Makapuku Forum

Rais Samia Suluhu leo ameendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza ikiwa ni siku ya pili, amekagua ujenzi wa Daraja la JPM linalojengwa kati ya Kigongo na Busisi lenye urefu wa kilometa 3.2, barabara unganishi ni kilomita 1.6, gharama za ujenzi ni Bilioni 716 na muda wa kuvuka ni dakika 4 badala ya saa mbili kwa kivuko.
 
Saa mbili za kivuko?sijaelewa hii sentensi ya mwisho
 
Rais Samia leo ameendelea na ziara yake Mwanza kwa siku ya pili, amekagua ujenzi daraja la JPM la Kigongo na Busisi lenye urefu wa KM 3.2, barabara unganishi ni KM 1.6, gharama za ujenzi ni Bilioni 716 na muda wa kuvuka ni dakika 4 badala ya dakika 30 kwa kivuko, ujenzi umefikia asilimia 27.
 
“Sengerema Halmashauri haifanyi vizuri, haipo vizuri kwenye matumizi ya fedha, haikusanyi fedha za kutosha lakini inafuja fedha zinazoletwa, Serikali tumeamua kuleta Wakaguzi maalum kwenye Halmashauri hii kuangalia hesabu za Halmashauri”———Rais Samia akiwa Mwanza leo.

“Kuna madeni Halmashauri ya Sengereama inadaiwa, inashangaza kuona Serikali tunaongeza kila mwaka Bajeti ya dawa na vifaa tiba lakini maeneo mengine unakwenda unaambiwa dawa hakuna hii inaonesha udhaifu wa Uongozi katika eneo husika kwahiyo Sengerema tutaiangalia vizuri”———Rais Samia

“Naambiwa Wananchi Sengerema wanakosa maji kwasababu Wakala wa Maji Sengerema wanadaiwa bili za umeme, sasa kama Wananchi wanalipa kwanini washindwe kulipa na wao bili za umeme ili maji yapatikane!?, hii inaonesha kwamba Sengerema bado kuna kazi kubwa ifanye kwenye nyanja za Uongozi wa Wilaya hii na Halmashauri zake”———Rais Samia

“Sengerema kuna tatizo la Baraza la Ardhi tumetoa kibali Baraza liundwe na tutasimamia uundwaji wake ili kuondoa changamoto za ardhi Sengerema”———Rais Samia
 
Picha mbalimbali za leo hapa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya ambako hukumu ya Mdude Nyagali ilikua ikitarajiwa kusomwa leo, hata hivyo hukumu hiyo ya kesi ya kusafirisha dawa za kulevya imeahirishwa hadi June 28, miongoni mwa waliofika Mahakamani leo ni pamoja na Mwenyekiti Freeman Mbowe pamoja na Joseph Mbilinyi.
 
Mwili wa Mtangazaji Fred Fidelis ‘Fredwaa’ ukitolewa nyumbani kwake Mbezi Beach kuelekea Kanisani kwa ajili ya kuagwa na kisha kusafirishwa kwenda kuzikwa Sanya juu mkoani Kilimanjaro.

Fredwaa ambae aliwahi kuwa Mtangazaji wa Times FM, Radio Free Africa na CloudsFM alifariki jumamosi iliyopita Kawe Dar es salaam kwa ajali ya gari.
 
“Hakimu amekuja ndani ya Mahakama, ametoa taarifa kwamba hajakamilisha kazi ya kuandika hukumu, amepanga tarehe nyingine ambayo ni tarehe 28, kwa niaba ya Chama nawashukuru sana kwa kuja kumtia mwenzetu moyo naomba ninyi wote wa Mbeya mjiandae kuja tena Mahakamani na wala msichoke”

Ameyasema hayo Mwenyekiti wa CHADEMA leo Mahakama Kuu Mbeya baada ya hukumu ya Mwanachama wa CHADEMA Mdude Nyagali iliyokua isomwe leo kuahirishwa ambapo anakabiliwa na kesi ya kusafirisha dawa za kulevya.
 
Rais Samia Suluhu amezindua mradi wa maji safi na usafi wa mazingira wa Mji wa Misungwi Mkoani Mwanza ambao unazalisha lita milioni 4.5 kwa siku, utaunganishwa kwa Wateja 2,158 na kunufaisha Wakazi 64,000 wa Misungwi na jirani, umegharimu shilingi Bilioni 13.77.
 
"Mabenki yanatukopesha lakini riba zake ni kubwa, mimi mwenyewe nimekopa juzi kama mwezi mmoja hivi nimekopa MILIONI 600 katika MILIONI 600 riba ni asilimia 19, hivi tunalipaje?, kipindi kilichopita nilikopa BILIONI 1.532, nimemaliza kulipa wamenipa barua ya kunishukuru riba peke yake wameandika pale kunishukuru MILIONI 918, hiyo ni BILIONI nyingine, tunaomba benki waweze kupunguza riba kama mama jana alivyosema"——— Deo Kasenyenda Sanga, Mbunge wa Makambako.
 
Watu mbalimbali wamejitokeza leo kuuaga mwili wa Mtangazaji Fred Fidelis maarufu Fredwaa leo Kanisa Katoliki St. Gasper Mbezi beach kwa Zena Dar es salaam na kisha kusafirishwa hadi Sanya Juu mkoani Kilimanjaro, kwenye video hii anaonekana Mke wake pamoja na Watoto wake wawili. RIPFredwaa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…