Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu ya kesi inayomkabili Rais wa zamani wa Club ya Simba Evans Aveva na wenzake Oktoba 6 mwaka huu ambapo itakua ni siku moja baada ya Mawakili wa pande zote mbili katika kesi hiyo kuwasilisha hoja zao za mwisho kama Washitakiwa wana hatia au la.

Mbali na Aveva Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Godfrey Nyange (Kaburu) ambaye alikuwa Makamu pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya usajili Zachariah Hans Pope ambaye kwa sasa ni Marehemu.

Awali, Mahakama hiyo iliwaona Washitakiwa hao wanakesi ya kujibu katika mashitaka nane kati ya tisa yaliyokuwa yakiwakabili ambapo ni pamoja na kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi na kutoa maelezo ya uongo.

Katika shitaka la kughushi linalowakabili Washitakiwa wote inadaiwa walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28, 2016 wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zina thamani ya dola 40,577 sawa na zaidi ya Sh milioni 90 huku wakijua sio kweli.

Pia katika mashitaka mengine inadaiwa Aveva, Nyange na Hans Poppe kati ya Machi 10 na Septemba 30 mwaka 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,577.
Screenshot_20211001-190749_Instagram.jpg
 
Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy (2007-2012) amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na Mahakama ya Paris baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya ufadhili wa kampeni yake ya Urais ya mwaka 2012.

Sarkozy anatuhumiwa kutumia karibu mara mbili ya kiwango cha fedha kinachoruhusiwa kisheria ikiwa ni kiasi cha Euro milioni 22 na nusu katika kampeni yake ya kugombea muhula wa pili wa Urais katika uchaguzi alioshindwa na Francois Hollande.

Hukumu hii imetolewa wakati ambapo Sarkozy mwenye umri wa miaka 66 alikata rufaa baada ya kukutwa na hatia nyingine March 2021 katika kesi ya ufisadi ambapo alidaiwa kumuhonga Jaji ili apate taarifa za siri kuhusu kesi ya uchunguzi dhidi yake ambapo alihukumiwa miaka mitatu jela katika kesi hiyo lakini miwili ilifutwa akabakiwa na mmoja ambao bado hajaanza kuutumikia gerezani.

Hata hivyo Sarkozy huenda akaepuka kwenda jela kwa hukumu hii mpya kwani Jaji aliyetoa hukumu hiyo amesema Sarkozy anaweza kutumikia kifungo cha nyumbani japo atavishwa kifaa maalum cha kieletroniki cha kumfuatilia.
Screenshot_20211001-190849_Instagram.jpg
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ikionesha jinsi aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake wakiondolewa Mahakamani baada ya hukumu yao iliyokua itolewe leo kuahirishwa hadi October 15 2021 ikihusu kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayowakabali.
Screenshot_20211001-191020_Instagram.jpg
 
Habari ya Mwanajeshi wa Marekani Abdul Gene Malik kupambana na mamba aliyevamia nyumbani kwao kwa kutumia plastiki ya kuhifadhi takataka ni miongoni mwa habari kubwa za wiki hii.

Mwanajeshi huyu amesema aliamua kujitoa muhanga na kupambana ili kuiokoa Familia yake ambapo tukio hili la ujasiri lilirekodiwa na Majirani zake na wanasikika wakimshangilia baada ya kufanikisha kumfunikia ndani ya chombo hicho cha taka.
Screenshot_20211001-191152_Instagram.jpg
 
Mashabiki wa James Bond nchini Uingereza jana (Alhamisi) walifurika katika majumba ya sinema wakati filamu mpya ya 007 ilipoanza kuonyeshwa, ikiwa ni miezi 18 zaidi ya muda uliopangwa awali.

Majumba ya sinema yamekuwa yakiuza tiketi kwa wiki kadhaa kwa ajili ya filamu hiyo mpya ya "No Time To Die", ambayo ni ya upelelezi wa hali juu na iliyozinduliwa Jumanne jijini London, huku walioiona wakiizungumziwa vizuri.

Inatarajiwa kuwa na mauzo makubwa kuliko yote katika wiki ya kwanza tangu mwaka 2019, wakati kampuni ya kumbi za sinema za Vue ilipouza zaidi ya tiketi 270,000 na Odeon zaidi ya tiketi 175,000 za malipo ya awali.

Filamu hiyo, ambayo awali ilitakiwa itolewe mapema mwaka jana lakini ikaahirishwa kutokana na mlipuko wa janga la Covid-19, ni ya tano na ya mwisho kwa Daniel Craig, ambaye ameigiza nafasi hiyo ya James Bond kama mpelelezi.

"Ni nzuri zaidi ya uzuri. Ni safi," gazeti la The Times limemkariri mchambuzi wa filamu, Kevin Maher, ambaye ameipa hadhi ya nyota tano.
Screenshot_20211001-191334_Instagram.jpg
 
Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), umesema ujenzi wa barabara njia nane kutoka Kimara jijini Dar es Salaam hadi Kibaha mkoani Pwani, unaendelea vizuri na utakamilika kama ulivyopangwa.

Pia, umesema kuwa mpaka sasa mradi huo ambao utakwenda kupunguza tatizo la msongamano wa magari, umekamilika kwa asilimia 94, huku kazi iliyobaki ikiwa ni kujengea matofali pembezoni mwa barabara.

Mkurugenzi mtendaji wa Tanroads, Rogatus Mativila, amelieleza Mwananchi kuwa kwa sasa wameomba nyongeza ya fedha kutokana na ongezeko la kazi ambazo hazikuwapo kwenye bajeti ya awali.

“Kwa sababu kuna kazi nyingi zilijitokeza wakati ujenzi ukiendelea, hivyo kuna ongezeko la kazi na moja wapo ni kujengea matofali pembeni upande wa kulia na kushoto,”alisema.

Kuhusu mapipa yaliyowekwa kwenye barabara hiyo, amesema hatua hiyo inalenga kupunguza ajali hasa katika njia za katikati ambazo zimetengwa kwa ajili ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT).

“Hayo (mapipa) ya katikati hayajatolewa kwa sababu ukiyatoa ndiyo utasababisha ajali zaidi, kwani barabara itakuwa ni pana, itakuwa free (huru). Kwa kuwa zitakuwa ni barabara nane zote, hakuna namna ya kusema mtu anaweza kupata sehemu ya relief (unafuu) ya kusimama.

“Hata kwa magari yenyewe unajua kuna ku-overtake na nini. Hapo katikati ni kwa ajili ya BRT, lakini tunataka tutenganishe kwa kujenga hizo ‘cab stone’.

“Sasa ili kukamilisha hizo ‘cab stone’ tumeomba fedha wizarani kwa sababu bajeti yake haikuwepo kwenye kazi ya awali. Vipo vitu kadhaa ambavyo tumeviombea ambavyo havikuwamo awali. Kwa mfano, hata pale Mbezi, kuna tatizo la foleni pale ukiwa unakwenda Mbezi Beach kwa hiyo kazi hizo zitakamilika,” amesema Mativila.

Alhamisi Septemba 30, 2021, ndani ya gazeti la Mwananchi, tovuti na mitandao ya gazeti hilo, iliripotiwa kimakosa kuwa Mativila alisema kuwa ujenzi huo ulikwama kutokana na ukosefu wa fedha.
Screenshot_20211001-191511_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom