuwa chachu kwa Watoto wao kupata elimu bora na eneo hilo idadi kubwa yalikuwa ya wazazi wao"

Chuachua amesema kaya zinazopaswa kuondoka kwenye eneo hilo ni tano na sio 25 kama baadhi ya Wananchi hao wanavyodai.
Screenshot_20211109-042800_Instagram.jpg
 
Licha ya kuwa na mlima mrefu barani Afrika na misitu mikubwa Kilimanjaro ndio mkoa unaoongoza kwa joto kali kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA).

“Katika kipindi hiki viwango vya joto vilivyoripotiwa katika maeneo mbalimbali ni vikubwa ambapo mkoa wa Kilimanjaro uliripoti kiwango cha juu cha joto kilichofikia nyuzi joto 36.4 sawa na ongezeko la nyuzi joto 4.6 ukilinganisha na wastani wa muda mrefu kwa mwezi Novemba.

Vilevile, kiwango cha juu cha joto katika mkoa wa Dar es salaam kimefikia nyuzi joto 33.8 sawa na ongezeko la nyuzi joto 2.2 wakati katika mkoa wa Ruvuma kimefikia nyuzi joto 34.4 sawa na ongezeko la nyuzi joto 4.3”.
Screenshot_20211109-043041_Instagram.jpg
 
Watu watano wa familia moja wamefariki dunia baada ya nyumba waliyokuwemo kuteketea kwa moto katika mtaa wa Mandela uliopo Igoma Mashariki jijini Mwanza.

Akizungumza kwa njia ya simu na Mwananchi Digital, Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoani humo, Ambwene Mwakibete amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Mwakibete amesema kuwa moto huo umetokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu Novemba 8, 2021.

"Ni kweli waliofariki ndani ni Lameck Benedicto, mke wake, mtoto wake wa kike na wageni wake wawili ambao bado majina yao hayajatambulika," amesema Mwakibete
Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia Mwananchi.
Screenshot_20211109-044343_Instagram.jpg
 
Fikayo Tomori amekuwa kwenye msimu bora sana AC Milan na hata alivyokuwa Chelsea

Kiujumla kacheza mechi zaidi ya 47 bila kufanya makosa binafsi yaliyopelekea bao

Lakini Gareth Southgate wa England amemtema na ameenda na Tyron Mings

Screenshot_20211109-044656_Instagram.jpg
 
Nyota wa Benfica ambaye ni raia wa Brazil, Everton Cebolinha amepigwa faini na klabu yake baada ya kufanya mahojiano na chombo kimoja cha Habari nchini kwao Brazil

Kwenye mahojiano yake anasema alipata tabu sana kuwaelewa Wareno namna wanavyoongea maana wanaongea kwa haraka sana

Yani Brazil na Ureno wote wanazungumza Kireno ila yeye kasema Wareno wanaongea haraka hawaeleweki
Screenshot_20211109-045002_Instagram.jpg
 
Maisha mapya ndani ya Camp Nou yameanza, ni rasmi Xavi Hernandez ametambulishwa siku ya Leo

Mashabiki walijitokeza uwanjani na Rais Joan Laporta ndie aliemkaribisha Kijana wake

Barcelona mpya yenye matumaini mapya, ataweza kuvunja mfupa??___View attachment 2003764
Screenshot_20211109-045420_Instagram.jpg
 
Kama Hersi Said ndiye Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM na ndiye mwenye sauti kubwa baada ya Ghalib, anakuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga na anahusika kwa kiasi kikubwa katika shughuli za uendeshaji, pengine kuliko hata Ofisa Mtendaji Mkuu, basi hapo kuna tatizo.

Pengine tatizo laweza kuwa ushiriki wa wafanyakazi au watu wenye madaraka ya juu katika kampuni ya GSM, kujihusisha pia na klabu moja katika shughuli zote kubwa, wakati ndio wenye maamuzi makubwa katika kampuni zao. Vile vile hatuwezi kupuuzia kauli yake kwamba Yanga isipotwaa Ubingwa aulizwe yeye.

- Almas Kiganyi.
Screenshot_20211109-045803_Instagram.jpg
 
Serikali yatoa msimamo wake GSM kudhamini timu zaidi ya moja
.
Suala hilo limetolewa ufafanuzi na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa, amesema:
.
"Ukiachilia mbali TFF pia tuna baraza la Michezo (BMT) ambalo lipo karibu katika kusimamia sheria hizo, hivyo sioni na wala wananchi wasiwe na shaka katika hilo kwani kama kutatokea ukiukwaji wowote hawatasita kuchukua hatua kwa muhusika" amesema Waziri huyo.
.
Pia Bashungwa amesema katika suala hilo la udhamini wa GSM watu wasitie shaka nalo kwa kuwa kama ni sheria za mpira zipo, hivyo endapo kutaonekana kuwa na mambo tofauti wahusika watawajibishwa.

……………..
Screenshot_20211109-045926_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom