

MIKONO YA KIHAMU YA FARHAN JR
Wakati Cesc Fabregas anahitajika na Arsenal alikuwa na umri wa miaka 16 tu! Alikuwa kijana mdogo sana sana
Mama yake mzazi anaitwa Nuria Fabregas, alisema wazi kuwa hakuweza kukubali mtoto aondoke kirahisi, lakini akasema alikuwa anajua ni Mtoto lakini ni Mwanaume pia
Baada ya Fabregas kutua Jijini London, Kwenye baridi kali sana na maisha tofauti na mitaa ya kwao huko Arenys der Mar, Catalunya
Klabu ya Arsenal kupitia Profesa Arsene Wenger, walifahamu vyema kuwa Kijana wao bado mdogo sana! Wakaajiri Mama wa Kiingereza awe anamlea kama Mwanae, klabu ilikuwa inalipa mishahara yake
Kama hivyo haitoshi, klabu ya Arsenal ilimpa kazi ya ziada Gwiji ambaye ni Marehemu sasa, Jose Antonio Reyes awe Kaka yake wa hiyari na amfanye ajisikie nyumbani, nae alikubali! Mwisho ikawa historia
Nimesema hayo yote kwakuwa nataka kusema jambo kuhusu kijana PETER BANDA, usajili mpya wa klabu ya SIMBA ana umri wa miaka 20 tu, amezaliwa September 22, 2000
Niliwahi kufanya tafiti yangu nyepesi nikagundua Banda alikuwa na wakati mgumu wakati mwingine huko Moldova kutokana na umri wake na mazingira, ili Mtoto ajisikie nyumbani kuna namna klabu ya Simba ikubali gharama
Kitu cha kwanza! Ule usajili wa DUNCAN NYONI kutoka Malawi licha ya ubora wake mkubwa sana ila nyuma ya pazi pia Simba walimsajili kwa ajili ya Kijana Peter Banda, wote Wamalawi na wote wajisikie nyumbani
Anachofanya Simba ndicho alichowahi kufanya Arsenal juu ya Fabregas ili Mtoto awe anajisikia nyumbani, hii ndio maana halisi ya uwekezaji na projects za wachezaji kwenye mpira wa miguu
Mwisho, Peter Banda ni Kijana mwenye imaan ya Kilokole! Wakati naandika hii ni kuwa klabu ya Simba imepambana kumsaka Mama wa Kilokole kwa ajili ya kumlea Kijana na Familia yake, Klabu pia inalipia gharama hizo! Hii pia Arsenal waliwahi kufanya hivyo
Hivyo ndivyo klabu kubwa duniani zinalinda projects za wachezaji wa muda mrefu, wachezaji wenye potential kubwa! Unaingia gharama kwa mafanikio ya muda mrefu