

Farhan Jr
Miaka ya 1970 nchini England kupitia FA yao waliwahi kupiga marufuku matangazo kwenye jezi za wachezaji (Kit Sponsors) lakini baada yakabatilishwa
Yote hayo ni mabadiliko ya biashara ya mpira na sasa MERCHANDISING ni sehemu kubwa zaidi!
Kwenye wadhamini wa jezi (KIT SPONSORS) kuna Main Sponsor huyu ni Mdhamini Mkuu anaetoa pesa ndefu kuliko wote kisha kuna CO-SPONSORS ambao ni Minor wanaotoa pesa ndogo
Hakuna kanuni ya kudhibiti idadi ya Wadhamini kwenye jezi bali kuna vigezo na Masherti ya udhamini kulingana na Sheria za nchi au FA haswa kwenye mgongano wa kimaslahi
Kwanini watu wanasema jezi ya Simba ina Wadhamini wengi?
Kabla sijajibu nadhani tukaitazame jezi ya Santos ya Brazil, Al Ahly ya Misri na kidogo Fiorentina ya Italia yenye wadhamini watano, sahau kidogo kuhusu timu za Sudan maana zipo mbali kimpira ni dhambi kuwatumia kama mfano, mifano nimekupa ya nchi za kimpira
Well Simba kwenye jezi yake ana SPORTPESA, MO EXTRA, MO PROTECTOR SABUNI, MO SIMBA FOUNDATION jumlisha na free of charge Ad ya VISIT TANZANIA! Hapo matangazo ya pesa yapo matatu tu
Sportpesa anaweka pesa inayokadiriwa juu ya Million 900, MO EXTRA na MO SABUNI ni million 400 kwa Mwaka, hiyo MO SIMBA FOUNDATION ni Asasi ya Kijamii ni ya Simba haiwezi kutoa pesa kwakuwa ni msaada kwa Jamii
Tuje kwenye VISIT TANZANIA, Kutokana na CAF kuwa na Kampuni nyingine ya ubashiri, haikuwezekana Simba kwenda na Sportpesa kama Main Sponsor, hapa kwa heshma ya kimkataba klabu ikaona itangaze nchi yake
MO angekuwa mbinafsi ile nafasi pale kifuani si ingekaa Bidhaa yake? Wangekuwa wabinafsi kwenye idara ya Masoko ya CAF si wangepeleka matangazo yao binafsi? Hapa tukubaliane wameheshimu mkataba, hakuna kitu cha bure pale
Labda watu waseme kuhusu FONT SIZE inayotumika ni kubwa kwenye matangazo, again sio mbaya pia kuinadi biashara ya anaeweka pesa yake plus VISIBILITY