"Nilipoanza shule ya msingi nchini Uingereza nilianza urafiki na mtu aliyenifunza kuvuta sigara,siku ya kwanza nilikohoa mno, ya pili vile vile , ila mwisho wa juma hilo nakumbuka nikiwa mraibu,"
•
Mchungaji Rahab Mwangi anaelezea jaribio lake la kwanza la kuvuta sigara .
Anakumbuka kuwa uraibu huo ulimpatia starehe tofauti lakini hakujua kwamba ungemsababishia madhara ya aina yake.
•
"Uchunguzi ulionyesha uwepo wa moshi wa sigara kwenye mapafu yangu, wakati ambapo nilikuwa nikivuta sigara 20 kwa siku.
•
Vilevile kutokana na uvutaji wa bangi madaktari waligundua kwamba nilikuwa na ugonjwa wa kifua kikuu (TB)"
•
Mwisho wa siku aliolewa na mchungaji
"Mwanzo wa ndoa mambo yalikuwa shwari, mume wangu ambaye pia ni Mchungaji alinipa ushauri na kunipatia nguvu ya kuishi bila utumiaji wowote wa madawa hayo .
•
Kama mke wa mchungaji pia mimi nilijitosa katika shughuli za kanisa , ila sikutamani kuwa mchungaji au kuwa na majukumu ya kuwa mtumishi kama mume wangu.