Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20211006-165651_Instagram.jpg
 
Shirikisho la Soka Tanzania TFF na Benki ya Taifa ya Biashara NBC wameingia makubaliano ya udhamini wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara. NBC itadhamini ligi hiyo kama mdhamini mkuu kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia msimu huu.

Kwa msimu huu 2021/2022, kiasi cha shilingi bilioni 2.5 [kabla ya makato ya VAT] kitatolewa na benki hiyo kama mdhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Ligi hiyo itakuwa ikiitwa Ligi Kuu ya NBC.
Screenshot_20211006-165904_Instagram.jpg
 
Mkataba ni wa miaka mitatu, mwaka wa kwanza [msimu huu 2021/2022] tunaanza na Tsh. 2.5B [kabla ya makato ya VAT] lakini kutakuwa na ongezeko kwa miaka inayokuja kwa sababu kutakuwa na mazungumzo yanaendelea.

- Wallace Karia, Rais wa TFF
Screenshot_20211006-170005_Instagram.jpg
 
KIBU DENIS KWENYE RAMANI YA ALPHONSE DAVIES.

Anaandika Gharib Mzinga

Maisha ni safari, Hakuna anayejua kesho yake, Mungu pekee ndiye hukadiria kila sekunde ya Binadamu. Humpandisha na kumshusha atakaye.

Safari ya Nyota mpya wa Simba, Kibu Denis ni moja ya shuhuda na miujiza ya Mungu ikiendelea mbele yetu.

Nyota ambaye ameshapata uraia wa Tanzania, lakini nyuma yake kuna ramani mbaya ya kukimbia maisha magumu na kuitafuta amani.

Kutoka katika kambi ya Wakimbizi iliyopo Tanzania, Kibu anapita anapopajua yeye mpaka kuonesha alichonacho. Alichopewa na Mungu.

Geita, mpaka Mbeya City, Akiwa City anaitwa timu ya taifa ilikua msimu mmoja tu wa maajabu kwake. Msimu ambao kila mmoja aliona uwezo wake.

Alisukuma sana biashara ya magazeti kwa kuandikwa FrontPage akihusishwa na klabu kubwa Nchini mpaka klabu yenye mafanikio zaidi wakati huu ilipomnasa.

Haya aliyapitia Alphonse Davies anatajwa kama mlinzi bora zaidi wa kushoto kwa sasa Ulaya akiwa na Bayern Munich alizaliwa katika kambi ya wakimbizi huko Buduburam Ghana.

Wazazi wake walikimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Liberia, familia hii ilienda Canada kwa msaada wa UNHCR shirika la kimataifa la Wakimbizi.

Wakati huo Alphonse akiwa na miaka 5, Ughaibuni haiongopi, Kipaji chake kilionekana akiwa shule baadae akacheza Vancouver White Capes na sasa Bayern Munich.

"......Africa Oooh Africa"
Screenshot_20211006-170143_Instagram.jpg
 
Baada ya klabu ya Simba ku-post picha za wachezaji wakiwa mazoeni huku miongoni mwao akiwepo Jonas Mkude ambaye baada ya kuitwa timu ya taifa alijiondoa kutokana na matatizo ya kifamilia.

Yahya Njenge kupitia #SportsXtra amesema sio kitu cha kushangaza kumuona Mkude akiwa kwenye majukumu ya timu yake. Amesema inawezekana matatizo aliyonayo yanamfanya asiwe huru kuitumikia Taifa Stars lakini ni tofauti inapokuja suala la klabu.

“Ukubwa wa tatizo anaujua mtu mwenyewe mwenye tatizo, Mkude ndio anajua ugumu wa changamoto aliyonayo. Anaweza kufanya mazoezi lakini huenda hawezi kufuata taratibu za kambi ya timu ya taifa na pengine kucheza mechi za timu ya taifa.”

“Mimi sioni kama kuna ubaya, yeye ameona kwa changamoto inayomkabili hawezi kuwa na utumishi uliotukuka kwa majukumu ya timu ya taifa, kaamua kujiweka pembeni.”

“Jambo zuri ni kwamba kajiweka pembeni mapema ili kutoa nafasi kwa mwalimu kutoa nafasi kw watu wengine.”
Screenshot_20211006-170440_Instagram.jpg
 
Kocha mpya wa Mtibwa Sugar Joseph Omog ameamua kutowaruhusu wachezaji wake kwenda kwenye mapumziko kipindi hiki ambacho ligi imesimama kupisha mechi za kimataifa za kalenda ya FIFA.

Wachezaji wa Mtibwa wameendelea kufanya mazoezi kwa saa nane kwa siku [saa nne asubuhi na saa kumi jioni].

Mtibwa Sugar ilipoteza mchezo wa ke wa kwanza kwenye ligi [Mtibwa Sugar 0-1 Mbeya Kwanza] halafu ikatoka suluhu kwenye mchezo wa pili [Mtibwa Sugar 0-0 Tanzania Prisons].
Screenshot_20211006-170936_Instagram.jpg
 
CAF YAIKUBALIA TFF
.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeruhusu mchezo baina ya Taifa Stars na Benin kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuingia mashabiki wasiozidi 10,000
.
Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema kuwa:

“Tumepata taarifa hii kwa kuchelewa lakini sio sababu ya mashabiki kushindwa kuja kuisapoti timu yao. Watu 10,000 ni wengi lakini kulingana na ukubwa wa Uwanja wa Mkapa ni wachache hivyo tunawaomba wajitokeze kwa wingi
Screenshot_20211006-171118_Instagram.jpg
 
REKODI KUIBEBA STARS KESHO
.
Stars na Benin zimekutana mara mbili katika historia, huku mechi zote zikiwa za kirafiki, Stars ilishinda mchezo wa kwanza uliofanyika 2014, mabao 4-1, kwenye Uwanja wa Mkapa.
.
Na mwaka 2017 nchini Benini zikatoa sare ya kufungana bao 1-1, kwenye dimba la Tade de l’Amitie nchini Benin.
.
Ikumbukwe Stars inaongoza kundi ‘J’ ikiwa na pointi nne baada ya kucheza michezo miwili, ikiwa sawa na Benin ambapo Stars inabebwa na wingi wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Screenshot_20211006-171607_Instagram.jpg
 
KISA MABAO, YANGA KUTIA KAMBI ARUSHA KUJIFUA
.
Kaimu Mtendaji mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha amesema mwenendo wa timu yao hadi sasa ni mzuri lakini bado wana kazi kubwa ya kuhakikisha upatikanaji wa mabao unakuwa mkubwa.
.
“Kitu kikubwa kwa sasa tunashinda na kupata pointi tatu lakini tunahitaji kuongeza idadi ya mabao, kocha pia hilo alilizungumza na litafanyiwa kazi bila shaka kwa kipindi hichi ligi imesimama.
.
“Timu inaenda Arusha tunaendelea na kambi kama kawaida, huko kocha atafanya marekebisho ya makosa madogo madogo kama hayo hasa safu ya umaliziaji na morali ya wachezaji ipo juu na hili ndio jambo zuri likituaminisha tutafanya vizuri,” alisema Senzo.
Screenshot_20211006-171742_Instagram.jpg
 
Donny kutua Everton
.
Everton inafikiria kumsainisha mkataba wa mkopo wa miezi sita kiungo wa Manchester United na Uholanzi, Donny van de Beek, 24, katika dirisha lijalo la majira ya baridi baada ya kushindwa kufanya hivyo katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi.
.
Van de Beek amekuwa hapati nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza cha Man United hali inayosababisha hata yeye atamani kuondoka na Everton inataka kutumia nafasi hiyo kumvuta kwao.
Screenshot_20211006-171840_Instagram.jpg
 
Wachezaji wa Timu ya Taifa wakiwa kwenye mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia hatua ya makundi dhidi ya Benin utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kesho Alhamis Oktoba 7, 2021 saa 10 jioni.
Screenshot_20211006-173710_Instagram.jpg
Screenshot_20211006-173731_Instagram.jpg
Screenshot_20211006-173810_Instagram.jpg
 
[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

USTADH KHALID AUCHO, NITAFUNGUA BIBLIA NITAWAITA WATANZANIA

Salaam zangu kutoka njiani Ubena Zomozi, salamu za Waluguru wa Morogoro kwenye mizimu ya Kolelo! Salaam za wapogoro kutoka maporomoko ya Sanje hapo Mang'ula, salaam kutoka Morogoro

Salaam kwako Ustadh Khalid Aucho kutoka ardhi ya Kaguta Yoweri wa Museven, nina mengi ya kuongea kwenye mechi zako kadhaa kwenye ardhi hii ya Muasisi kutoka ardhi ya Wazanaki, Nyerereland

Basi Ustadh kwanza hongera kwa kiwango bora! Kwanza ningependa nianze na maneno ya biblia kama ambavyo Askofu Ndorobo alinifundisha kule seminarini, Mahenge Morogoro

Chukua Agano jipya! Fungua WAFILIPI 4:13! Inasema "Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu" basi basi Ustadh, najua wewe ni Professional nami naomba nikukumbushe vitu kutoka kilele cha Milima ya Udzungwa, Morogoro

Nasikia ni kiongozi bora huko kambini, ni mchezaji bora unaesikilizwa na vijana! Hivyo ndivyo inapaswa kuwa kwa Mchezaji kutoka nje, endelea kuwa kioo kwa Vijana wadogo wenye ndoto kubwa

Namsihi Kijana Shomari akae chini kukusikiliza kama Lwanga alivyoketi pale Uganda kuchota busara zako, namsihi Dickson Job aketi na kukusikiliza kama ambavyo Mustapha Kiza pale Uganda anavyoketi kuchota busara zako

Niendelee kukumbusha kuhusu Dar Es Salaam, Instagram na Facebook, kuhusu Magomeni, Sinza na Kinondoni! Siwezi kusema kila kitu ila nakusihi! Amani ya Mungu ipitayo akili zote ihifadhi moyo wako na nia yako njema

Niendelee kukwambia kuhusu nidhamu bora uliyonayo idumu kwa maslahi ya Yanga Afrika na mpira wetu nchini, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyoheshima, yalosafi, yalohaki na kupendeza, basi endelea kuyatafakari hayo

Naendelea kukutakia kheri Ustadh na nikuache na busara moja "Si kwamba nasema haya kwakuwa nina mahitaji, maana nimejifunza kwa radhi na hali yoyote niliyo nayo"
 
[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

KWANINI SIMBA WANAANZA MSIMU KWA KUCHECHEMEA? (MWISHO)

Nilisema kitu kuhusu WATER THERAPY na elimu aliyonipa Daktari yule! Lakini nilihitaji muda wa kwenda ndani zaidi kusoma kitu kuhusu CONTRAST WATER THERAPY (CWT) au COLD WATER IMMERSION

Timu nyingi zenye scale kubwa ya mashindano hutumia hii ikiwemo Simba, wakihitaji kujenga fitness ya Mchezaji kwa haraka lakini wakijua wazi kuna risk pia ya hiyo fitness ya Wachezaji, nitaeleza vyema

Kwanini licha ya yote Simba wanaipenda njia hii ijapo inawafanya waanze msimu kwa gia ya chini? Yes kwanza uliwahi kufanywa utafiti wa kitabibu duniani kupitia jarida la Sports Physiology and Performance, wakaja na vitu kadhaa muhimu

Walichukua Wachezaji 24 baada ya mechi na mazoezi kwa ajili ya recovery kwa njia hii ya WATER THERAPY, wakapata majibu baada ya masaa 48 kuwa recovery ipo vizuri mno, kwenye physical na pyschometric, ijapo ipo slow kidogo

Hii kwa timu za Ulaya inakuwa rahisi sana lakini huku kwetu ina ugumu kidogo, hapo ndipo nikamuuliza Daktari kwanini iwe tabu huku kwetu na kwanini Simba waitumie kama inawapa tabu?

Daktari akaanza kuniambia kuhusu afya za Wachezaji wetu, wengi wanacheza viwanja vibaya tangu utotoni, wana enka na majeraha mengi sana tangu utotoni na hawatibiwi vyema, kwahiyo kutumia barafu kunafanya watoneshe vidonda

Na ndio maana wengi wanaanza gia ya chini, wanaumia sana ila hii ndio hupelekea vyumba vyao vya kitabibu kutafuta suluhisho la mapema na ndio suluhisho hilo hupelekea afya bora kwa muda mrefu wa msimu

Akasema Simba wanaifanya kwakuwa inawalipa ni njia nzuri ya kubalance vyema uchovu na utulivu wa kiakili, haiwasumbui sana kupata kwao Wachezaji majeraha mwanzoni wakijua kuna muda utafika watatulia na kuwa katika form wote

Daktari akaniuliza, kwa misimu mitatu mfululizo umesikia sana ishu za majeraha mengi kwa Simba kati mwa msimu? Umewahi kuwaona Wachezaji wao wakichoka mwishoni wakati wengine wamechoka sana? Mwisho akasema na ndio sababu wanamaliza msimu kwenye top gear

Tukamalizana kuwa ni sababu za Kitabibu, alinimegea elimu yake
 
Muasisi na Mmiliki wa kampuni ya Facebook Mark Zuckerberg, amepinga vikali madai kwamba mtandao huo wa kijamii unachochea migawanyiko na kuleta madhara kwa Watoto kwa makusudi ili kujinufaisha kibiashara.

Akijibu tuhuma nzito zilizotolewa na Mfanyakazi wake wa zamani, Zuckerberg aliandika kwenye ukurasa wake wa Faceebok kwamba kuhoji kuwa kampuni inashadadia kwa makusudi maudhui ambayo yanawakasirisha Watu kwa maslahi tu ya kutengeneza faida hakuna mantiki.

Kauli ya Zuckerberg imekuja baada ya Mvujisha siri Frances Haugen kuliambia baraza la Congress nchini Marekani kwamba mtandao huo unachochea migawanyiko, una madhara kwa Watoto na ni lazima uwekwe haraka sana chini ya uangalizi
Screenshot_20211006-182413_Instagram.jpg
 
Ongezeko la idadi ya Watu pamoja na joto duniani ni sababu zinazotajwa kuongeza joto mijini, matatizo ya kiafya na kufanya iwe vigumu kuhamia maeneo ya mijini hasa katika mataifa maskini, utafiti mpya umeeleza.

Ripoti hiyo iliyochapishwa na jarida la Chuo cha Taifa cha Kisayansi Marekani inasema kuwa karibu robo ya idadi ya Watu duniani wanaathirika na ongezeko la joto na kwamba kwenye miaka ya karibuni, mamilioni ya Watu wamehama kutoka maeneo ya vijijini na kuhamia mijini ambako joto kwa ujumla ni kali.

Utajiuliza chanzo kingine kilichotajwa kuongeza joto mijini ni nini ? utafiti huo umesema ni barabara nyingi za lami ambayo inachangia joto kwa sababu inafyonza joto vilevile ukosefu wa mimea kama miti mijini ni chanzo cha joto.

Wanasayansi walioandika ripoti hiyo walifanya uchunguzi wa viwango vya joto na unyevu wa kila siku katika miji zaidi ya 13,000 kutoka mwaka 1983 hadi 2016.
Screenshot_20211006-182721_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom