Makapuku Forum

Makapuku Forum

KWA TAARIFA YAKO MAKAPUKU FAMILY
: Ukikaa gizani kwa zaidi ya siku tatu, unaweza kupofuka


Utakapoamua kujifungia katika giza totoro unaweza kuwa kipofu. Kwa mujibu wa wachambuzi kutoka tovuti elimishi ya quora, tatizo hili linaweza kuwa ni la muda tu na hali yako kurudi baada ya muda.
Hata hivyo, ukikaa katika giza kwa siku tatu mfululizo utapofuka na kusababisha hisia zingine za mwili wako kufunguka zaidi na kukufanya uweze kufanya mambo bila kuona.
Macho ni moja ya baraka tuliyopewa, kuishi bila macho ni dhana inayotisha. Mambo mengi tunayofanya kila siku hutafsiriwa kwa kupitia macho kwenda kwenye ubongo.
Ni kweli tunategemea sana macho yetu, kama hatuoni, ni ngumu kuelewa na tutashindwa kufanya mambo mengi ya kila siku. Pata picha maisha bila macho, japo ni vigumu, lakini umeshawahi kufikiria watu wenye ulemavu wa kutoona? Watu milioni 39 duniani hawaoni.
Kila mwaka maelfu ya watoto wanazaliwa na upofu. Wengine hupofuka kutokana na magonjwa.
Tiba nyingi zinafanyiwa utafiti, japo baadhi ya magonjwa yanayosababisha upofu hayatibiki. Watafiti wengi pia wanaendelea kujitahidi kutengeneza macho ya bandia.
 
Cristiano Ronaldo wa Manchester United

Real Madrid:
438 games
450 goals

Man Utd:
292 games
118 goals

Juventus:
134 games
101 goals

UCL:
176 games
134 goals

La Liga:
292 games
311 goals

PL:
196 games
84 goals

Serie A:
98 games
81 goals

Portugal:
180 games
111 goals

Cristiano Ronaldo's incredible record.
Screenshot_20210902-180011_Instagram.jpg
 
Baada ya Cristiano Ronaldo jana kufunga goli mbili kwenye mechi ya Portugal vs Ireland na kuifikia rekodi ya kuwa Mchezaji mwenye magoli mengi kwenye Timu ya Taifa, ameingizwa kwenye kitabu cha kumbukumbu za rekodi za dunia cha Guiness.

Ronaldo amempokonya rekodi hiyo Mchezaji wa Iran Ali Daei mwenye magoli 109 ambapo mpaka sasa Ronaldo ameichezea Ureno mechi 180 na Daei ameichezea Iran mechi149.


Nawakumbusha tu huyo ni Ronaldo wa Manchester msimu huu
Screenshot_20210902-180814_Instagram.jpg
 
: • Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo amekwenda Bagamoyo Pwani ikiwa ni muendelezo wa kurekodiwa vivutio vya Utalii vya Tanzania kutakakosaidia kuitangaza zaidi Tanzania, kuongeza Wawekezaji na Watalii ambapo akiwa njiani alisimama Tegeta na kuongea na Wananchi.

“Naomba mniruhusu niendelee na safari niko na Timu ya wapiga picha wa Kimataifa wanapiga picha kwenda kutengeneza Filamu ya Kitanzania, filamu ile tutaizindua Marekani na itaoneshwa Ulimwengu nzima, ikioneshwa itatusaidia kuitangaza Tanzania, itaongeza Watalii na Wawekezaji nchini”

“Watu watatujua Tanzania ni kina nani siasa zetu tunaendeshaje, ule uongo unaopelekwa sasa hivi watakuwa wamepata ukweli watakapoona Filamu ile, kwahiyo naomba mniruhusu niendelee na safari, Crew imeshafika Bagamoyo inanisubiri na kwa bahati nzuri Mimi ndio Tour Guide ninayetoa maelekezo” ———Rais Samia akiwa Tegeta asubuhi hii njiani kuelekea Bagamoyo.
Screenshot_20210902-181711_Instagram.jpg
 
Cristiano Ronaldo wa Manchester United

Real Madrid:
438 games
450 goals

Man Utd:
292 games
118 goals

Juventus:
134 games
101 goals

UCL:
176 games
134 goals

La Liga:
292 games
311 goals

PL:
196 games
84 goals

Serie A:
98 games
81 goals

Portugal:
180 games
111 goals

Cristiano Ronaldo's incredible record.View attachment 1921248
The Beast!
 
: • Rais Samia Suluhu Hassan leo akiwa Tegeta Dar es salaam njiani kueleka Bagamoyo ameahidi kulifanyia kazi ombi la Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima la kujengewa shule ambapo amesema fedha zitakazoijenga shule hiyo ni zile zinazotokana na tozo mpya.
Screenshot_20210902-182024_Instagram.jpg
 
Siku chache tangu kuuawa kwa Hamza na polisi August 25, 2021 baada ya kuwaua kwa risasi Askari watatu na Mlinzi mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi jirani ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amezungumza leo Mkoani Mwanza na kusema uchunguzi uliyofanywa na Polisi umebaini kwamba Hamza Mohammed alikuwa Gaidi wa kujitoa mhanga.

“Uchunguzi wetu uligusa mambo matatu, kwanza tulitaka kujua Hamza Mohammed ni nani, nini kilimsukuma Hamza kwenda kufanya tukio lile na kutaka kutambua mshiriki mwingine katika tukio hilo”

“Hamza amekuwa akijifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ambayo kwa kipindi kirefu amekuwa akijifunza mambo ya kigaidi kwa kuangalia mitandao ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ISIS yanayoendelea na wagaidi wengi hujifunza kupitia mitandao hiyo”


“Tabia zake na vitendo vyake alivipata kupitia mawasiliano aliyokuwa nayo na Watu wanaoishi katika Nchi zenye matendo ya kihalifu ikiwemo ugaidi hasa wa kupitia mtandao yanayojulikana kama "Radicalisation through social media)”
Screenshot_20210902-182209_Instagram.jpg
 
“Kumekuwa na mijadala mbalimbali kwamba ni kwanini Hamza aliwashambuliwa Askari pekee, ni kweli aliwashambulia Askari wa kwanza akachukua silaha zao, akashambulia Askari mwingine wa usalama Barabarani akataka kwenda kumshambulia Askari mwingine anayelinda Ubalozi wa Ufaransa hakufanikiwa, Gari la Askari lilipopita pia alilishambulia”

“Duniani kote Mtu yoyote mwenye viashiria au tabia za kigaidi target yake kubwa ni Askari awe Askari wa Jeshi, Askari wa Polisi au Askari yoyote na chuki kubwa ya Magaidi ni hawa Watu wa vyombo vya dola na sio jambo la kwanza tumeona Askari wa Kituo cha Polisi Stakishari, Ushirombo wakishambuliwa na kuuawa, tumeona Kibiti mara kadhaa Askari wameshambuliwa tena akiwepo Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya wakauawa, Tanga, Nairobi na maeneo mengine mengi tu Askari wanauawa”

“Kwahiyo tunawaomba Wananchi kwenye matukio haya makubwa tunapoomba tupewe muda tufanye uchunguzi kisha tutarudi Wananchi wawe watulivu waaache kuhisi watupe muda tufanye kazi”

“Niwakumbushe Wananchi Jeshi la Polisi limejitoa mhanga na kuwalinda kuhakikisha wako salama ndio maana unaona tunaweza kupoteza maisha yetu kwasababu ya kuwalinda Wananchi wa Nchi hii, mfano suala la Hamza ndio mfano nzuri kwamba tupo tayari kupoteza maisha yetu kwa ajili ya ulinzi wa Watu na mali zao, uliona Mtu mwenye silaha 3 moja kubwa na mbili ndogo anarusha risasi lakini Askari wanakwenda kushambuliana nae ana kwa ana kwa ukaribu lakini Askari wale ukiwapiga risasi nao wanakufa”—— Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Camilius Wambura.
Screenshot_20210902-182356_Instagram.jpg
 
Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo leo amepima uzito akiwa na Mpinzani wake Julius Indongo kutokea Namibia ambaye atapambana nae kesho September 3 2021 Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam katika pambano la round 12 la uzito wa 69 Kg
Screenshot_20210902-182702_Instagram.jpg
Screenshot_20210902-182720_Instagram.jpg
Screenshot_20210902-182740_Instagram.jpg
Screenshot_20210902-182758_Instagram.jpg
 
“Kumekuwa na mambo yameendelea mitandaoni kwamba kwanini Polisi hawakumkata Hamza akiwa mzima ili kupata taarifa zaidi kutoka kwake, hilo Polisi walijitahidi matokeo yake wamejeruhiwa Polisi 6 na mpaka sasa wamelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili”

“Suala la mapambano na Mtu mwenye silaha hilo huamuliwa na Askari aliye field ni wakati gani amkamate, amjeruhi au amuue, mapambano ya ana kwa ana kama ilivyokuwa kwa ishu ya Hamza tuwaachie Polisi, inashangaza kwamba pengine ilihitajika wafariki Askari zaidi ya watatu ndio Watu wangejua kulikuwa na umuhimu wa kumuua yeye”

“Kumekuwa ikisemekana kwamba Hamza alijisalimisha kwa kupiga magoti na kunyoosha mikono la hasha walioangalia ile clip vizuri Hamza hakujisalimisha, Hamza alipiga magoti baada ya kushambuliwa, tuna uhakika Polisi waliokuwa front line siku ile walifanya kazi nzuri”

“Imeendelea kusemwa kwamba Askari waliogopa kwamba Hamza angepona angeeleza mengi kuhusu Askari, hilo sio kweli, Hamza alikuwa Gaidi wa kujitoa muhanga hakuna ambacho Askari wangeogopa kwanza hakuna Askari ambaye alikuwa anamfahamu zaidi ya yeye kupora silaha na kuanza kuwashambuliwa na Hamza hakuwa Mtu mwema” ——— Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camilius Wambura.
Screenshot_20210902-183002_Instagram.jpg
 
Baheshta Arghand ambae ni Mwandishi wa Habari wa kwanza Mwanamke wa Afghanistan kumuhoji Afisa wa Taliban Live kwenye TV baada ya Wanamgambo hao kushika Nchi, ameikimbia Nchi hiyo na sasa anaishi kama Mkimbizi Qatar.

“Najua Familia yangu itatishiwa na Taliban kwa ajili yangu, nimelazimika kuondoka Afghanistan maana sikuwa na raha, Wataliban wanataka ufanye kile wanachotaka wao, hakuna uhuru wa habari, sioni kesho yangu, nataka kuwa sauti ya Wanawake wenzangu wanateseka, naomba Jumuiya za Kimataifa fanyeni kitu kuwasaidia Wanawake wa Afghanistan”
Screenshot_20210902-183301_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom