Makapuku Forum

Makapuku Forum

Baada ya Mitandao, Radio na TV mbalimbali Tanzania kuripoti Mkali wa Bongofleva Nandy kusainiwa na Msanii wa Nigeria Oluwatosin Ajibade maarufu Mr. Eazi, leo ameweka wazi kwamba hakuna kitu kama hicho isipokua wao ni Business Patners tu.

"Mimi na Mr. Eazi ni Business Patners sio kwenye mziki tu hata biashara sababu kutoa mziki kuna vitu vingi nyuma ya mziki wetu, maswali yamekua mengi sana page zinaandika sana mara nimesainiwa, mara hivi mara vile...... noo guys, mimi ni Msanii ninaejitegemea na kushirikiana na Wafanyabiashara wenzangu, punguzeni habari fake" ——— Nandy
Screenshot_20210807-192539_GBInsta.jpg
 
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Sara Msafiri amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Butamo Ndalawa kumsimamishwa kazi Afisa Mazingira wa Mji mdogo wa Mlandizi baada ya kushindwa kusimamia usafi katika eneo hilo.

DC Msafiri pia ametangaza kuweka zuio kwa Wafanyabiashara wanaoendesha biashara zao pembezoni mwa Barabara kusitisha shughuli zao mpaka pale watakapofanya usafi katika mifereji inayopitisha maji.

Msafiri ametoa kauli hiyo wakati wa zoezi la usafi ulioongozwa na DC huyo pamoja na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama wakiwemo JWTZ, JKT, Polisi, Magereza, Mgambo pamoja na Wananchi wa Mlandizi na Wafanyakazi wa Halmashauri hiyo.
Screenshot_20210807-192729_GBInsta.jpg
Screenshot_20210807-193029_GBInsta.jpg
 

Attachments

  • Screenshot_20210807-192729_GBInsta.jpg
    Screenshot_20210807-192729_GBInsta.jpg
    64 KB · Views: 16
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Tanzania Profesa Abel Makubi amemsimamisha kazi Muuguzi Scholastica Khanje wa Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Arusha kwa kosa la kufanya mzaha wa chanjo ya Corona kwa kuigiza kumchoma sindano Abdallah Kwesiga, Makubi pia amelitaka Baraza la Uuguzi na Ukunga kumchukulia hatua stahiki.

Ofisi ya Rais- TAMISEMI jana ilisema imesikitishwa na kitendo cha Watumishi wawili Mwalimu Omary Kwesiga, Mkuu wa Idara Elimu Msingi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na Scolastica Kanje, Afisa Muuguzi Msaidizi Hospitali ya Mkoa wa Arusha kufanya igizo kwenye zoezi la chanjo ya Covid-19 kinyume cha taratibu na kanuni za utoaji wa chanjo hivyo kuleta sintofahamu kwa Wananchi kuhusu zoezi la chanjo linaloendelea nchini kote.

Kufuatia hali hiyo, Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu alimuagiza Katibu Mkuu OR-TAMISEMI kumsimamisha kazi Mwalimu Omary Kwesiga, huku akiagiza pia Scolastica apelekwe kwenye Baraza la Wauguzi na Wakunga kwa hatua zaidi.
Screenshot_20210807-193406_GBInsta.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge leo Agosti 7 akiwa na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ameshiriki mazishi ya Watoto watano waliofikwa na umauti kwenye ajali iliyohusisha Pikipiki na Fuso eneo la Kata ya Kimange Halmashauri ya Chalinze.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa amesema August 6 saa 1 :15 jioni gari aina Mitusubish Fuso namba 198 CWN likitokea Dar es salaam kwenda Arusha lilimgonga Mwendesha Pikipiki kusababisha vifo vya Wanafunzi wanne palepale na mmoja kufariki akipatiwa matibabu Hospital ya Jeshi Kihangaiko.

Wanafunzi hao watano wa Kimange Sekondari walikuwa wamepakiana kwenye Pikipiki wakitokea Kimange kuelekea Mbwewe na walikuwa wakitokea michezoni shule jirani ya kwamakocho Sekondari.

Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni uzembe wa Dereva wa Fuso lililokua kwenye mwendo kasi uliosababisha kushindwa kulimudu na kupelekea kumgonga Mwendesha Pikipiki akiyekuwa mbele yake, Polisi wanamshikilia Dereva wa Gari hilo kwa hatua zaidi za kisheria.

Kunenge ametoa pole sana kwa Familia na Wananchi wa Kata hiyo kwa Msiba mkubwa ambao wameupata———“Kwa niaba ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan nitoe pole nyingi kwenu”.
Screenshot_20210807-193554_GBInsta.jpg
Screenshot_20210807-193611_GBInsta.jpg
Screenshot_20210807-193628_GBInsta.jpg
Screenshot_20210807-193645_GBInsta.jpg
Screenshot_20210807-193701_GBInsta.jpg
 
Wananchi wa Goroka na mzinga, jimbo la Mbagala wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam wakishirikiana na Mbunge wa jimbo hilo Abdallah Jafari Chaurembo, wameanza kutekeleza ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 42. litakalogharimu kiasi cha Sh20 milioni hadi kukamilika kwake.
Screenshot_20210807-194356_GBInsta.jpg
 
Rais Tanzania Samia Suluhu Hassan, aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokutana leo Jumamosi Agosti 07,2021 Ikulu Jijini Dar es salaam.
Screenshot_20210807-194553_GBInsta.jpg
 
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa na vilevile Mbunge wa jimbo la Ushetu Elias Kwandikwa umefikishwa Kijijini kwao Butibu halmashauri ya Ushetu Wilaya ya Kahama leo kwa kutumia Helikopta ya Jeshi la Anga la Tanzania.

Tayari Viongozi mbalimbali wamewasili Kijijini hapa akiwemo Mkuu wa Majeshi CDF Venance Mabeyo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dr. Philemon Sengati.

Marehemu Elias Kwandikwa atazikwa kesho August 9 hapahapa Kijijini kwao Butibu na shughuli hiyo inatarajiwa kuongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa .
Screenshot_20210808-182658_GBInsta.jpg
Screenshot_20210808-182720_GBInsta.jpg
Screenshot_20210808-182749_GBInsta.jpg
Screenshot_20210808-182808_GBInsta.jpg
Screenshot_20210808-182830_GBInsta.jpg
Screenshot_20210808-182844_GBInsta.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom