Makapuku Forum

Makapuku Forum

Timu zetu zote zimeshindwa kufanya vizuri kwenye mashindano ya Afrika [Yanga, Azam, Biashara na Simba] hii inamaanisha bado tupo mbali.

Simba ndio timu ambayo tulikuwa tunaona inakwenda kwenye hatua ambazo sio za kwetu lakini kwa hiki ambacho ameanzanacho msimu huu inaonekana wamepiga hatua kadhaa nyuma.

Kuna kutolewa lakini ulikuwa bora uwanjani lakini Simba wametolewa huku kiwango chao kikitia mashaka!

- Amri Kiemba
Screenshot_20211025-172816_Instagram.jpg
 
Goli la pili walilofungwa Simba lilitokana na mpira wa kurushwa, haukuchezwa na mchezaji yoyote wa Simba hadili linafungwa goli!

Mpira wa kurushwa hadi unatua chini haujaguswa na mchezaji wa Simba tena kwenye eneo la ulinzi, mfungaji anafunga kwa mguu sio kwa kichwa.

Nadhani kulikuwa na haja ya Kennedy Juma kuingia mapema kuongeza idadi ya walinzi wa kati ili Simba icheze kutafuta kufuzu sio kutafuta ushindi!

Kwa mpira jinsi ulivyo, baada ya Jwaneng kupata goli la pili kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa Simba kwa sababu Jwaneng wakaongeza kujiamini wakati huo Simba kujiamini kunashuka wakifikiria wakifungwa goli la tatu wametoka.
Screenshot_20211025-172933_Instagram.jpg
 
Mamelodi Sundowns wanafuzu hatua ya makundi CAF Champions league kwa mara ya saba mfululizo baada ya Jana kuwaondosha Meneama ya Kongo

Samba Masandawana [emoji119]
Screenshot_20211025-173208_Instagram.jpg
 
Mshambuliaji Wa kimataifa wa Tanzania @smsuva27 anaekipiga Kwenye klabu ya @wacofficiel Huko Nchini Morocco jana Amekuwa na Siku Nzuri kazini

Baada ya Kuifungia Timu Mabao mawili Kati ya 6 Walio Shinda dhidi ya Timu Kutoka Ghana timu ya Accra Heart of Oak Ligi ya mabingwa

Ikumbukwe Mabingwa hao Wa ligi kuu Nchini Morocco Walipoteza Mchezo wa kwanza huko Ghana kwa kufungwa 1-0

Wydad sasa inaungana na timu zingine ambao zimefuzu hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa kufatia ushindi Huo wa jana na kufanya Matokeo ya jumla Agg: kuwa (6-2)


Screenshot_20211025-173408_Instagram.jpg
 
Kujiamini kulikopiliza kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi. Kadiri muda ulivyokuwa unaenda mchezo ulikuwa unabadilika lakini benchi la ufundi halikuonesha kubadilika kuendana na uhitaji wa mchezo.

Walikuwa wanaamini Jwaneng hata kama wamefunga magoli mawili, wao hawawezi kushindwa kupata goli kwa hiyo hakukuwa na mipango ya kujilinda.

Hata mabadiliko ya wachezaji ambayo yalifanywa na Simba ilikuwa ni kukamilisha taratibu lakini hayakuwa ya kimbinu.

Kwa hiyo kujiamini hakukuwa kwa wachezaji pekeyao bali hadi kwenye benchi lao la ufundi na hawakuwa wanawaza kwamba tayari mechi imebadilika.

Matokeo ya 2-1 yalikuwa yanaifanya Simba isonge mbele hatua inayofuata lakini waliendelea kuamini Jeaneng sio timu ya kuwafunga.

- Amri Kiemba
Screenshot_20211025-173616_Instagram.jpg
 
Leo tumejifunza somo la maana: ‘Kamwe usiwadharau wapinzani wako hadi filimbi ya mwisho itakapopulizwa.’ Hakuna dhamana katika mpira wa miguu. Bado ninaamini tuna timu nzuri. Kuteleza si kuanguka. Tutarudi tukiwa na nguvu zaidi!

-Barbara Gonzalez
Screenshot_20211025-173805_Instagram.jpg
 
[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

MO DEWJI, NI SHIDA JUU YA SHIDA?

Nimezitazama tweet za Mwekezaji wa Simba, MO Dewji kisha nikaona Tweet ya Mzee Magori zote nimeziona kwa uzuri kabisa ila nina shida ya tweet mbili hizi

Tweet ya MO Dewji kwangu haipo sawa, timu imetoka kupoteza ipo katika hali ngumu kisha yeye anakuja kusema kuna watu wawajibishwe, thats not football, kila timu inafahamu kuna matokeo matatu

Nani awajibishwe kama timu bado haina ubavu wa kiuchumi wa kupambana na wakubwa Afrika?? Kama top players ambao ni mhimili wa project wanauzwa nani awajibishwe?

Football ni mchezo wa wazi una namna yake! Kwa mauzo yaliyofanyika na maingizo mapya bado hayajaingia vyema kwenye mfumo niliwahi kusema ni kawaida timu hii kustruggle hapa mwanzoni

Ina maana MO hataki kuheshimu mchakato ambao wao bodi waliuanzisha kwa kuuza?? Nani alilaumiwa wakati Real Madrid walivyomuuza Ronaldo kwenda Juventus? Unamlaumu Kocha au Viongozi? Nani achukuliwe hatua ikiwa wachezaji waliondoka ikiwa yeye ni Mwenyekiti wa bodi?

Wakati TP Mazembe wameingia kwenye falsafa ya PRINCIPLE OF PERCENTAGE RESALE, hawapo vizuri hivi sana hivi sasa kushindana na miamba mingine, umewahi kuona Viongozi wanalalamika?

Simply ni kuwa wanajua wameamua kuuza sana hivyo ni ngumu kutawala Afrika unless project yao ya sasa ikomae! Sasa kama Mazembe wanasubiri ikomae, kwanini MO yeye haamini hilo?

Hizi tweets zinatoa tafsiri halisi ya mpira wetu! Ni sawa na penseli kutuibia kisha unakuja kutusaidia kutafuta! Tatizo halipo kwenye Makocha, tatizo ni huko juu kwenye bodi (Utawala)

Kama mlikubali kuuza basi lazima mkubali timu ijiunde upya taratibu itarejea tena, mnawahi wapi au mlitegemea nini kwa kikosi hiki mapema hii? Kikosi kilindwe na kipewe muda ndio FOOTBALL

Tusihame mada, tubaki kwenye mpira na trusting the process, THATS FOOTBALL
Screenshot_20211025-174357_Instagram.jpg
 
[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

SIMU YA PROFESA KUHUSU SIMBA SPORTS CLUB

Baada ya Simba kuondoshwa kwenye michuano ya Champions League leo, nimetoka kupokea simu ya Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, dakika kadhaa nyuma

Katika mazungumzo akanambia timu Inahitaji utawala bora, benchi bora (technical bench) na Miundombinu (fedha na rasilimali) vyote hivi hutengeneza timu bora

Kwenye issue ya UTAWALA, Profesa alinikumbusha kuhusu ile simu yangu ya siku kadhaa nyuma kuhusu Viongozi wa timu hii kucheza biti tofauti, hakuna wimbo mmoja unaoimbwa

Profesa akaniambia Viongozi kama hawaimbi wimbo mmoja ni nadra kufanikiwa, pale Chelsea walikuwa na utata kati ya Michael Emenalo na waandamizi wenzake, ikiashia yeye kuondoshwa ndani ya Chelsea

Profesa akaendelea kunipa mifano ya FC Barcelona, wajumbe walipishana wengine wakajiuzulu na ile dhambi ya USALITI ikaishia kumuangusha mpaka Rais Bartomeu, mpaka sasa Barca inalipa dhambi ile ya usaliti

Profesa aliongea mengi eneo hili na mengine nimeyaweka nyuma ya pazia! Tukahitimisha kuwa, wanapaswa kuimba wimbo mmoja kwa ajili ya maslahi mapana, they need to sing along

Tukaja kwenye issue ya bench la Ufundi, Profesa akaniambia kwake yeye anaona kuna shida ya muendelezo (CONTINUITY) kwa klabu ya Simba kwenye CAF CL, msimu waliofika Robo kisha uliofata wakatolewa na UD Songo, msimu jana walifika robo na msimu huu wametolewa na Galaxy

Kuna shida ya kiufundi! Profesa akaniambia ya pili ndani ya eneo hilo ni Kocha Gomes Da Rosa, hii Simba tuionayo sasa ndio Gomes halisi anaeanza project yake, Simba wawe tayari kupitia mengi kwakuwa Kocha bado anajitafuta

Kifupi Prof anasema Kocha aliishi kwenye script ya Sven na sasa anaanza kuandika script yake! Wanahitaji muda, haswa na kikosi kipya baadhi ya maeneo

Mwisho Profesa akasema kitu kuhusu Miundombinu haswa FEDHA! Ni wazi project bora inalindwa kwa pesa, ndio pesa hii ilimfanya Chama na Miquisson waondoke, Simba wanaanza upya

Prof anasema, huwezi kutawala Afrika kama huna ubavu wa kiuchumi, ukiishi kwenye misingi ya FEEDER CLUB, utajenga kisha watu wanabomoa! Ndio malipo ya Football development model
Screenshot_20211025-174727_Instagram.jpg
 
Leo October 25, 2021 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson, ameungana na baadhi ya Wananchi pamoja na Viongozi wa Kiserikali katika tukio la kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Mbunge wa Mbeya Mjini Benson Mpesya aliyefariki Dunia Octoba 23, 2021.

Miongoni mwa walioshiriki pia tukio hilo ni Mbunge wa Jimbo hilo aliyemaliza muda wake Joseph Mbilinyi maarufu kama SUGU, Mpyesya ameagwa na kuzikwa nyumbani kwake Kata ya Iganzo Jijini Mbeya.
Screenshot_20211025-175226_Instagram.jpg
Screenshot_20211025-175248_Instagram.jpg
Screenshot_20211025-175422_Instagram.jpg
 
Mtoto wa kitanzania Barka Seif (7) mara baada ya kurejea Tanzania akitokea Ajax ya Uholanzi alikofanya majaribio na kufaulu, wakati wowote kutokea sasa anaweza kurejea Ajax, kwa sasa inaangaliwa njia nzuri ya Barka kujiunga nao pasipo kuvunja sheria za usajili za FIFA kwa watoto chini ya umri wa miaka 18.
Screenshot_20211025-180341_Instagram.jpg
 
Polisi nchini New Zealand wamepongezwa kwa upendo wao baada ya kuamua kufika nyumbani kwa Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne ili kuangalia kama midoli yake ni mizuri kama alivyoiambia Polisi kupitia namba za dharura.

Mtoto huyo alipiga namba za dharura za Polisi na baada ya simu kupokelewa na Askari wa Kike akasema ——— "Askari naweza kukuambia kitu?, midoli yangu mizuri unaweza kuja kuiona!?"

Baada ya Polisi wa Kitengo cha Dharura kutoa taarifa kwa Boss wake kuwa hakuna dharura bali Mtoto anataka midoli yake ikatazamwe na Polisi, Boss akatoa taarifa kwa Askari walio karibu na anuani ya ilipopigwa simu waende ——— "kuna Mtoto wa miaka minne anataka Polisi wakaione midoli yake, OVER"

Constable Kurt alifika anapoishi Mtoto huyo na Wazazi wake na akaiona midoli na kupiga nae picha huku akisema Mtoto huyo anafanya vizuri pia darasani ——— "tunawaomba Watoto wasitumie namba ya dharura 111 kuwapigia Polisi waende kwao kutazama midoli lakini tukio hili la Mtoto huyu limetuvutia"
Screenshot_20211025-180531_Instagram.jpg
 
Mamia ya Watu wameingia mitaani, wakichoma matairi na kupanga matofari barabarani wakipinga hatua ya Jeshi kutaka kufanya mapinduzi nchini Sudan.

Wanajeshi wamemkamata Waziri Mkuu wa Sudan, Abdalla Hamdok baada ya kukataa kuunga mkono mapinduzi kufuatia wiki kadhaa za mvutano baina ya Jeshi na Viongozi wa kiraia juu ya mpango wa kugawana madaraka.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya habari katika ukurasa wa Facebook, Wanachama wa kiraia katika Baraza linalotawala Sudan na mawaziri katika serikali ya mpito ya Waziri Mkuu Abdalla Hamdok, nao pia wamekamatwa.

Huduma za inteneti zimekatwa kote nchini huku barabara kuu na madaraja yanayounganisha mji mkuu wa Khartoum vikifungwa, Wanajeshi walivamia makao makuu ya Televisheni ya taifa ya Sudan iliyoko katika mji wa Omdurman, wakati nyimbo za kizalendo zikirushwa katika televisheni.

Taarifa zaidi zinasema kwamba Waziri mkuu Hamdok na Mawaziri wake wamepelekwa eneo lisilojulikana, mmoja wa Waandamanaji amepinga hatua ya Jeshi akisema kinachofanywa na Jeshi ni usaliti kwa raia wote katika pande zote na kwamba ni wajibu wa raia wote kupinga na kuzuia barabara zote za nje, kuzuia vikosi vyovyote vya Jeshi kusonga.
Screenshot_20211025-180702_Instagram.jpg
 
Kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS limedai kuhusika na shambulizi la bomu lililoua Mtu mmoja kwenye Mji Mkuu wa Uganda, Kampala Jumamosi usiku, haya yameelezwa kupitia ukurasa wa Telegram wenye mafungamano na kundi hilo ambapo IS imesema wamelipua bomu hilo katika Club moja ambayo Majasusi wa Serikali ya Uganda hupendelea kukaa.

Taarifa ya polisi wa Uganda imesema kuwa shambulio hilo liliilenga baa inayouza nyama ya nguruwe katika kitongoji kimoja cha Mji wa Kampala ambapo Wanaume watatu waliingia kama Wateja wakaweka mfuko wa plastiki wenye vilipuzi chini ya meza na kisha wakaondoka kabla ya mlipuko.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema shambulio hilo linaonekana kuwa la kigaidi, mbali na mmoja aliyeuawa, shambulio hilo liliwajeruhi wengine watatu, wawili wakiwa katika hali mahtuti ambapo baada ya IS kukiri kuhusika na mlipuko huo wameiita Serikali ya Uganda kama Adui wa Uislamu.
Screenshot_20211025-180847_Instagram.jpg
 
Viatu vya legend wa mpira wa kikapu nchini Marekani Michael Jordan vya toka mwaka 1984 vimeuzwa kwa bei ya USD milioni 1.472 kwenye mnada Las Vegas na bei hiyo kuvunja rekodi katika mnada na kuwa viatu vya michezo vilivyouzwa kwa bei kubwa zaidi mnadani vikiipiku rekodi iliyowekwa August 2020 ya Nike Air Jordan vilivyouzwa kwa $ laki 6.15.

Jordan alitumia viatu hivyo aina ya Nike Air Ships vyenye rangi nyekundu na nyeupe wakati wa msimu wake wa kwanza akiichezea Chicago Bulls, mwaka ambao yeye na Nike walianza kushirikiana kuingiza sokoni bidhaa zenye nembo yake ikiwemo nguo na viatu.

$ milioni 1.472 kwa pesa za Tanzania ni sawa na Bilioni tatu, milioni mia tatu tisini na tatu laki tano na elfu tisini na mbili na mia tano ishirini na mbili.
Screenshot_20211025-181016_Instagram.jpg
 
Felisiana Raphaeli Mkazi wa kata ya Kibosho Magharibi Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro ametimiza umri wa miaka 124, jana Jumapili alipelekwa kanisani kumshukuru Mungu na baadaye kufanyiwa sherehe ya birthday nyumbani kwake.

Mtoto wa mwisho wa Bibi huyo Steven Raphael amesema Mama yake amebarikiwa Watoto, Wajukuu 22 na Vitukuu 42 ambapo kwa umri alionao sasa hawezi kuongea chochote lakini anaweza kutembea kidogo pale anapopatiwa msaada.

"Bibi amefikisha umri huo kutokana na matunzo, Babu mzaa Bibi alifariki akiwa na miaka 128, uzao wa bibi unaonekana Mungu ameubariki” ——— Steve.

Video nzima ya Bibi huyu na sherehe aliyofanyiwa ipo kwenye Youtube ya millardayo.
Screenshot_20211025-181123_Instagram.jpg
 
Wavuvi tisa wanaofanya shughuli zao katika Ziwa Victoria Mkoani Kagera wameokolewa baada ya kutelekezwa ziwani kwa siku 15.

Wavuvi hao ambao walitelekezwa tangu tarehe 8 October mwaka huu, kati yao nane wamepokelewa jana na Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jeneral Charles Mbuge katika bandari ya Bukoba baada ya kuokolewa wakiwa washaingia upande wa Uganda.

Baada ya mapokezi hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera amekiri kupokea taarifa zao tangu walipotelekezwa na kunyang'anywa baadhi ya vifaa vyao ikiwemo mitumbwi na kuachiwa mtumbwi mmoja huku ukiondolewa baadhi ya vifaa ili usifanye kazi huku Afisa uvuvi mfawidhi wa kikosi cha doria Mkoa wa Kagera Yohana Milunde akituhumiwa kuwafanyia kitendo hicho.

Meja Jeneral Mbuge amesema kuwa tayari Mtu mmoja kati yao alichukuliwa na ndugu zake na kuongeza kuwa Afisa wa Doria anayetuhumiwa tayari yupo mikononi mwa TAKUKURU na kuahidi kuwa wataendelea kufuatilia kwa ukaribu tukio hilo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa atakayekutwa na hatia.
Screenshot_20211025-181300_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom