Timu imecheza vizuri ila Benin walikuwa bora kwa Mchezaji mmoja mmoja ikaamua matokeo.
Tanzania tumejitahidi wachezaji wametengeneza nafasi ila Benin wameoneka kama wamekuja kwa lengo moja kutafuta alama moja, Kadri muda ilivyokuwa unaendelea plan yao ndani ya Uwanjani ikabadilika, class ya kwao na class yetu ni tofauti
Wakatumia ubora wao, tamaza yule Mchezaji aliyetufunga alipata nafasi moja tena akiwa mbali na nafasi hiyo ilikuwa ni Moja ya nafasi ngumu kwake hiyo hiyo ikaamua mchezo,
Kwaiyo Mimi naamini class, mbinu na hamasa za timu zinaamuliwa na ubora za wachezaji
Mwisho wa siku Benin wametumia ubora wao wa Mchezaji mmoja mmoja sasa hatupaswi kuanza kumlaumu Mwalimu na kuilaumu timu tutakuwa tunakosea
Timu imecheza vizuri lakini Class imeamua, nafasi waliyoipata Benin ni Moja ambayo iliamua mchezo, sisi tulipata nafasi ambazo tulishindwa kuzitumia ndo kama hivyo.
Mwandishi wa Habari za Michezo Charles Abel akielezea mchezo wa kufuzu kombe la Dunia Qatar, Tanzania dhidi ya Benin.