“Naomba kuungana na kauli ya Rais wetu Mama Samia, Watanzania tuendelee kushirikiana, kuzidisha upendo, umoja na mshikamano miongoni mwetu huku kila mmoja kwa imani yake tukiendelea kumuombea Mpendwa wetu kwa Mwenyezi Mungu”- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye shughuli za kumuaga Hayati Magufuli
“Watanzania, naomba tuendelee kutenda mema, nasi Viongozi tutaendelea kuendeleza yote aliyotenda na kubuni yenye muelekeo wa mambo aliyoyafikiria Rais Magufuli kuwa yataifikisha Tanzania mahali pazuri”- MAJALIWA
“Nawashukuru sana Madaktari na Watu wa Msalaba Mwekundu waliojenga vibanda vya huduma ya kwanza na kutibu waliofikwa na matatizo ya kiafya huko Dar es Salaam na maeneo mengine wakati wa kumuaga Mpendwa wetu”- MAJALIWA
“Nawashukuru Vyombo vya Habari kwa kazi ya kuwaelekeza Watanzania kila hatua ya matukio ambapo Watanzania wote sasa wamepata uelewa wa ratiba ya kumuaga Hayati Rais Magufuli”- MAJALIWA
RIPHayatiMagufuli
View attachment 1731795