Makapuku Forum

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Kherry James kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Basilla Mwanukuzi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, Basilla aliwahi kuwa Miss Tanzania 1998.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Gabriel Zakaria kuwa Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, Zakaria aliwahi kuwa Mtangazaji wa TBC.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mtangazaji Mwandamizi wa ITV/Radio One Abdallah Mwaipaya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mtangazaji Mwandamizi wa ITV/Radio One Abdallah Mwaipaya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mwigizaji Juma Chikoka maarufu Chopa Mchopanga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Afisa Uhusiano wa Clouds Media Group, Simon Simalenga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songwe Mkoani Songwe.
 
Kuna Wakuu wa Wilaya wawili wateule kwenye hii post wote kutoka Mkoani Lindi, Hassan Ngoma ameteuliwa na Rais Samia kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, kabla ya uteuzi huo Ngoma alikuwa DAS Singida.

Kuna Hashimu Komba pia ambaye ameteuliwa kuendelea kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea.
 
Rais Samia Suluhu amemteua Mtangazaji wa Azam Media, Fatma Nyangasa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dar es salaam.
 
Kuna Wakuu wa Wilaya wawili wateule kwenye hii post wote kutoka Mkoani Kilimanjaro, Said Mtanda ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi.

Kuna Juma Irando pia ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Lengai Ole Sabaya ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
 
Hatutaki hizi taarifa na hatuziamini...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…