[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr
FC Barcelona kwa miaka mingi wamekua wakihusudu Makocha waliocheza kwenye klabu yao na kuuishi utamaduni wao
Pep Guardiola alifundisha na alikuwa legend wa Barca, akaja Tito Villanova na baadae wakina Luis Enrique na hata huyu Ronald Koeman wote walikuwa Malegend kuna kitu wanakipenda
Wana lugha yao ngumu kidogo kuhusu Makocha ambao hawajui utamaduni wa Barca wala kucheza wanawaita MERCENARIES
Msemo wa ONE THING ABOUT FOOTBALL IS NOT ABOUT FOOTBALL unatumika hapa! Kitu kimoja kuhusu mpira wala hakihusu mpira, ndipo hapo unahitaji kitu cha ziada
Hii video fupi ilinasa kidogo tukio moja wakati bench la Simba lote limechanganyikiwa basi kulikuwa na kichwa kimoja kimepoa, kichwa cha KOCHA SULEIMAN MATOLA
Pengine labda kwakuwa alikuwa anacheza nafasi ya KIUNGO MKABAJI Maana kuna bromance Kati ya Viungo na kuwa Makocha bora
Matola baada ya Kennedy Juma kupata hitilafu alisimama kwa haraka, kwanza alivyomtazama Kennedy alijua haendelei tena (uzoefu) akamwambia INONGA apashe kisha akawahi kwa touchline kuituliza timu
Wakati machela inaingia yeye Matola anazidi kupoint INONGA aingie kwakuwa anajua mechi imechangamka na hakuna muda, hii ndio akili iliyokuwa inafanya vingi kwa pamoja
Kisha akarudi kwa INONGA kumpa maelekezo na wakati Gomes analalamika kutokana na ile rafu, yeye akamuita na kumwambia aongee na Mchezaji anaingia
Moves nyingi za Matola kwenye bench zinaonesha ukomavu wake na uzoefu wake na pengine anafahamu vyema nini Maana ya badge ya Simba! Alikuwa na matukio mengi ila Nilifanikiwa kurecord hili, Mara zote hapanic ila anatoa SOLUTION