[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr
SIMU YA PROFESA, SIMBA VS POLICE TANZANIA
Dakika kadhaa kabla ya mchezo nilipata wasaa wa kuzungumza na Professor na dakika chache baada ya mchezo nimezungumza nae
Prof leo alinipa kazi nikasome kazi ya Msomi mmoja anaitwa Robert Brimmer kutoka Chuo kikuu cha Winthrop na Joni Boyd,PhD, CSCS!
Wasomi hawa wa Sayansi ya michezo waliandika kitu kuhusu mambo 9 Makocha hufanya wanaporithi timu ya mpira wa miguu!
Nianze na point ya pili inasema "Focus forward, glance back" ni wazi Kocha Hitimana anafahamu kutakuwa na ukosoaji mkubwa wa Simba hii dhidi ya Simba zilizopita, atautazama msimu uliopita kama sehemu ndogo ya kuujenga msimu huu
Profesa wangu anasema "use something from last season but just a piece of the puzzle not the landscape of the picture" ni wazi kwa mechi ya leo Kocha anatazama kidogo cha msimu uliopita na kujenga picha yake ya msimu huu
Point ya tatu inasema "change what you can control" badili kile ambacho unaweza kukidhibiti, hapa kuna basics na fundamentals! Leo tumemuona Hitimana, hajakibadili sana kikosi, hajaweka sana vitu vipya, anashikilia basics kwanza, ndicho anaweza fanya kwasasa
Mwisho ni "keep concepts simple" mbinu zake lazima ziwe nyepesi ili wachezaji wamuelewe kirahisi sana, hii inasaidia wachezaji wasicheze kwa kufikiria sana na watacheza wakiwa na uhuru, kama leo kwenye transition Simba chini ya mstari ilisalia na mabeki wawili tu!
Profesa alimaliza kwa kuniambia, hii project imeanza upya, tegemea kuona ikipoteza au kushinda kwa mbinde, ndio mpira wa miguu na zama mpya zimeanza, muhimu alama tatu