“Wakati tukiwa Morocco tuligawanyika katika makundi, kuna wachezaji walifanya mazoezi lakini wengine walikutana na changamoto na hatukuwa nao sehemu ya mazoezi.
.
“Tumerudi hapa kwa makundi, hatujafanya mazoezi kwa pamoja, pengine ndio maana tumepoteza mchezo wa kirafiki na Zanaco.
.
- Nasreddine Nabi.
Zlatan Ibrahimovic afunguka alivyoachana na mchumba kisa kuombwa mkwanja:
"Girfriend wangu wa kwanza alikuwa mwanasoka, kuna siku aliniomba nimpatie Euro 100,000, alisema alitaka kuhudhuria harusi huko USA.
.
Nilimwambia "sikiliza mrembo wangu, ukitaka kuchepuka wewe chepuka kwangu mimi freshi tu . "
.
Ukweli ni kwamba endapo ningedumu naye, leo hiii angekuwa tajiri kuliko Zlatan wakati hana ajira. Nilimwambia awe mwangalifu anapozungumzia masuala ya pesa. Mimi ni mtawala, kama hapendi, sio mrembo kwangu."
Kama nawaona wanaume ambao hampendi kuombwa hela na wapenzi wenu mtakavyokuwa upande wa Zlatan
Chelsea Yashtakiwa na FA kwa Kushindwa Kudhibiti Wachezaji
Shtaka hilo linahusiana na visa viwili kufuatia uamuzi wa mwamuzi Anthony Taylor kumtoa beki Reece James kwa kadi nyekundu na kuipatia Liverpool penati katika kipindi cha kwanza baada ya beki huyo kuamuliwa kuwa alitumia mkono wake kwa makusudi kuzuia shuti.
.
Wachezaji wa Chelsea walimvaa mwamuzi kwa hasira, mlinzi Antonio Rudiger na mlinda mlango Edouard Mendy wakiwa vinara wa vurugu hizo, na mzozo uliendelea baada ya mwamuzi Taylor kupuliza filimbi ya mapumziko
.
Blues imeshtakiwa kwa makosa mawili wa Sheria ya FA E20.1 na imepewa hadi Ijumaa kujibu.
Rayo Vallecano ipo kwenye hatua nzuri ya kumsainisha straika wa zamani wa Manchester United na Chelsea, Radamel Falcao, 35, kwa mkataba wa miaka miwili.
.
Falcao amevunja mkataba wake na Galatasaray vilevile
amekataa ofa kibao kutoka Italia na nchi nyingine kubwa barani Ulaya. Sasa Rayo inataka kuinasa saini yake.
Beki wa kulia wa Atletico Madrid na England, Kieran Trippier, 30, anatarajiwa kujiunga na Manchester United dirisha lijalo la majira kiangazi pale mkataba wake utakapomalizika.
.
Man United ilitamani sana kuipata saini ya Trippier katika dirisha lililopita
lakini Atletico ilikataa ofa yao ya Pauni 18 milioni. Mkataba wake unamalizika mwaka 2022.
Kumbe Martial Aligoma kuuzwa
.
Staa wa Manchester United na Ufaransa, Anthony Martial, 25, alikataa ofa ya kujiunga na Olympique Lyon dakika za mwisho za dirisha lililopita la usajili.
.
Man United ilikuwa inahitaji kumuuza mchezaji huyu kwa sababu kocha wao Ole Gunnar Solskjaer haonekani kuwa na mpango wa kuendelea kumtumia msimu huu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.