FEISAL SALUM FANYA YAFUATAYO ILI UWE BORA ZAIDI
:
Imeandaliwa na Gen FUMBWE
:
Feisal SALUM kwasasa ndiyo kiungo mzawa Watanzania tunajivunia kuwa naye kwa uwezo wa kiufundi na kimbinu uwanjani.
Pamoja na yote hayo ila amekuwa akipata tabu pindi akutanapo na viungo wanaotumia ukabaji wa karibu (MAN TIGHT MARKING), wepesi na wenye kasi kwenye kukaba.
Mfano wa viungo hao ni Sadio KANOUTE wa Simba SC. Tafuta mkanda wa video mechi ya SIMBA vs YANGA uone FEISAL alivyopata tabu kipindi cha kwanza wakati KANOUTE akicheza kwenye majukumu ya ulinzi (DEFENSIVE ROLES).
Mfano mwengine ni jana vs GEITA. Mwl. NDAIRAGIJE alipoona Feisal na FARID wametawala katikati, dakika ya 30+ aliamka na kutoa maelekezo kwa viungo wake wafanye "MAN TIGHT MARKING" ambapo Yusuf KAGOMA alifanikiwa kumkaba FEISAL na kusababisha UBUNIFU na MIKOGO yake tuliyoizoea kutoonekana.
Kuna muda FEISAL alipaniki hadi alikataa kupokea mkono wa FAIR PLAY FEISAL baada ya kukutwa na KAGOMA.
USHAURI
Feisal ili awe bora zaidi inampasa ajifunze kucheza na viungo wa aina hii kwa kufanya yafuatayo:
1). Afanye mazoezi ya kuongeza "reaction speed". Hii itamsaidia kufikia mpira haraka hata ikitokea akipigwa "MAN TIGHT MARKING".
2). Aongeze kasi ya "side movements" ili kuwakimbia wapinzani na kutengeneza nafasi kati yao (SPACE CREATION).
3). Afanye upokeaji wa mpira kwa kugeuka haraka na kumuangalia mpinzani wake.
HITIMISHO
Endapo akifanya hayo na kuongeza na aliyonayo, hakika hakuna kiungo mkabaji wala beki atathubu kumkaba FEISAL hata wakimkamia kwa kiwango gani.
:
:
Imeandaliwa na Gen FUMBWE