Makapuku Forum

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa ni sehemu tu y Wakuu wa Mikoa walioko hapa uwanja waJamhuri kumuaga Hayati Rais Dkt John Magufuli

Hawa ni sehemu tu (tunatambua mchango wa viongozi wote) ya walioaminiwa na Hayati Rais Magufuli kuhakikisha mikoa ya Tanzania inapata maendeleo kwa kasi na ufanisi. Ni wajibu wao na viongozi wote waliobaki kuhakikisha ndoto ya Hayati Rais Magufuli inaendelea kuishi

 
Rais Mstaafu wa awamu ya 4, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndiye alimpasia kijiti cha Urais Hayati Dkt John Pombe Magufuli anaomboleza na watanzania hapa uwanja wa Jamhuri Dodoma
 
"Wengi tulitamani Dk John Magufuli kuendelea kuwa nae kimwili lakini kifo hakizoeleki na wala hakizuilika. Hatuna budi kukubali mapenzi ya Mungu kuwa alitoa na sasa ametwaa," Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

RIPMagufuli
 
Viongozi mbalimbali wa Kimataifa wakiwemo Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa wamefika kwenye shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

 
JPM ALIJENGA VIWANDA 8477

"Hayati John Magufuli alikuza sekta ya viwanda kwa kuhamasisha ujenzi wa viwanda vidogo vya kati na vikubwa nchini ambapo Idadi ya viwanda vipya vilivyojengwa katika kipindi cha utawala wake vilifikia elfu 8477" Profesa Palamagamba John Kabudi.

KutokaDodoma
PumzikaBaba
 
TANZANIA; UCHUMI WA KATI

"Mwaka 2020 Hayati John Magufuli aliifanya Tanzania kuingia kwenye kundi la nchi zenye uchumi wa kati miaka mitano kabla ya muda uliopangwa mwaka 2025 na kuongeza fursa za kiuchumi na biashara kwa makundi mbalimbali hususani Watanzania wenye kipato cha chini" Profesa Palamagamba John Kabudi.

KutokaDodoma
PumzikaBaba
 
JPM KWENYE SIASA; ALIPENDWA

"Mwaka 1995 aligombea ubunge na kushinda katika uchaguzi Mkuu wa vyama vingi katika jimbo la Bihalamuro Mashariki, mwaka 2000 aligombea tena ubunge katika jimbo hilo alipita bila kupingwa kutokana na kupendwa na wapiga Kura wake, 2005 alishiriki tena kugombea tena jimbo hilo kwa sababu za kupendwa alipita bila kupingwa na kuendelea kuwa Mbunge, mwaka 2010 aligombea ubunge jimbo la Chato aliendelea kupita bila kupingwa mwaka 2015 aligombea Urais na kushinda" Profesa Palamagamba John Kabudi.

KutokaDodoma
PumzikaBaba
 
Mh!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…