“Leo hii Wanawake mmempa Tuzo Rais wenu, Rais Mwanamke kwa bashasha na furaha kubwa lakini nataka niwaambie Wanawake bado hatujaweka Rais Mwanamke, tulichokichangia sisi ni ile kusukuma mpaka Mwanamke akawa Makamu wa Rais, lakini kufika hapa kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana”
“Sasa Ndugu zangu Rais Mwanamke tutamuweka Mwaka 2025, Wanawake Oyeee, Tanzania Oyee, Ndugu zangu Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana, wameanza kutuchokoza, kuandika kwenye vigazeti ‘Samia hatosimama (kugombea Urais)’ nani kawaambia!?”
“Fadhila za Mungu zikija mikonononi mwako usiziachie, hizi ni fadhila za Mungu, Wanawake tumefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa Nchi hizi, kujenga siasa za Nchi hizi, tumebeba sana Wanaume katika siasa ya Nchi hizi, leo Mungu ametupa baraka mikononi tukiiachia Mungu atatulaani”———Rais Samia Suluhu Hassan akiongea leo Dar es salaam kwenye maadhimisho ya siku ya Demokrasia duniani. View attachment 1939670