“Kauli ya Askofu Gwajima kuhusu chanjo na dhamira ya Serikali kuleta chanjo nchini haikubaliki, ni hatari kupotosha Watu wanaotuamini kuhusu mambo ambayo hatuna utaalam nayo” asema Mbunge wa Bumbuli January Makamba.
“Mjadala kuhusu usalama wa chanjo ni sahihi lakini kiapo kwamba Serikali imeileta kuwadhuru Watu si sahihi” ——— January
January Makamba ameandika hayo kufuatia Askofu Josephat Gwajima ambae ni Mbunge wa Kawe kupinga kitendo cha Serikali kukubali kupokea chanjo ya Corona kwasababu ya kile alichokiita ni mpango wa Mataifa ya nje kuwaangamiza Watanzania na kusema ambao wanaipigia chapuo chanjo hiyo wameshakula hela za watengenezaji wa chanjo hiyo.
“Naomba watanzania wenzangu tusikubali kuchanjwa kwa sababu chanjo hii hatuna uhakika na usalama wa chanjo hiyo, Mimi nina akili timamu ukiona napinga hii chanjo ujue haiko salama"——— alisema Askofu Gwajima.
View attachment 1869275View attachment 1869277