Makapuku Forum

Makapuku Forum

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo October 26,2021 amemtembelea Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa na kumjulia hali nyumbani kwake Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Itakumbukwa Mwezi September mwaka huu, Lowassa alimpongeza na kumshukuru Rais Samia kwa kuifanya vyema kazi ya kuijenga Nchi, ambapo alisema ——> "kupitia hotuba yake katika Baraza Kuu Umoja wa Mataifa, Mama Samia amelirejesha tena Taifa letu katika ramani ya dunia"

"Rais Samia amethibitisha pasi na shaka kwamba Tanzania imepata nyota ya jaha kwa kuwa na Kiongozi Mkuu Mwanamke Hodari na Shupavu ambaye leo hii tuna kila sababu ya kujivunia na kumuunga mkono" ——— alisema Edward Ngoyai Lowassa, wakati akimpongeza Rais Samia Mwezi September,2021.
Screenshot_20211026-172223_Instagram.jpg
 
Club ya Simba SC baada ya kutolewa club Bingwa Afrika sasa imepangwa kucheza dhidi ya Red Arrows ya Zambia katika mchezo wa play off kuwania kuingia hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Simba itaanzania nyumbani November 28 2021, marudiano December 5 2021
Screenshot_20211026-172400_Instagram.jpg
Screenshot_20211026-172441_Instagram.jpg
 
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema Mtu aliyefariki kwenye mlipuko wa Basi jana alikuwa ni Gaidi aliyelipua bomu la kujitoa muhanga na ndiye alisababisha mlipuko huo uliomuua yeye mwenyewe na kujeruhi wengine kadhaa, karibu na Mjini Mkuu Kampala Uganda .

Museveni amesema Mtu huyo anaitwa Muzafala lakini pia anajiita Isaac Matovu na alikuwa katika ‘’orodha ya wanaotafutwa’’ pia alikuwa mjumbe wa kikundi cha Kiislamu chenye uhusiano na Allied Democratic Forces (ADF), wanaoendesha harakati zao katika nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Itakumbukwa Jumamosi pia mlipuko mwingine ulitokea katika mgahawa mjini Kampala na kumuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine watatu, Polisi ilisema kuwa kuwa mlipuko wa Jumamosi ulisababishwa na kifaa cha vilipuzi kilichokuwa na misumari pamoja na vipande vya vyuma, kilichokuwa kimefunikwa na mfuko wa plastiki.

Wachunguzi walibaini kuwa kulikuwa na uhusiano wa hali ya juu baina ya mashambulio mawili "Kuna watu binafsi au makundi ya watu wanaoandaa hivi vilipuzi vya kutengenezwa ambao ni washirika wa makundi ya Washambuliaji hao"
Screenshot_20211026-172640_Instagram.jpg
 
“Namuheshimu sana Kaka yangu Karim Benzema na nampongeza amekuwa na msimu bora sana ila hii Ballon dor anastahili Lionel Messi” Sergio Ramos

Una maoni gani juu ya maneno ya Nahodha wa zamani wa Real Madrid?
Screenshot_20211026-173637_Instagram.jpg
 
Shabiki alivamia uwanjani kwenye mchezo kati ya Marseille na PSG wakati Lionel Messi na PSG wakilishambulia lango la Marseille kwa nguvu

Kitendo hicho kilisababisha mchezo kusimamishwa kwa muda

Ni Ngoswe hii, penzi kitovu cha uzembe [emoji3]
Screenshot_20211026-174512_Instagram.jpg
Screenshot_20211026-174530_Instagram.jpg
 
[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

Katika historia ya klabu zote kubwa duniani ukishafika juu all the way is down, ni kawaida kurudi chini na kuanza upya

Barcelona waliwahi kuanguka huko 1988 kwenye kile kisa maarufu cha Hesperia Mutiny, wachezaji na Viongozi walipishana sana ila wakarudi tena kwa nguvu

Ni kawaida kuanguka na kurudi tena Kama ambavyo Rais Perez wa Real Madrid alijiuzulu hata Ramon Calderon alijiuzulu ila Madrid ikarejea tena

Sikilizeni Simba, mpira ndivyo ulivyo hakuna asiepoteza na hakuna asiyejua Maana ya ushindani ila huu ni mpira wa miguu ni kawaida kutokea yanayotokea

Kwa Viongozi kama kuna Mtu anataka kubaki basi abaki na Kama mtu anataka kuondoka basi aondoke, huu sio muda wa kuwa wa Uvugu uvugu bali Kama moto uwe moto na baridi uwe baridi, Simba inahitaji sana mshikamano

Kwa bench la Ufundi, ni vyema mtambue hii ni Simba, ni klabu kubwa yenye malengo makubwa! Hizi kelele ni kawaida inaonesha ukubwa wa timu, endeleeni kufanya Kazi yenu mpaka itakapokuwa vinginevyo, mnafahamu kanuni za ajira ni kuajiriwa na kufukuzwa, mnafahamu basi msikate Tamaa fanyeni Kazi

Kwa Wachezaji, ninyi ni washindi tena wakubwa! Misimu minne mfululizo kwenye ubora kwa klabu na taifa lenu, hakuna anaewachukia, kikubwa ni kuendelea kupambania badge na watu watakumbuka daima majina yenu

Mimi Nipo upande wenu, sidhani Kama mnaenda uwanjani ili mpoteze wakati hii ni ajira yenu, endeleeni kupambana ni morali ile ile GO HARD OR GO HOME, kilichotokea ni mpira wa miguu, enndeleeni kupambana

Kwa Mashabiki wa Simba, huu ni mpira na hii ni timu! Msipende kupelekwa na upepo! Kama umeipenda timu kisa mtu basi jua mtu anaweza kuondoka ila Simba itasalia, timiza wajibu wako wa kikanuni ni kushangilia au kuzomea ila sio kupelekwa na upepo wa mtu

Hizi ni nyakati za kawaida tu kwenye mpira, kwanini muumie sana?! Kwanini mnahangaika kutaka kutakasa kaniki wakati ni rangi yake?? Hii ni Simba ni zaidi ya klabu, RESPECT [emoji110]
Screenshot_20211026-175254_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom