Tayari mwili wa Hayati Dr. John Pombe Magufuli umefikishwa Mwanza Airport ambapo umepokelewa na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Waziri Mkuu Majaliwa.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ni miongoni mwa Watu waliofika leo katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kumuaga Hayati Dr.John Pombe Magufuli.
Mwanamuziki Mkongwe wa Muziki kutoka Congo Koffi Olomide ameelezea kusikitishwa kwake kufuatia kifo cha Hayati Dr.John Pombe Magufuli na ametuma pia salamu za rambirambi kwa Familia ya Marehemu na Watanzania wote kwa ujumla.
“Hayati Magufuli ameondoka mapema, moyoni mwangu najiona kuwa Mimi ni Mtanzania, najua upendo wenu kwa Koffi na mnajua upendo nilionao kwa Watanzania, Dr.Magufuli alikuwa ni Rais wangu pia ndio maana naumia”- Koffi
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na Waombolezaji wengine wakitoa heshima zao za mwisho kwa Hayati Dr.John Pombe Magufuli kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza leo.
Tayari mwili wa Hayati Dr.John Pombe Magufuli umeshaagwa katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza na sasa safari inaendelea kuelekea Chato huku Watu wakiwa wamejipanga Barabarani kwa wingi ili kuuaga mwili.