Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amempongeza na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuunga mkono na kupenda michezo ambapo amekuwa akitoa wito kwa Watanzania kupenda kufanya mazoezi ya viungo na kutoa maelekezo kuwa kila Jumamosi ya pili ya Mwezi iwe siku ya kuhamasisha kufanya mazoezi ya viungo kote nchini, Bashungwa amesema Wizara yake itaendelea kusimamia maelekezo hayo.
Waziri Bashungwa ametoa kauli hiyo baada ya kumaliza mazoezi na mbio za taratibu (jogging) katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma ( Muungano na Dodoma Fitness) Leo April 10, 2021.
“Natoa wito kwa Ma-RAS na Ma-DAS ambao ni Wenyeviti wa Michezo katika Mikoa na Wilaya nchini kuendelea kusimamia maelekezo hayo yaliyotolewa Rais Samia Suluhu Hasssan, moja ya faida kubwa ya mazoezi ni kuimarisha afya ya mwili na hivyo kusaidia kuepuka magonjwa na kupunguza gharama za matibabu”———BASHUNGWA
Kwenye matukio ya picha ni Waziri Bashungwa akinywa uji pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kyerwa, Innocent Bilakwate (kushoto) na Brown Focus kijana kutoka Karagwe ambaye aliwahi kucheza Timu ya Kagera Sugar kwenye timu ya vijana chini ya miaka 20, muda mfupi baada ya kumaliza jogging.