Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe, ametoa maelekezo kwa Uongozi wa Shule ya Msingi Toangoma, pamoja na Uongozi wa Kata, kuchukua hatua za haraka kukomesha vitendo vya uvunjifu wa maadili vinavyodaiwa kukithiri katika Shule hiyo.
Gondwe ametoa maelekezo hayo alipotembelea Shuleni hapo kwa lengo la kupata ukweli wa kile kilichoripotiwa na Vyombo vya Habari kuhusu kukithiri kwa vitendo vya ngono ambapo ametoa siku saba kwa Uongozi wa Shule na wa Kata kuweka mikakati ya pamoja kwa kushirikiana na Uongozi wa Mtaa ili kwa pamoja wakubaliane ni kwa namna gani vitendo hivyo vitakoma.
Gondwe ameagiza kufukuzwa Shule kwa Wanafunzi watatu ambao wamethibitika kuwa vinara wa vitendo hivyo viovu pia ameagiza kupigwa kwa kura ya siri kwa kila darasa ili kuwabaini wanafunzi wote wanaojihusisha na vitendo hivyo na baada ya kuwabaini wafanyiwe uchunguzi wa kitabibu kuthibitisha tuhuma hizo.
Amesema baada ya kuthibitisha Wazazi wao waambiwe kwa uwazi na hatua stahiki za kitabibu zichukuliwe kwa wale walioathiriwa kiafya na kisaikolojia, na kwa wale vinara hatua kali za kisheria zichukuliwe ikiwemo kuondolewa Shuleni.
View attachment 1727296