Makapuku Forum

Makapuku Forum

1632994162860.png
 
Kiongozi wa kijeshi nchini Guinea Kanali Mamady Doumbouya ambaye aliongoza Mapinduzi ya Kijeshi yaliyomuondoa madarakani aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo, Alpha Conde, ameapishwa kuwa Rais wa mpito baada ya kuondolewa kwa Conde.

Mamady ambaye ana umri wa miaka 41 anakuwa kiongozi wa pili mdogo Barani Afrika, mwingine ni Rais wa Mali,Assimi Goïta mwenye umri wa miaka 38, ambaye pia aliongoza mapinduzi ya kumuondoa Rais Keita.
Screenshot_20211001-183808_Instagram.jpg
 
Wengi wetu tunafahamu kwamba miongoni mwa waliotangaza nia za kugombea Urais Nchini Ufilipino wakati huu ni pamoja na Bingwa wa mchezo wa ngumi duniani Manny Pacquiao ambae leo amewasilisha fomu za kuthibitsha kuwania urais wa Ufilipino na kuwa mwanasiasa wa kwanza kutangaza rasmi kwamba atagombea nafasi hiyo ya juu kabisa kwenye uchaguzi utakaofanyika mwakani.

Wengi wanatamani kufahamu ni vitu gani au ni vipaumbele gani alivyonavyo Pacquiao iwapo atashinda kiti cha Urais........ anasema vita yake ya kwanza itakua ni kuushinda wa Wananchi, kupigana na ufisadi na kushughulikia janga la COVID 19, kuimarisha huduma za intaneti na kushusha gharama za umeme Nchini humo.

Ingawa Pacquiao ni Mwanachama wa Chama tawala cha PDP-Laban kinachoongozwa na Rais Rodrigo Duterte, Pacquiao atagombea kupitia Chama chake cha People's Champ Movement kufuatia mvutano baina yake na Duterte ambaye muungano wake umeweka nia ya kumsimamisha Mgombea mwingine.
Screenshot_20211001-185748_Instagram.jpg
 
Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Gerson Msigwa amekanusha taarifa iliyoandikwa mtandaoni leo kwamba ujenzi wa barabara ya njia nane ya Dar es salaam - Kibaha ya kilometa 19.2 umekwama.

“Ukweli ni kwamba mradi huu unakwenda vizuri na umefikia asilimia 94, malipo ya Mkandarasi yanafanyika vizuri na ameshalipwa kwa zaidi ya asilimia 90 (takribani Bilioni 161), kwa sasa kinachofanyika ni kukamilisha asilimia chache zilizobaki na kuongeza mahitaji mengine ambayo hayakuwepo kwenye mkataba”

“Mapipa, uzi na kingo ambazo bado zipo barabarani ni kwa sababu za kiusalama kwa Watumiaji wa barabara, haina maana ujenzi umekwama” asema Gerson Msigwa.
Screenshot_20211001-190313_Instagram.jpg
 
Kwenye habari za biashara na viburudisho leo, Kampuni ya Tanzania Breweries leo imetangaza rasmi kuiingiza sokoni Nchini Tanzania bia mpya iitwayo Flying Fish ambayo TBL wameitaja kama ya kipekee ikiwa na ladha tamu ya limao na itawafaa pia wale wasiopenda uchungu kwenye bia.

Kwenye taarifa yao TBL wamesema "kama mliona video zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Wavuvi kumuona baharini Samaki anaepaa.... samaki mwenyewe sasa ndio hii bia mpya ya Flying Fish, leo ndio tunaizindua rasmi na kutakuwa na tukio pale Kitambaa Cheupe Tabata kuanzia saa kumi na moja jioni"
Screenshot_20211001-190530_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom