Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika watashuka dimbani kesho Oktoba 23 na 24 kumalizia mechi za marudiano
Screenshot_20211022-142452_Instagram.jpg
 
Kilichobaki ni Luke Shaw kuendelea kutazama Youtube namna Marcelo alivyokuwa anaweka mitungi kwenye box

Kijana ameanza kuelewa nini Ronaldo anataka
Screenshot_20211022-150238_Instagram.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla ametoa onyo kwa Wafanyabiashara wanaoendelea kufanya biashara pembezoni mwa barabara ya Airport licha ya vibanda vyao kuondolewa kuhama mara moja na kwenda kwenye maeneo yaliyotengwa.

RC Makalla ametoa onyo hilo mapema leo alipotembea mguu kwa mguu kutoka Airport hadi Chang'ombe kuona utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ambapo ameshuhudia baadha ya Wafanyabiashara wakipika vyakula chini ya miti na kuwataka waondoke na kwenda kwenye maeneo yaliyotengwa.

Aidha RC Makalla amesema kuvunja kibanda na kuendelea kupika chini ni kazi bure hivyo amewaelekeza Wakurugenzi, Watendaji wa Kata na Mitaa kuhakikisha wanasimamia Wafanyabiashara hao wasirudi upya.
Screenshot_20211023-034652_Instagram.jpg
 
Director wa movie aitwae Halyna Hutchins (42) amefariki baada ya kupigwa risasi kwa bahati mbaya na Mwigizaji Alec Baldwin wakati wakiwa ‘location’ kurekodi filamu iitwayo Rust New Mexico nchini Marekani.

Polisi wamesema bado wanachunguza tukio hilo na hakuna anayeshikiliwa kwa sasa kwakuwa tukio limetokea wakati Watu wakiwa kazini ambapo Director mwingine aitwae Joel Souza (48) amejeruhiwa na amelazwa Hospitali.

"Hakuna maneno ya kufikisha mshtuko na huzuni yangu juu ya ajali mbaya ambayo ilichukua uhai wa Halyna Hutchins, Mke, Mama na mwenzetu, moyo wangu umevunjika nikiwawaza Mume wake, Mtoto wao na wote ambao walimjua na kumpenda Halyna” alaindika Baldwin kwenye twitter.

Hii sio mara ya kwanza kwa Mtu kufariki akiwa location kwa kupigwa risasi ya moto wakati ambapo huenda silaha ilidhaniwa haina risasi za moto, mwaka 1993 wakati inarekodiwa Filamu ya The Crow Mwigizaji Brandon Lee (Mtoto wa Bruce Lee) aliuawa pia kwa risasi kwa bahati mbaya.
Screenshot_20211023-034804_Instagram.jpg
 
Baada ya Madaktari wa New York Marekani kufanikiwa kwa mara ya kwanza katika historia kufanya upandikizaji wa figo ya nguruwe kwa Binadamu na upandikizaji huo kukamilika bila kuleta madhara kwa Binadamu, imeelezwa kwamba hatua hii itafungua mlango wa chanzo mbadala cha viungo vinavyohitajika sana na itasaidia pia kuepusha Watu kuchangiana figo ambapo kila mmoja kubaki nazo zote mbili.

Upandikizaji huo umefanywa NYU Langone Health, New York City ambapo Watafiti wengi walikuwa wakipambana kwa muda mrefu kuwapandikiza Binadamu figo za Wanyama lakini walikuwa wanakwamishwa na kuwafanya Binadamu hao wasipate madhara baada ya upandikizaji.

Tatizo la Watu kupata shida ya viungo limekuwa kubwa Duniani ambapo kwa Marekani pekee Watu 107,000 wanasubiri kupandikizwa viungo mbalimbali kwa sasa huku kati ya hao Watu 90,000 wakisubiri kupandikizwa figo.
Screenshot_20211023-035024_Instagram.jpg
 
Kitendo cha baadhi ya wateja kushindwa kulipa mikopo kwa wakati, kimetajwa kuwa moja ya changamoto kubwa kwa uendeshaji wa taasisi hizo za fedha nchini.
Pia, hatua hiyo imetajwa kusababisha baadhi ya taasisi hizo kupungua kwa mitaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Equity, Ester Kileo, ameeleza hayo leo Ijumaa Oktoba, 22,2021 katika kongamano la wiki ya huduma za kifedha linaloendelea kwenye hoteli ya Serena, Dar es Salaam.
Screenshot_20211023-035327_Instagram.jpg
 
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania, Sanjay Rughani amesema huduma za kifedha kwa njia ya mtandao kwenye mabenki zimekuwa kwa kasi na kufikia asilimia 60.

Rughani ameyasema hayo leo Ijumaa Oktoba, 22, 2021 kwenye kongamano la wiki ya huduma za kifedha linaloendelea katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo limeandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru.
Screenshot_20211023-035449_Instagram.jpg
 
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) amewafutia mashitaka 10 ya utakatishaji fedha washtakiwa watatu kati ya watano akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu.

Mbali na Maimu washitakiwa wengine waliofutiwa mashitaka hayo ni aliyekuwa Ofisa Usafirishaji Nida, George Ntalima na Xavery Silverius maarufu Silverius Kayombo waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Screenshot_20211023-035558_Instagram.jpg
 
Upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili Mwanasheria wa kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Joseph Makandege umesema bado hawajafikia muafaka wa mazungumzo baina yao na mshtakiwa huyo.

Makandege anayekabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya dola za Marekani 980,000, ameomba kufanya majadiliano na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali (DPP) ili kukiri kosa. Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladislaus Komanya ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na kutoa mrejesho wa majadiliano ya mazungumzo ya awali, ambapo hawajafikia muafaka wa mazungumzo baina yao.

Oktoba 20, 2021 Makandege aliomba tena kufanya mazungumzo na DPP kufanya majadiliano ya kukiri makosa yanayomkabili ili kupata nafasi ya kwenda kushiriki msiba wa baba yake mzazi.

Komanya amedai kuwa baada ya kutafakari DPP ameridhia kufanya mabadiliko katika hati ya mashtaka hivyo, kurekebisha kifungu cha 234(1) cha sheria ya mwenendo wa jinai.
Screenshot_20211023-035655_Instagram.jpg
 
“Vijana wengi waliozaliwa kuanzia miaka ya 1990 ni kizazi kinachofikiria tofauti sana kuanzia kwenye Kazi na maisha ya kawaida, wengi wanachukulia vitu ni rahisi sana” Cristiano Ronaldo

Vijana Mwanenu kawachana, mpunguze kuchukulia vitu poa

Navyowajua mtasema “Ronaldo mwenyewe sharobaro tu”
Screenshot_20211023-035827_Instagram.jpg
 
Mpaka Leo najiuliza Serge Gnabry alifeli vipi pale Emirates na ameenda kuwa mchezaji bora Bayern Munich

Nawaza tu Munich walifahamu vipi ubora wa Gnabry mpaka kujiamini na kumpa nafasi

Unaposema watu wa mpira ndio wapo Bayern Munich [emoji119]
Screenshot_20211023-035929_Instagram.jpg
 
Simba hapa wamechemka, walishatoka huko na kufika mbali zaidi, hawakutakiwa kurudi tena nyuma.

Sikupendezwa na wahamasishaji kuzungumza mambo ya mtu binafsi! Kama wameamua kwenda uelekeo huo basi watu wazungumze mambo yanayohusu mpira, sio kumzungumzia mtu tena kwa mambo yake binafsi. HAIPENDEZI

Shaffih Dauda
Screenshot_20211023-040643_Instagram.jpg
 
Kipengele kilichonishangaza ni MVP pale walipo Chama, Bocco na Mukoko, tuzo hutolewa kwa yule aliefanya makubwa zaidi, Chama amehusika kwenye mabao 23 ya Ligi kuu

Chama ana assists 15 za ligi na mabao 8, jumla ni 23 hapo! Chama ana mabao matano na assists tatu kwenye CAF ikiwa sawa na amehusika na mabao nane, jumla Chama mmoja kwa michuano miwili tu amehusika kwenye mabao 31

Kuna mchezaji kafikisha idadi hiyo??? Tulitaka Chama afanye nini kutoka eneo la Midfield?? Hata Kama angechukua MVP back to back, ni haki yake alistahili

Kwenye namba Chama amewaacha mbali sana! Pengine yatabaki kuwa maoni yangu binafsi ila ifike wakati tujue Kura zinapigwa vipi, Kama ambavyo wenzetu duniani huweka Wazi kura zao kuliko kamati ambayo itawasilisha mawazo yao binafsi

Maoni ya farhan Jr
Screenshot_20211023-040922_Instagram.jpg
 
TFF: BIASHARA IMESHINDWA KUONDOKA
.
“Licha ya kupatikana kwa Ndege ya kukodi ya ATCL, Biashara United Mara imeshindwa kuondoka kutokana na kukosekana vibali vya anga vya Kimataifa nchini Sudan, Sudan Kusini na kile cha kutua Benghazi utakapochezwa mchezo huo.
.
“TFF imeliandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuomba mchezo huo kusogezwa mbele mpaka Jumanne Oktoba 27, 2021 kupata vibali.

- Cliford Ndimbo, Ofisa Habari na Mawasiliano TFF.
Screenshot_20211023-041424_Instagram.jpg
 
VITA WAAGA MASHINDANO CAF
.
FT | AS Vita Club 1-1 Gallants FC
[Jacques Mangoba Iyadi || Sibusiso Nkosi] [emoji460]️
.
(Agg. 2-3)
.
[emoji830]︎ AS Vita wametupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika
Screenshot_20211023-041715_Instagram.jpg
 
MTIBWA HALI NI MBAYA
.
FT: KAGERA SUGAR 1-0 MTIBWA SUGAR
[emoji460]️ Dickson Mhilu 40’
.
Mtibwa hadi sasa hawajapata ushindi katika mchezo wowote (D2, L2).
Screenshot_20211023-041825_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom