Makapuku Forum

Makapuku Forum

#MBOWE
Screenshot_20210411-193839_Twitter.jpg
 
“Namshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai wetu, wapo wengi ambao walikuwa hai mara ya mwisho nilipozungumza na Taifa Mwezi January mwaka huu ambao leo hatunao tena, tumempoteza Rais wetu Dr. Magufuli, nasikitika nilishindwa kurejea nchini kushiriki mazishi”———Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Freeman Mbowe akihutubia, Dar es salaam leo

“CHADEMA ilishiriki katika hatua zote za mazishi ya Hayati Dr. Magufuli chini ya uongozi wa Katibu Mkuu wetu John Mnyika, kwa mara nyingine natoa pole kwa Mjane Mama Janeth Magufuli, Watoto, Ndugu, Familia, Rais na Mama Yetu Samia Suluhu na CCM”———MBOWE

“Nimekuwa sipo kwa muda mrefu nimetoka nchini kuanzia December 04, 2020 na nimekuwa nje ya Nchi kwa muda wa miezi minne na wiki moja, nimefanya ziara Nchi mbalimbali Afrika na nje ya Afrika, nyuma yametokea mengi, wakiuliza Mbowe yuko wapi na hata wengine kunibashiria kifo, lakini Mimi ni mzima, sijaumwa wala nini”———MBOWE
20210411_204514.jpg
 
“Namuomba Rais Mama Samia japo amekiri kwamba hatuwezi kuishi tofauti na Dunia, naomba alikimbize jambo hili (la mapambano ya Corona) kwa haraka, Mimi nimekuwa nje ya Nchi nimepata chanjo ya AstraZeneca”———Mwenyekiti wa CHADEMA- Taifa, Freeman Mbowe akitoa hotuba leo Dar es salaam

“Namuomba Rais Mama Samia aweke mikakati ya kupambana na Covid, hiyo Kamati aliyosema ataiunda aiunde haraka, ikiwezekana afikirie namna ya kuchanganya Wataalamu kutoka Nchi mbalimbali wenye uzoefu washirikiane pamoja (kwenye mapambano ya Corona)”———MBOWE
20210411_205628.jpg
 
“Hayati Magufuli atakumbukwa kwa mengi mabaya na mazuri, sifa za kipekee za Hayati Magufuli, moja ni uthubutu wa kufanya maamuzi magumu, alikuwa na kipaji hicho nakiita kipaji, la pili aliamini na kusisitiza uchapaji kazi kwa bidii hii ni sifa nzuri”———Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Freeman Mbowe akihutubia leo Dar es saalaam

“Rais Magufuli hakuwa mvivu, alijituma alifanya kazi usiku na mchana, alisisitiza Watu wafanye kazi, aliishi Falsafa ambayo CHADEMA tunaiamini kwamba asiyefanya kazi na asile, jambo lile sisi tulilikubali, hapa sijadili Maisha yake binafsi, namjadili aliyekuwa Rais wa Nchi”———MBOWE
20210411_205838.jpg
 
“Mimi kwa niaba ya CHADEMA nimemuandikia barua Rais Mama Samia Suluhu Hassan, tumemuomba rasmi kukutana nae, tumueleze ni kwa vipi mioyo yetu inavuja damu na kwa vipi macho yetu yanatiririka machozi, hatukusudii kumzingua nasi hatutegemei kuzinguliwa”———Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Freeman Mbowe akihutubia leo Dar es saalam

“Tumemuomba Rais Samia kukutana nae, hatupo kwenye biashara ya Siasa bali tunautafuta ufumbuzi utakaotutoa kwenye mkwamo huu na utakaorejesha furaha, haki na ustawi kwa Watu wetu wote, tunategemea kumkabidhi Rais mapendekezo ya kina ya namna bora ya kuuanza ukurasa mpya”——-MBOWE
20210411_210216.jpg
 
“Kipekee tunamshukuru Rais wetu leo (Samia Suluhu) ambaye akiwa Makamu wa Rais alikuwa Kiongozi pekee Mwandamizi wa Serikali ya Awamu ya Tano aliyejitwika ujasiri wa kwenda kumjulia hali Tundu Lissu Nairobi alikolazwa baada ya kushambuliwa na wasiojulikana, wanaojulikana”-Mwenyekiti wa CHADEMA- Taifa, Freeman Mbowe akitoa hotuba leo Dar es saalaam

“Tusipomshukuru Rais Samia kwa jambo lile (la kwenda kumuona Tundu Lissu Hosptali Nairobi), tutakuwa hatumtendei haki Mama Samia nimeona leo nimpe shukrani”———MBOWE
20210411_210335.jpg
 
“Mwaka 2018 nikiwa Gerezani Segerea, TRA waliandika barua kwangu kwamba Kampuni yangu moja inadaiwa kodi ya Bilioni mbili kitu ambacho sio Kweli wakafunga akaunti zangu, Juzi pengine baada ya kauli za Mama Samia, TRA wameniandikia kuwa tumeondoa zuio la akaunti zako, tunafungua”———Mwenyekiti wa CHADEMA- Taifa, Freeman Mbowe akihutubia leo Dar es salaam

“Sababu mojawapo iliyonifanya niende Nchi za nje nilienda kutafuta uwekezaji, ni kama sikuruhusiwa kufanya biashara Tanzania, kila biashara niliyojaribu kuifanya ilizuiwa, ilibomolewa, nikaona naweza kufanya biashara Dubai, South Afrika n.k, sasa Mimi ni Mbowe, je wangapi wamekimbia kuwekeza Tanzania?”———MBOWE
20210411_210513.jpg
 
“Hatutashiriki Uchaguzi wowote, bado mifumo ya Uchaguzi ni ileile, Wasimamizi ni walewale, hapana, hatuna haraka ya kwenda kwenye Uchaguzi wowote mdogo wa Udiwani, Wabunge hata Mwenyekiti wa Mtaa hadi tupate mwafaka wa Kitaifa, na nafasi ya Chaguzi za Kidemokrasia”———Mwenyekiti wa CHADEMA- Taifa, Freeman Mbowe akihutubia leo Dar es salaam
20210411_210651.jpg
 
“Unafiki ni jambo baya katika Maisha yetu wote na kama Viongozi wetu wakiwa Wanafiki wasipokuwa wakweli hawatomsaidia Rais Mama Samia, wale wa CHADEMA wakiwa Wanafiki kwangu hawatoisaidia CHADEMA, tujenge Taifa la Watu wanaoheshimu ukweli, ukweli utatuweka huru”———Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Freeman Mbowe akihutubia leo Dar es salaam

“Ili kuipata kesho yetu iliyo salama na bora zaidi, hatuna budi sasa kutafakari kwa uwazi, tulipotoka, tulipo na tunakokusudia au kupaswa kwenda, Adui mkubwa
wa ustawi wa Binadamu ni kuufumbia ukweli macho”———MBOWE

“Pamoja na kuwa kukosea au kutokosea ni mtazamo wa Mtu binafsi, ni ukweli pekee ndio usiohitaji mtazamo wa Mtu, kwani haubadiliki na ndio utakaotupa majibu ya wapi tulipokosea na namna bora na salama ya kwenda mbele”———MBOWE

“Nikiri, baada ya taarifa za Mimi kukusudia kuhutubia Taifa leo, nimeshtushwa na wingi wa ujumbe na ushauri wa Watu mbalimbali, ninaowajua na nisiowajua, wa Vyama mbalimbali na hata waliopo Serikalini”———MBOWE
20210411_210802.jpg
 
“Hatupaswi kumtakia mabaya Rais Samia Suluhu kwa sababu tu ni zao la CCM, bali tunatakiwa kuongeza juhudi na maarifa kumkabili kwa ushindani wenye kujenga na sio wa kubomoa, tunamwombea afanye mema wakati wa utawala wake ili kupata ustawi wa Taifa letu”——Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Freeman Mbowe akihutubia leo Dar es salaam

“Wote tumejifunza, Serikali ikiharibikiwa Nchi yote inaingia simanzi, hii haina maana sisi wa CHADEMA tumegeuka waimba mapambio wa Rais Mama Samia, inatupa sisi changamoto ya kuongeza juhudi za kuboresha sera zetu na kuongeza ushindani wa hoja”———MBOWE
20210411_210951.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amerejea nchini (Dar es Salaam) kutoka Uganda ambako yeye na Mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wameshuhudia utiaji saini wa mikataba ya bomba la mafuta la Hoima-Tanga.
20210411_211120.jpg
 
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania,, Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni leo April, 11, 2021 wameshuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa bomba mafuta ghafi la Afrika Mashariki ( East Africa Crude Oil Pipeline- EACOP) kati ya Serikali na Kampuni za Uwekezaji uliofanyika katika Ikulu ya Entebbe nchini Uganda

Hafla ya utiaji saini mikataba ya mradi huo imehudhuriwa na Mawaziri na wawakilishi wa kampuni hizo za uwekezaji ambazo ni Total ya nchini Ufaransa na CNOCC ya China.

Marais wameshuhudia utiaji saini wa mkataba wa kwanza ambao ni wa uenyeji wa mradi kati ya Serikali ya Uganda na wawekezaji (Total na CNOCC), mkataba wa pili wa ubia ambapo Serikali za Tanzania na Uganda zimetiliana saini na kampuni hizo (Total na CNOCC) na mkataba wa tatu wa masuala ya kikodi na usafirishaji ambapo Serikali ya Uganda imetiliana saini na kampuni hizo (Total na CNOCC).

Pamoja na kushuhudia utiaji saini wa mikataba hiyo, Marais pia wametia saini tamko la pamoja kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo na wameagiza vipengere vilivyobaki katika utekelezaji wa mradi huo vikamilishwe haraka

Mradi huo utahusisha ujenzi wa bomba la mafuta lenye kutumia teknolojia ya joto (heated oil pipeline) lenye urefu wa kilometa 1,445 ambapo kati yake kilometa 1,115 zinapita Tanzania, uwekezaji katika mradi huu unatarajiwa kugharimu Dola za Kimarekani Bilioni 3.5, utazalisha ajira takribani 10,000 wakati wa ujenzi na utasafirisha mapipa Bilioni 6.5 ya mafuta yaliyogundulika katika Bonde la Ziwa Albert nchini Uganda kwenda Bandari ya Tanga nchini Tanzania.
20210411_211257.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom