Makapuku Forum

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ameondoka Tanzania asubuhi hii kwenda Uganda kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema ———> “Rais Samia na Rais Museveni watashuhudia utiaji saini kati ya Serikali ya Uganda na Kampuni itayotekeleza mradi wa kuchimba bomba la mafuta la kutoka hoima kwenda hadi Bandari ya Tanga Tanzania”

“Kumekua na mkanganyiko kidogo mbona mikataba imekua mingi ikisainiwa, mkataba huu unaosainiwa leo ni wa makubaliano kati ya Serikali ya Uganda ambayo ndio Nchi yenye eneo unakotekelezwa mradi huu na hii kampuni”

“Vipo baadhi ya vipengele ambavyo Nchi ya Uganda inatakiwa ikubaliane na hizi Kampuni zilizoungana kutekeleza mradi huu mfano maswala ya makubaliano juu ya matumizi ya maji, mkataba kama huu utakuja kusainiwa Tanzania wa kati ya Serikali ya Tanzania na hiyo Kampuni ya bomba la mafuta”
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…