Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20211023-042314_Instagram.jpg
 
Yanga Wajibiwa Ishu ya Wachezaji 12!
.
Bodi ya Ligi Tanzania imezikumbusha timu za Ligi Kuu Bara kwamba kanuni ya kuwachezesha wachezaji 12 kwenye mechi moja, ililenga michuano ya kimataifa pekee na si vinginevyo.
.
“Timu zenyewe hasa zinazoshiriki mashindano ya kimataifa ndizo zilitushinikiza kuongeza idadi hiyo ili kuweza kufanya vizuri kimataifa kutokana na wachezaji wetu wa ndani wengi hawana uzoefu na ubora wa kutoa ushindani kwenye michezo ya kimataifa ambayo ina ushindani,”
.
“Napongeza mwanzo sio mbaya wageni waliosajiliwa wameweza kutubeba kimataifa na kufanikiwa kupata nafasi nne za kuiwakilisha nchi kimataifa lakini hilo lisiwe sababu ya kutushawishi tuongeze idadi ya wageni kwenye ligi yetu, haiwezekani na haitatokea, wazawa na wao wanahitaji kukuzwa na kujengewa uzoefu.
.
“Hatuwezi kuendelea kusikiliza kila kitu tunachoshauriwa. Kwenye kanuni hii tulipokuwa tunaipitisha tulishirikisha viongozi wa klabu na kukubaliana. Hakuna haja ya kushindwa kupandisha vipaji vya wazawa kwasababu ndio wanaoiwakilisha nchi kwenye timu ya taifa.”
.
“Mimi nashauri gharama za kusajili waanzishe vituo vya vipaji,” amesema Mtendaji Mkuu wa TPLB, Almasi Kasongo.

Screenshot_20211023-042744_Instagram.jpg
 
[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

SIMBA SPORTS CLUB, WATU WALE MATAPISHI YAO?

Kuna kitu kinaitwa Fantasy world, hii ni dunia ya kusadikika ambayo kiuhalisia hii dunia haipo, dunia hii imetenengenezwa tu kichwani ila kivitendo haipo

Umewahi kuiwaza dunia hii?? Dunia hii ambayo hata klabu ya Simba tuliiweka kwenye dunia hii nami nikiwemo niliamini Simba wapo dunia yao ila ilikuwa ya kusadikika

Tuliwahi kuamini kuondoka kwa Haji Manara basi dunia mpya Simba imeanza kujijengea, dunia ya kuondoka kwenye kelele nyingi na kuhamia kwenye makaratasi zaidi Kama wakubwa wengine Afrika na duniani

Nikaandika makala za kupongeza sana na mapambio kutokana na hatua hiyo ila sasa imenilazimu kula matapishi yangu mwenyewe kwa kile kilichotokea Jana

Kuna misamiati miwili kuna Developing clubs and developed clubs! Kuna klabu inayoendelea na klabu iliyoendelea, lakini Profesa wangu wa Chuo kikuu aliniambia Tanzania hakuna klabu iliyoendelea, ni suala la muda na wasaa tu

Profesa alinikumbusha Kitabu cha SIZITAKI MBICHI HIZI, kisha akamaliza tena na kuniambia hakuna klabu iliyoendelea Tanzania Bali zote zipo kwenye process!

Kwa tafsiri fupi baada ya press ya Jana ni kuwa bado Simba inazimiss kelele za Haji Manara, bado Simba inamiss dunia yake halisi na sio dunia ile ya kusadikika tuliyowatengenezea

Kifupi ni Kama kusema mrithi wa Haji hajapatikana hivyo wamechukua vichwa viwili vya kuungana kisha kuleta flavor kama ya Haji, michambo kama kawaida, ngebe Kama kawaida na kutrend Kama kawaida! Ndio tafsiri sahihi ya nyuma ya pazia

Kwakuwa imechaguliwa style ya INFORMAL (mdomo) basi tunaamini yaliyosemwa Jana na yatakayoendelea kusemwa ndio msimamo wa Simba na Viongozi wao! NIMEKUBALI KULA MATAPISHI YANGU

Kitengo cha Mashabiki na Wanachama kinajifia tunaliona hilo?? Nguvu inawekwa idara ya Habari tu?
Screenshot_20211023-043013_Instagram.jpg
 
FEISAL SALUM VS LUIS MIQUISSON

Takwimu zao kwenye AZAM SPORTS FEDERATION CUP (ASFC) 2020/21

FEISAL
Mechi -[emoji2392]
Mabao -[emoji2388]
Assist -[emoji2389]

MIQUISSON

Mechi -[emoji2393]
Mabao -[emoji2390]
Assists -[emoji2390]

Ila tuzo ya MVP imeenda kwa Feisal Salum [emoji102]

Miquisson is robbed [emoji31]
Screenshot_20211023-043218_Instagram.jpg
 
[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

Clatous Chota Chama by miles away NO DOUBT! Again NO DOUBT! On repeat NO DOUBT

Miguu yake iliamua matokeo mengi Muhimu ndani ya Simba, miguu yake imepiga zaidi ya assists 15 na kachangia zaidi ya mabao 25 in total

Sidhani kama kuna kitu kingine tulikihitaji Chama akufanyie tena kutoka eneo la Midfield, anachezesha, Anaassist na anafunga

Ni muendelezo wa historia mbaya ya viungo kwenye ramani ya soka duniani! Aliwahi kukosa Iniesta mpaka Leo hatujui sababu, aliwahi kukosa Xavi hatujui sababu! Kifupi Triple alipaswa kubeba hii back to back

Midfield ya nipe mbaya nikupe nzuri, Ulaya ndani ya Dar Es Salaam! Labda ni muendelezo wa dunia kutohusudu sana Technicians, Mimi nakubali sana soka la Kibrazil

Clatous Chama, one of the best to grace the football soil of this country

He’s robbed

Screenshot_20211023-043331_Instagram.jpg
 
Baada ya Madaktari wa New York Marekani kufanikiwa kwa mara ya kwanza katika historia kufanya upandikizaji wa figo ya nguruwe kwa Binadamu na upandikizaji huo kukamilika bila kuleta madhara kwa Binadamu, imeelezwa kwamba hatua hii itafungua mlango wa chanzo mbadala cha viungo vinavyohitajika sana na itasaidia pia kuepusha Watu kuchangiana figo ambapo kila mmoja kubaki nazo zote mbili.

Upandikizaji huo umefanywa NYU Langone Health, New York City ambapo Watafiti wengi walikuwa wakipambana kwa muda mrefu kuwapandikiza Binadamu figo za Wanyama lakini walikuwa wanakwamishwa na kuwafanya Binadamu hao wasipate madhara baada ya upandikizaji.

Tatizo la Watu kupata shida ya viungo limekuwa kubwa Duniani ambapo kwa Marekani pekee Watu 107,000 wanasubiri kupandikizwa viungo mbalimbali kwa sasa huku kati ya hao Watu 90,000 wakisubiri kupandikizwa figo. View attachment 1983739
Hii technolojia wana I promote sana...

Haya BBC, CNN wanao promote sana...
 
Serikali ya Luxemburg imetangaza rasmi kuruhusu kilimo cha bangi na matumizi ya bangi ambapo hatua hii inaifanya Nchi hii iwe Nchi ya kwanza kwenye Bara la Ulaya kuruhusu kilimo cha bangi pamoja na matumizi yake ambapo chini ya sheria hii mpya, Watu wazima wenye zaidi ya miaka 18 wataruhusiwa kutumia bangi na kuotesha hadi mimea minne kwa kila nyumba.

Hata hivyo bado kutumia bangi hadharani itabaki kuwa haramu ndani ya Taifa hilo, vilevile kwenye upande mwingine mbegu za biashara pia zinaruhusiwa chini ya sheria mpya bila kikomo kwa kiwango au viwango vya Tetrahydrocannabinol (THC), sehemu ya kisaikolojia ya bangi.

Luxemburg ambayo ni miongoni mwa Nchi kumi tajiri duniani inatajwa kuwa miongoni mwa Nchi zinazojali zaidi Watu wake ambapo vingine vilivyoruhusiwa ni usafiri wa Mabasi na Treni kuwa bure kwa Watu wote iwe ni Raia au asiye Raia.
Screenshot_20211023-153835_Instagram.jpg
 
Mkali wa soka Mohamed Salah ambaye mkataba wake wa kuichezea Liverpool umebakiza chini ya miaka miwili kumalizika amesema angependa asiondoke Liverpool maisha yake yote na kusisitiza kwamba maisha yake ya baadaye "yanategemea Club"

Salah ambaye amefunga goli 12 katika mechi 11 msimu huu na kuisaidia Liverpool kushika nafasi ya pili kwenye Premier League aliiambia Sky Sports kwamba "ukinuliza mimi nitakwambia ningependa nikae Liverpool mpaka siku yangu ya mwisho ya kucheza soka lakini siwezi kuzungumza zaidi kuhusu hilo kwasababu halipo mikononi mwangu, itategemea na Club inachokitaka sio mimi"

"Kwa sasa siwezi kujiona nikicheza na Timu nyingine dhidi ya Liverpool, hyo inaweza kunisikitisha, ni ngumu, sitaki kuizungumzia lakini itanisikitisha sana lakini acha tuone nini kitatokea baadaye" ——— Salah.

Umewahi kuwaza tofauti na alivyosema Salah?
Screenshot_20211023-154156_Instagram.jpg
 
Jeshi la Marekani limethibitisha kumuua Kiongozi mwingine mkubwa wa Kikundi cha kigaidi cha Al - Qaeda Abdul Hamid al - Matar kwa kufanya shambulio la Ndege isiyo na Rubani (drone) Kaskazini Magharibi mwa Syria.

Marekani imesema mauaji ya Kiongozi huyo yatadhoofisha uwezo wa Al-Qaeda kufanya mashambulizi Duniani, kuitishia Marekani na Watu wasiokuwa na hatia.
Screenshot_20211023-154336_Instagram.jpg
Screenshot_20211023-154404_Instagram.jpg
 
Msafara wa magari ya Wanajeshi Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania #TANZBATT8 ulilazimika kusimama kwa muda na kujibu mashambulizi ya risasi baada ya kuanza kushambuliwa na Waasi wanaodhaniwa kuwa wa ADF eneo la Kilia, Ruwenzori Jamhuri ya Kimokrasia ya Congo.

Walinda Amani hawa kutoka Tanzania walifanikiwa kuwadhibiti Waasi hao ambao baada ya kuzidiwa nguvu walikimbilia msituni.
Screenshot_20211023-154524_Instagram.jpg
 
Mwanafunzi mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka 17 akisoma kidato cha nne akisoma Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Gathiruini Nchini Kenya amefariki kutokana na majeraha aliyopata kutokana na kipigo alichokipata baada ya kuingia kwa siri na kinyemela kwenye bweni la Wanafunzi wa kike kwenye shule jirani ya Wasichana.

Inadaiwa Mwanafunzi huyo aliingia na wenzake watano ambapo walipoonekana Wanafunzi wa kike walipiga kelele na ndipo Walinzi na Wafanyakazi wa Shule hiyo walipojitokeza na kushambulia marehemu akapata majeraha na kufariki baadae, wenzake watano walifanikiwa kutoroka.
Screenshot_20211023-154832_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom