Makapuku Forum

Muigizaji Maarufu Duniani kutoka Kenya Lupita Nyogo amefika Tanzania na kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo ni Hifadhi bora zaidi Duniani.

Mwezi March mwaka huu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr. Damas Ndumbaro alisema Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imetajwa kuwa Hifadhi bora zaidi Duniani na kushika namba moja katika Hifadhi 25 zilizotajwa na mtandao maarufu wa Trip advisor, Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro na Tarangire zimo pia katika orodha hiyo ya Hifadhi bora Duniani.
 
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bakari Msulwa amelazimika kuitembelea Familia ya Seleman Mpange, mkazi wa Kijiji cha Lukulunge Kata ya Mvuha Mkoani humo baada ya Familia hiyo ya Watu 8 kuzua taharuki kwa kutembea wakiwa hawana nguo (kama walivyozaliwa) asubuhi kutoka kijiji kimoja hadi kingine huku chanzo kikitajwa kuwa ni imani za kishirikina.

Katika hali isiyo ya kawaida Watu wanane wa Familia moja wakiwemo Watoto, Wakwe pamoja na Baba na Mama wa Familia hiyo walivua nguo zote na kutembea umbali wa zaidi ya kilometa tatu asubuhi, Aprili 7 mwaka huu wakidai wanatekeleza masharti ya mizimu.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya, Baba wa Familia hiyo, Seleman Mpange amesema ameamua kufanya hivyo ili kutii masuala ya mizimu, mila na desturi za ukoo wao, Mwenyekiti wa kijiji Kibwana Senza amesema Kuwa baada ya kupata taarifa za tukio hilo alitoa taarifa Polisi na kwamba tukio kama hilo hailijawah kutokea katika kijiji hicho.

Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bakari Msulwa amesema msimamo wa Serikali ni kuwa suala hilo linatakiwa kuzungumzwa Kifamilia ili kubaini ukweli wa jambo hilo wakiwashirikisha Wazee wa kimila.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…