Msichana mmoja anayetambulika kwa jina Happy Nyasumo (18) Mkazi wa Kata ya Majimoto Wilaya ya Serengeti katika Mkoa wa Mara anashikiliwa kwa kosa kumuua Mume wake Bebe Mbogo (26) kwa kumkata kwa panga shingoni kwa madai halikuwa chaguo lake baada ya wiki mbili kupita tangu kufugwa kwa ndoa yao.
Happy aliolewa March 31, Mwaka huu kwa mahari ya ng’ombe sita lakini ndani ya wiki moja Happy alirudi kwao kijiji cha Mosongo na kuwaambia Wazazi wake kuwa huyo Mwanaume sio chaguo lake na warudishe ng’ombe zake, hata hivyo Wazazi walikataa na kumtaka arudi kwa Mumewe kwakuwa ndoa ni kuvumilia.
Akielezea tukio hilo Diwani wa Kata ya Majitoto Johannes Masirori amesema Aprili 14, 2021, saa 4 usiku baada ya Mume wake kulala fofofo Happy alimuua Mume wake kwa kumkata
na panga kali shingoni mara tatu, panga hilo Mumewe alilinoa kwa ajili ya kukatia miti ya kuchomea mkaa.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurdin Babu amethibisha kushikiliwa kwa mtuhumiwa huyo na kutoa rai kwa Wananchi kutojichukulia sheria mkononi pia ameagiza hatua kali za kisheria zichukuliwe endapo uchunguzi utakapokamilika na kumkuta Msichana huyo na hatia.