Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20210929-075313_Instagram.jpg
 
Wanajeshi wanne wa Rwanda wameuawa na wengine 14 wamejeruhiwa katika Oparesheni ya kijeshi dhidi ya Wanamgambo wenye itikadi kali nchini Msumbiji katika Jimbo la Cabo Delgado, hii imetokea zikiwa zimepita siku chache tangu Rais wa Rwanda Paul Kagame alipokwenda Msumbiji na kukutana na Rais wa Msumbiji Filippo Nyusi ambapo kwa pamoja waliwapongeza Wanajeshi wa Nchi zao kwa kupambana na Kikundi hicho.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rwanda kutangaza majeruhi katika kikosi chake cha Wanajeshi 1,000 tangu waanze Oparesheni nchini Msumbiji.

Jumamosi iliyopita Rais wa Msumbiji na Rais wa Rwanda walikuwa wanawapongeza Wanajeshi ambao wamejitoa kupambana na Wanamgambao hao.
Screenshot_20210929-153253_Instagram.jpg
 
Baada ya gari lake aina ya Brevis kuchomwa moto usiku wa kuamkia leo Sept. 29 2021 kama inavyoonekana kwenye post iliyotangulia, Mbunge wa Jimbo la Mbozi mkoani Songwe George Mwenisongole amesema ni kwa takribani miezi miwili sasa amekuwa halali nyumbani kwake.

Amesema amekuwa akilala maeneo tofautitofauti kwani kuna Watu anahisi wamekua wakimfuatilia maisha yake hivyo anafanya hivyo kuwakwepa ambapo wakati tukio hili la moto linatokea hakuwepo nyumbani kwake na analihusisha na vita ya kisiasa.



Screenshot_20210929-153411_Instagram.jpg
 
Mfanyabiashara na Muwekezaji wa Simba SC Mo Dewji ambaye anamiliki 49% ya hisa za Simba SC kwa thamani ya Tsh Bilioni 20 leo ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba SC na nafasi yake itachukuliwa na aliyekuwa Makamu wake Salim Abdallah (Try Again), MO Dewji amefikia uamuzi huo kutokana na mara nyingi kutokuwa nchini.

“Mmetuunga mkono kwa miaka minne ya Uongozi wangu kama Mwenyekiti wa Bodi, kwenye miaka minne tumepata mafanikio makubwa tumeshinda Ligi mara 4 na kufanya vizuri kwenye Champions League muda umefika kama Mohammed na tumekubaliana mimi nitajiuzulu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC naomba sana msifikie kuwa Mimi nimeondoka Simba bali bado ni Muwekezaji”
Screenshot_20210929-153510_Instagram.jpg
Screenshot_20210929-153527_Instagram.jpg
 
[emoji3578][emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

MTAZAMO WANGU KUJIUZULU KWA MO DEWJI

Kuhusu neno KUJIUZULU ni la kawaida duniani kote, mpirani, siasa na hata kwenye mapenzi! Hakuna mgeni kwenye hili

Ramon Calderon aliwahi kujiuzulu Urais wa Real Madrid na kupisha uchaguzi Mkuu uliomleta Perez kwa awamu ya pili na ikumbukwe hata Perez aliwahi pia kujiuzulu

Perez aliwahi kusema kitu kuhusu watu KUJIUZULU, alisema kuna muda mambo hayaendi kisa wewe, kuna muda unajiona nje ya mfumo na kuhitaji mwingine aongoze na kuna muda masherti kadhaa

Well! MO DEWJI wa Simba kajiuzulu Uenyekiti wa klabu ya Simba na majukumu anayo Try Again! Naomba hapa niseme kitu kuhusu MASHERTI

Moja wapo ya matakwa ya FCC ni kuwa huwezi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na bado ukawa Mwekezaji kwenye timu, ni sawa na kusema kesi ya Nyani umpe Ngedere, hapa walitaka kuondoka CONFLICTS OF INTERESTS

Kujiuzulu kwa MO ni dalili za wazi hivi sasa mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa Simba unaenda kutimia rasmi kwakuwa hata FCC walisema mchakato upo mwishoni kukamilika, pongezi kwa MO

Sababu nyingine ya MO kujiuzulu ni kutokana na ratiba yake! Ni ngumu Mwenyekiti kuwa nje ya nchi zaidi ya miezi mitatu hata kama teknolojia imepiga hatua ila Bodi ni shughuli za kila siku

Mambo mengi yalikuwa hayaendi kutokana na kukosekana kwake, hivyo kujiuzulu kwake kunaleta Mwenyekiti ambae atapatikana kwa muda wote na kujihusisha na shughuli zote

FARHAN unasemaje kuhusu MO kujiuzulu? To me ni uamuzi mzuri kwa maslahi ya klabu as long as anasalia kuwa Investor basi hakuna shida, hii pia itasaidia kuondoa presha, MO personally alikuwa mwepesi kubebwa na presha ya matokeo haswa kutweet (utani tu)

Hawa wakina Salim wanazijua presha, wanajua kuishi nazo kwakuwa wamezizoea sana
Screenshot_20210929-163711_Instagram.jpg
 
[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

Jana niliandika kitu kuhusu Chris Mugalu, tulioelewana tukaelewana na ambao hatukuelewana tukakubaliana kutokuelewana

Nadhani Kocha wa Simba aliishi kwenye presha za Mashabiki na kuamua kumdrop Mugalu kikosini leo! Bila kuwaza namna defense ya Biashara ilivyo imara

Bila shaka mnaosema Mugalu hana jambo mmeona namna Saad Kipaga na Abdul Mangalo walivyocheza kwa kujiachia siku ya leo, walikuwa huru kwakuwa hakuna anaeusumbua mstari wao

Kocha wa Simba aliingia na Standard 4-4-2 na akitegemea mipira mirefu! Akimini Meddie Kagere na John Bocco ni poachers na wanaweza kumpa matokeo lakini haikuwa kweli

Haikuwa kweli kwakuwa kwenye mstari wa mwisho Bocco na Kagere hawana movements, hawawezi kuusumbua mstari na wote wanataka kuchezeshwa! Kimsingi mstari wa juu ulikuwa MFU

Plan B ya Simba ilikuwa huduma kutoka Midfield sehemu ambayo Rally Bwalya pekee ni creative, anaeweza kuifanya timu iflow! Lakini Biashara waliweka tight spaces na kifupi alihitaji forward wa kudrop kufanya link up

Mugalu ni forward pekee pale Simba mwenye huo ubora! Kuja chini walipo viungo na kusaidia timu ipande, kuja kwake chini anakuja na mabeki na hii huwapa nafasi Simba kuzitumia na kupata mabao tangu msimu uliopita

Inafikirisha sana! Timu haina wabunifu na wanyumbufu! Unaanza na kiungo cha Inongo Baka na Erasto Nyoni kisha Bwalya pekee creative, unataka ushindi mbele ya tough team kama Biashara, haiwezekani

Muweke Mugalu ndani kwa style yoyote awe double au awe lone forward bado atakupa kitu cha ziada! Hichi ndicho kimewatesa Simba leo

Hii ndio maana jana niliandika kuhusu Mugalu! Suala wala sio uwanja bali POOR SQUAD SELECTION

Screenshot_20210929-164040_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom