Kufuatia agizo la Rais Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo chini ya Waziri Innocent Bashungwa pamoja na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari chini ya Waziri Dr. Faustine Ndugulile na zimetatua changamoto mbalimbali zinazotokana na sheria na tararibu za TCRA katika sekta za utangazaji na sanaa.
Kikao cha Mawaziri wa Wizara hizo kilifuatiwa na kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara hizo, miongoni mwa mambo mengi waliyoagiza ni pamoja na kuitaka TCRA kupitia upya kanuni upya ili kupunguza ada za usajili ama kuhuisha usajili wa Online TV———“mapitio ya kanuni yafanyiwe kazi haraka sana ili Bei ya usajili ipungue na kuwasaidie Vijana wengi kujiajiri”
Kwa sasa Blogu, Online Forum na Waombaji wapya wa Radio na Television Mtandaoni wasio na leseni ya Utangazaji unaotumia mitambo iliyosimikwa ardhini hulipia Laki moja ya gharama ya maombi ya usajili, ada ya kupatiwa leseni ni Tsh. Milioni moja, ada ya mwaka ya leseni ni Tsh. Milioni moja na gharama ya kuhuhusisha (Renew) leseni ni Tsh. Milioni moja.
Leseni zote ni za miaka mitatu ambapo baada ya muda huo huitajika kuomba kuhuishwa na kupewa Leseni nyingine kwa anayekidhi vigezo husika.