Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20211106-062802_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20211106-062821_Opera%20Mini.jpg
 
Tunafurahi kumtangaza Pablo Franco Martín kuwa Kocha Mkuu wa timu yetu.

Taarifa zaidi kuhusu Kocha @pablofrancomartin inapatikana kwenye Simba App. #NguvuMoja

Nyieee njooni mumuone kocha wetu nawakumbusha tu huyu alipita Madrid
Screenshot_20211106-202719_Instagram.jpg
 
Kocha mpya wa Simba, Pablo Franco anakuja kurithi mikoba ya Didier Gomes alieondoka kwa makubaliano ya pande zote mbili

Kocha huyo ana miaka 41 na ni raia wa Hispania, ambaye pia amepita Real Madrid kama Kocha Msaidizi
Screenshot_20211106-202719_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

Nimekuwekea picha tatu za Kocha mpya wa Simba, Mhispania Pablo Martin katika harakati zake za Ualimu wa mpira wa miguu

FRAME 1- NEYMAR JR NA KOCHA WA SIMBA

Hapo kipindi hicho alikuwa anafundisha Getafe klabu ya Ligi Kuu nchini Hispania! Hapo alikabiriana na Barcelona dume ya MSN (Messi, Suarez na Neymar)

Huu ulikuwa msimu wa 2014/15! Getafe walipoteza mchezo pale Nou Camp lakini hii ni CV kubwa ya Kocha! Kupambana na Barcelona iliyobeba ubingwa wa UEFA Msimu huo wa 2014/15

FRAME 2- DIEGO SIMEONE NA KOCHA WA SIMBA

Mchezo huo ulikuwa wa La Liga! Ni Getafe dhidi ya Atletico Madrid kwenye dimba la Vicente Calderon! Hapo ilikuwa kabla ya mchezo wakisalimiana

Kumbuka hii ilikuwa Atletico Madrid dume iliyotoka kucheza fainali ya UEFA dhidi ya Real Madrid dume chini ya Carlo Ancelotti! Lakini huyu Kocha alicheza nayo kwenye Ligi Kuu!

FRAME 3- WACHEZAJI WA REAL MADRID NA KOCHA WA SIMBA

Hii picha ni msimu wa 2014/15 baada ya dakika 90 pale Santiago Bernabeu ambapo Kocha aliingia kusalimiana na wachezaji baada ya mchezo na kuwapungia Mashabiki

Kumbuka hii ilikuwa Real Madrid chini ya King Carlo Ancelotti ambae alitoka kutwaa nao UEFA, nae pia akiwa amefanya makubwa barani Ulaya, ila yeye alicheza nao

FRAME 4- ZINADINE ZIDANE NA KOCHA WA SIMBA!

Niwakumbushe tu kuwa kwenye mechi za Vijana, Zinedine Zidane alikuwa na timu ya Real Madrid Castilla na Kocha wa Simba alikuwa na Getafe B

Mechi iliisha kwa Getafe kuondoka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Castilla ya Zizzou yenye Mastaa Kama Martin Odegaard, Fede Valverde na mafundi wengi kikosini

Mkumbuke mafanikio yake GETAFE B ndio yalimpeleka GETAFE A na alipoondoka timu ya Getafe ikaenda mikononi mwa Escriba alietoka Elche!

CV nzuri na imeshiba let’s wait and see the football

Screenshot_20211107-065227_Instagram.jpg
Screenshot_20211107-065149_Instagram.jpg
Screenshot_20211107-065250_Instagram.jpg
Screenshot_20211107-065344_Instagram.jpg
 
Takwimu za Kocha mpya wa Simba sc, Pablo Franco Martin. Alivyokuwa alikihudumu kibarua chake kama Kocha mkuu wa vilabu tofauti tofauti Barani ulaya katika Nchi ya Hispania.

lets hope he will cope up with African football...?!

@mpira_takwimutz_
Screenshot_20211107-070047_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

Kuna kitu kimoja kuhusu United! Nacho ni Sir Alex Ferguson, ana heshima kubwa sana pale na bahati mbaya amekuwa akisimamia anachokiamini bila kujali nyakati

Fergie kuendelea kutaka OGS awe Kocha ni kutaka influence yake iendelee kutawala, bado anataka kuitwa Boss na anahitaji Kocha ambaye atalitambua hilo, ni ngumu yeye kupendekeza jina la mtu Kama Antonio Conte

Kuna kitu kimoja kuhusu Kocha wa Manchester United, bado hajui anataka nini, akifeli mfumo mmoja anakimbia na kucheza mwingine, bado hajui yupo bora sehemu gani, anajitafuta misimu yote

Klopp alijenga timu kwa mfumo unaoleweka jumlisha na pressing, Pep pia na City yake alisimamia kile anachoamini! Ila United Leo ni 3-5-2 kesho ni 4-2-3-1 Mara 4-3-3 hakuna uniformity, wapo kizani na Hawajui kabisa wapite njia gani

Kuna kitu kuhusu dirisha la usajili, wanaendelea kujaza wachezaji bila kutambua shida halisi ipo wapi, wakirhusu sana wanaleta mabeki, wasipotengeneza wanaleta Viungo, ile format ya Klopp kujenga timu ni bora zaidi, wamuige yeye

Kuhusu Pep Guardiola nadhani ni ubora wake kimbinu, imara kwenye eneo lake! Pressing nzuri kuanzia mstari wa chini wa Mpinzani, kubana uwanja wakati wanashambuliwa na idadi sahihi ya namba kwa eneo

Ukimtazama Phil Foden unasikitika kuona Jadon Sancho anastruggle kwa OGS, ukimtazama Kiungo Kama KDB alivyo huru unaumia kwanini POGBA Hawaki pale United, City inanunua wachezaji lakini bado inapika sana wachezaji, Kocha yupo imara

United wameruhusu mabao 7 kwenye mechi mbili za EPL, kwa ratiba ilivyo kidogo game mbili zijazo ni rahisi nadhani wafukuze Kocha na waanze maisha mapya!
Screenshot_20211107-070416_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom