Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema tangu Mradi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ulipoanza Mabasi yamekuwa yakipungua kutoka 140 hadi 85——-“Watendaji wapo tu ofisini wanapigwa na AC (viyoyozi) wananchi wanaumia, hatuna sababu ya kumbakiza Mtu kama hafanyi kazi”
Amesema wakala huo ulianzishwa na Serikali kwa ajili ya kuondoa adha ya usafiri kwa wananchi lakini Viongozi hao wameshindwa kusimamia vizuri na hivyo kusababisha mradi huo kutoendelea vizuri.
Waziri Mkuu amesema mapato mengi ya Serikali yamekuwa yakipotea kutokana na uendeshaji wa wakala huo———“kwanini ukatishaji wa tiketi haufanyiki kwa njia ya kielektroniki kwa asilimia 100? , tiketi zinauzwa kwa vifurushi”
“Haiwezekani Watu wanafanya ujanjaujanja tu wakuja na tiketi zao za mfukoni halafu wakimaliza anauza za POS (Mashine ya Kielektroniki ya Kukusanyia Mapato) na Wasimamizi wapo tu, kwanini mnauza tiketi kwa vifurushi hamtumii mashine kukata tiketi, Mnaua wakala huu kwa sababu wauzaji wa tiketi wanakuja na tiketi zao na nyingine mnazileta nyinyi”———MAJALIWA