Mikono ya kihamu ya Farhan Jr
Klabu zote Kusini mwa Jangwa la Sahara ni FEEDER CLUBS kwa miamba huko Kaskazini mwa Afrika ambazo tunaziita BIG CLUBS
Kwenye kila msimu ukifanya vizuri una uhakika wa kuuza Wachezaji wengi muhimu kuelekea klabu hizo kubwa, hapo lazima uwe na PLAN B
Kwenye dirisha hili la usajili Simba wameuza Clatous Chama na Luis Miquisson, lakini fahamu kuwa hata Rally Bwalya alikuwa mbioni kuondoka ijapo haijatimia
Simba wamefanya kitu gani kuendana na kasi ya Wachezaji wake kuondoka kwenda kwenye malisho makubwa zaidi? Ndipo hapo kuna kitu klabu zote FEEDERS duniani wanafanya
Tutazame kitu kuhusu SIMBA VS AGENCIES! Niliwahi kusema mahusiano ya Simba na Kampuni kubwa za Uwakala barani Afrika umewapa malipo makubwa sana, ikiwemo kuchukua wachezaji kwa bei ndogo na kuuza kubwa
Ndio maana kuelekea Pre Season na dirisha la Usajili Simba walipokea maombi ya wachezaji 74 Afrika nzima hii wakitaka kujiunga na Simba, ila sote tunafahamu Simba bado hana scouting network kubwa Afrika, hivyo jicho lake ni AGENCIES
Wao wanaona sehemu kubwa Afrika, wamewaletea vijana wengi wadogo sana ambao wanafahamu baada ya muda itakuwa biashara kubwa! Simba itafaidika, wao watafaidika na Mchezaji atafanikiwa
Kwanini Simba hawakutangaza wapi wanaenda wachezaji wao, Chama na Miq mapema? Lakini ni kwenye eneo hili la mahusiano kati ya Klabu, Wakala na Klabu anayoenda! EXCLUSIVITY ni kanuni ya kibiashara, Simba walikubali kutunza siri kwa engo ya kuitazama Kesho yao kibiashara
Al Ahly walipofika muda wao wakamtangaza Miquisson, Berkane ulipofika muda wao wakamtangaza Chama, hii ndio BUSINESS PERSPECTIVE, usinyee kambi
Simba wao wanafahamu ukweli kuwa Afrika ina Wachezaji wengi bora tena wa bei nafuu, ila unahitaji macho ya AGENCIES wakuletee kitu hicho, ndio maana wapo nao karibu