Makapuku Forum

Makapuku Forum

Ligi ya Mabingwa Afrika inaendelea kesho, unataka kuwashuhudia wawakilishi wa Tanzania pale kwa Mkapa? Kama jibu lako ni ndio kamata tiketi kutoka kituo kilicho karibu yako!

Mnyama anaenda MAKUNDI??
Screenshot_20211023-155706_Instagram.jpg
 
Pichani ni Cristiano Ronaldo na Dada wa Alex Telles baada ya mchezo wa United dhidi ya Atalanta

Ronaldo alitumia dakika 30 kupiga picha na familia za wachezaji wenzake ambao walisubiri nafasi hiyo adhimu

Wake za wachezaji, familia zao na Rafiki zao walipata nafasi hiyo
Screenshot_20211023-155824_Instagram.jpg
 
Ugeni wa mashindano unawasumbua Biashara United, hawana uzoefu wa michuano na safari zinakuaje. Kila kitu kwao ni kipya, likitokea tatizo utatuzi wake unachukua muda mrefu.

- Amri Kiemba.
Screenshot_20211023-160000_Instagram.jpg
 
Kwa mujibu wa Zaka Zakazi, kocha wa Azam FC George Lwandamina amesema timu yake inafanya kama ambavyo anataka na maendeleo yanaongezeka kidogokidogo kadiri siku zinavyozidi kwenda. Anatarajia mchezo mzuri na matokeo yanaweza kupatikana.

Wachezaji wana ari na kila mmoja anautamani mchezo dhidi ya Pyramids FC huku wakiendelea kuhamasishana wao kwa wao
Screenshot_20211023-160537_Instagram.jpg
 
Mabeki wa Chelsea, Trevoh Chalobah na Antonio Ruddier asili yao ni Sierra Leon, nchi ambayo ipo barani Afrika

Rudiger anacheza timu ya taifa ya Ujerumani na Chalobah amechagua England
Screenshot_20211023-160717_Instagram.jpg
 
Thierry Henry amekataa kama Mo Salah ndiye bora zaidi duniani kwa sasa:
.
"Mabao ambayo Salah anafunga, kwa sasa, ni mazuri sana. Lakini unawezaje kumsahau Lewandowski? Unawezaje kumsahau Benzema? Unawezaje kusahau inahitajika kufanya hivyo katika mechi za kimataifa pia?"
.
Mnasemaje, nani Bora kwa sasa: Mo Salah; Benzema au Lewandowski ?? [emoji848]
Screenshot_20211023-160838_Instagram.jpg
 
Nabi afichua siri ya Kiwango Bora cha Feisal Salum Feitoto:
.
“Hamjui kwanini amekuwa bora (Fei Toto) nilipoanza msimu nilikaa naye nikamwambia nataka awe bora msimu huu nitakuwa nampanga namba 10, akiwa hapo awe anarudi kukaba pale kati kazi ambayo anaifanya, pia awe akichezesha timu vizuri,” aesema Nabi na kuongeza;
.
“Majukumu hayo anayafanya vizuri sababu ni kijana mdogo ambaye ana nguvu ya kujituma lakini pia nikamwambia kufanya hayo pekee haitoshi, nataka pia afunge mabao kwa mashuti. Najua ubora wa Feisal anajua sana kupiga mashuti makali, ila nilimwambia nataka mashuti yanayolenga lango akiweza afunge, naona sasa ameanza kufanya kile ninachotaka.”
.
“Najua yapo mashuti yatakosa kulenga lango, ila yale yatakayopanguliwa na makipa, najua kuna Mayele. Huyu ni mshambuliaji anayejua kukaa maeneo sahihi sioni kama atakosa kumalizia nyavuni na kuisaidia timu kupata matokeo mazuri,”
Screenshot_20211023-161004_Instagram.jpg
 
Barcelona yajitosa rasmi kwa Mbappe
.
Licha ya Real Madrid kuonekana ina nafasi kubwa ya kuinasa saini ya staa wa PSG na Ufaransa, Kylian Mbappe, 22, dirisha lijalo la majira ya kiangazi dili hilo lipo hatihati ya kufeli.
.
Hiyo inatokana na mabosi wa Barcelona kujitosa kwenye vita ya kuwania saini ya straika huyo ili kuboresha eneo la ushambuliaji. Mbappe ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu alikuwa akitajwa kuwa na nafasi kubwa kujiunga na Madrid dirisha lililopita lakini PSG ilikataa ofa iliyotolewa.
.
Taarifa zinadai Barca inataka kutumia ushawishi wa Lionel Messi na Neymar ili kuipata huduma ya supastaa huyo.

..................
Screenshot_20211023-161659_Instagram.jpg
 
Nigeria ni moja kati ya nchi yenye vipaji vingi sana barani Afrika

Bahati mbaya sana nyota wao wengi wanaishia kucheza mataifa ya Ulaya, unajaribu kuwaza ingekuwaje kila mtu acheze taifa lake la asili?

Pichani ni David Olatukunbo Alaba , nyota wa Austria mwenye asili ya Nigeria, Baba yake alikuwa ni Mwanajeshi na Mama yake Gina alikuwa ni Nesi

Alaba ni mchanganyiko wa damu ya Nigeria na Ufilipino
Screenshot_20211025-172150_Instagram.jpg
 
Mo ni mwekezaji ndani ya Simba lakini pia ni shabiki. Kuna mahali anashindwa kutambua yeye ni nani ndani ya Simba. Anaposimama kuongea kama shabiki watu wanamhukumu kama mwekezaji sio kama Mwijaku.

Kwa hiyo Mo ana vitu viwili kwa wakati mmoja lakini akiibuka kama shabiki watu wanaendanae kama mwekezaji.

- Alex Luambano
Screenshot_20211025-172613_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom